Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani?

Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani?

Jibu hoja, sio kunishambilia mimi, nina haki ya kusema, kuhoji na kuuliza kama ulokuwa nayo wewe unayempigia chabu Lissu.
CHadema ilipoteza Wanachama wengi wakati yeye akiwa mgombea wa Urais, mkasema wamehongwa na CCM, leo mmebadilika ni kwa sababu ya Mbowe, kwa nini isiwe sababu ni Lissu aloshindwa Urais akakimbia nchi?
Baada ya uchaguzi wa 2020, CDM chini ya Mbowe ilikataa kupokea ruzuku kutoka serikalini. Kwa zaidi ya miaka miwili imekuwa ikijiendesha kwa mapato na michango yao wenyewe. Na badala ya kufa kama wahasimu wao walivyotegemea kikazidi kupanuka. Mbowe akafunguliwa kesi ya ugaidi. Kijana mmoja akawa anaenda mahakamani siku zote na kutoa taarifa almost verbatim yaliyokuwa yakijiri Mahakamani. Wakina mama wa Bawacha wamepigwa na kutupwa rumande kwa kupigania Mwenyekiti wao asitoke. Leo wote hao wanataka kutuambia kuwa walikuwa machawa!

Yericko alisema Lissu alinyang'anywa u anasheria Mkuu kwa sababu alikuwa haitishi vikao na utendaji mbovu. Mpaka leo hawajajibu shutuma hizo.

Lissu alikuwa manhandled Mbeya na akamtaja mpaka aliyehusika. Akaahidi kuwa atamshughulikia kama mtu binafsi. Mpaka leo kimyaaaa.

Amandla....
 
Waswahili wanasema "Akili ni nywele kila mtu ana zake" Najiuliza hii timing ya Mgogoro wa Chadema inaashiria nini wakati kumebakia miezi 10 tu kufikia Uchaguzi Mkuu wa Taifa?

Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani wakati ambao Chama kinatakiwa kuwa pamoja wakipanga mikakati ya Uchaguzi Mkuu ujao?

Kama Mbowe mzee na hafai kuongoza, wamejua haya toka lini? Kwa nini sasa hivi sio mwaka juzi, jana ila leo ndio imekuwa hoja ya msingi kufanya mabadiliko ndani ya Chama. Hivi wakimundoa Mbowe madarakani ndio wataweza kumkabiri vema Mama Samia na CCM hiyo November 2025 kupitia sera gani? Maana Kama Chadema haikufanya vema chini yake, je wale Wagombea Urais waloshindwa walikuwa Chaguo la nani, Mbowe?

Nikiitazama safu ya wapambe wa Tundu Lissu ni kundi la wanaharakati wanaodai TANGANYIKA HURU kwa sababu hawaridhiki na Uongozi wa Mama Samia. Na wala tusidanganyane ya kwamba mpango wa kumuondoa Mbowe madarakani umetokea ghafla.

Nina hakika Ulikuwepo na ulipangwa sawa kabisa na ule wa kina Zitto 2013. Tofauti ni kwamba kina Zitto waligunduliwa mapema na hawa kwa usiri mkubwa wameweza fikia hatua ya mwisho. Pengine walijifunza yalowakuta kina Zitto na Kitila.

Niliwahi kusema rasimu ya Warioba ilishindikana kutokana na madai ya Serikali 3. Na nazidi kusisitiza kuwa haitawezekana kurudiwa Rasimu ya Warioba kupitia madai yale yale ya Kudai Serikali ya Tanganyika. Kama Chadema itasambaratika basi Tanzania itabakia imara kwa kulindwa na KATIBA hii hii.

Binafsi sielewi kina Lissu na Heche wana Mpango gani lakini niseme tu kwamba sasa hivi CCM wanatafuna popcorn huku wakisukumiza na juice baridiii kwa mrija. Sinema ya Mdudu ndio kwanza imeanza.

Maasalam.
Mbuyu umedondoka hatimaye.
 
Back
Top Bottom