Uchaguzi sina tatizo nalo isipokuwa ukiwasikia madai yao ndio utajua ni kampeni. Mgombea ni Lissu kwa nini kila mtu anataka Mbowe aondoke, sijui asigombee, mara mla rushwa, Mbowe ni CCM!
Kweli ndio denokrasia inavyotakiwa? Kwa nini Tundu Lissu asingeweka nia ikaisha bila kuwa na kundi la washabiki nyuma kummaliza kisiasa hata kabla ya Uchaguzi wenyewe? Halafu yanayozungumzwa sii kwamba mapungufu ya itikadi, sera wala misimamo ya Chama bali MBOWE hafai, Mbowe CCM, mzee n.k. Chama cha Siasa hakiongozwi kwa mihemko ya Wanaharakati bali huongozwa na Wanasiasa. Kugombea Urais shauri jingine lakini sio timu moja kumnanga captain wenu. Lissu anazungumza kama Wakili mwanasheria na kesi ya Mbowe ipo mahakamani, kitu ambacho kinaharibu kabisa Demokrasia
.