Acha hizo mzee mwenzetu, tumefika hapa tulipo kama taifa kwa sababu ya UNAFIKI. Unafiki umekuwa kama ugonjwa wa kuambukiza na muda umefika wa kuiita kolea kwa jina lake na si kijiko kikuubwa!
Hii ni JF where we dare, remember? Umesahau jinsi baadhi yetu nyakati zote tumemkoma nyani giledi bila kumuangalia usoni? Hizo siasa zako kwa sasa zimepitwa na wakati...Unafiki basi, CCM has to go!
Kwanza nitoe shukran zangu kwako kumbe bado mpo? Mkuu nadhani unakumbuka sana kwamba mada nyingi zamani mlikuwa mnakataa mwisho wa siku mnakutana na ukweli nilousema. Toka wakati ule kina Zitto, January, Maria Sarungi, Kitila, Nape, Mnyika wakiwa hapa mara nyinti nilikuwa upande msoupenda.
Sasa kumkoma nyani sii lazima iwe Mbowe wakati najua fika Lissu ndiye hafai kuwa Kiongozi bali ni Mwanaharakati na wakili mtetezi wa hata Jambazi. Lissu anaweza mtetea jambazi alokamatwa na nyala za Serikali na akashinda kesi. Ni mjuzi wa kujenga hoja za UONGO na akashinda.
Mimi mwananchi siwezi kutetea Ushindi huo, nitasema Ukweli ninao uona na naoujua. Siandiki kitu kama sina hakika nacho. Niliwahi sema humu zamani kuwa namjua Lissu kuliko mnavyodhania. Alisomeshwa Marekani na LEAT ambayo wafadhili wake ni Ford Foundation ni tapeli mpenda sifa na majivuno kuwa yeye ndiye Alfa na Omega hakuna zaidi yake.
Hata wakati wa Magufuli, Lissu alipinga Sheria mpya ya mikataba ya madini na nishati akisema mikataba hiyo ni ya Kimataifa hatuwezi kuivunja. Lakini haada ya mwendazake akarudi nchini tukaanza kudaiwa madeni hayo ili mradi tu muendelee kumchukia Magufuli - Nawaelewa.
Kule west Bukina Faso, Chad, Mali n.k wamefuta mikataba ya zamani, wamekubali kulipa madeni yote, leo wako HURU na mfano bora kwa viongozi wa KiAfrika kila mtu anawaona hawa ndio Viongozi tunaowataka.
Senegal inafuata na baadhi ya nchi chini ya Wafaransa wanafuata njia hiyo ya Magufulification. Huku kwetu sisi ni malumbano tu wenyewe kwa wenyewe. Haya kama sii matunda ya Umaskini na Ujinga kitu gani kimetusibu?