Miaka inashirini na moja ni mingi sana. Hata kama wewe ni baba mtoto wako wa mwisho akifikisha miaka 21 inakuwa ni wakati sahihi wa kuaanza kuwapa watoto majukumu yako. Kwanza kwa kiongozi mwenye akili hawezi kukaa kwenye nafasi moja kwa zaidi ya miaka ishirini. Hata Salum kikeke alivyo ona amekaa BBC kwa mda mrefu aliamuwa kuondoka. Sasa Mbowe ni kitu gani kinamfanya aendelee kung"ang'ania uenyekiti ? Kama kweli niya yake ni kuleta mabadiliko ya kisiasa kwa manufaa ya watanzania anaogopa nini kumpa mtu mwingine jukumu hilo.
Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa TAA toka mwaka 1953, Chama kikabadili jina na kuitwa TANU mwalimu bado akawa Mwenyekiti, wakabadilisha tena jina kuwa CCM, Nyerere aliendelea kuwa Mwenyekiti na wala hakujiuzuru Uenyekiti 1984 bali alijiuzuru Urais, akaendelea kuwa Mwenyekiti kwa mwaka mmoja au miwili kabla Ally Hassan Mwinyi hajachukua Uenyekiti wa Chama kulingana na mfumo wa Uongozi wa CCM.
Sasa labda nikuulize wewe kwa nini Mwalimu alikuwa Mwenyekiti wa Chama kwa miaka zaidi ya 30? Ukiweza nambia sababu nitarudi tuendelee na mjadala.. Kisha hii sio hoja yangu mimi pengine hamuwezi kusoma hoja zangu mnachukua maelezo kama yalivyo na kuongeza yenu juu yake.
Hoja yangu ni hii, Kwa nini Viongozi wa Chadema wanavuana nguo hadharani kwa TUHUMA NZITO ambazo zingeweza shughulikiwa toka miaka ilopita (2021/22 - 2024) kupitia vikao vya ndani vya Chama? Kama Mbowe ni CCM walishindwaje kumuondoa karika Uchaguzi uliopita ama kuitwa na kamati ya maadili kujibu tuhuma hizo ila wamesubiri Uchaguzi unakaribia na Uhasama kuanza kutokea baina ya Wagombea?
Lissu kaeleza wazi kwa nini anagombea Uenyekiti ni Kumkomoa alomtuma Wenje kugombea Umakamu. Hii statement pekee inawapeni picha gani kama sio katangaza vita ya wenyewe kwa wenyewe?
Hivi UMAKAMU ilikuwa nafasi yake peke yake au? na kwa nini anasema tena bila aibu wala kuficha ati alikuwa na Kikao cha siri baina yake na Mbowe ili kugawana nafasi za kugombea? Mbowe alikataa akisema bado hajaamua - Hii kweli ndio Demokrasia?
Wakati Vyama vya Siasa nchi nyingine wanapanga mbinu kujua Strength na Weekness za Chama tawala, Chadema wanapambana wenyewe WHY?
Nikidhani Uongozi wa Chama ni KUJITOLEA, hii vita ya nini? Ina maana moja tu, KUNA ULAJI ndani ya Uongozi wa Chama. Na kama Mbowe kweli hupokea FEDHA kutoka CCM kukiendesha Chama ama zake, basi bila shaka hao wengine pia wanataka kupokea hizo FEDHA maana wanajua zinatokaje kwa Ushahidi walonao.
Vita ya Chadema sio MBOWE wala LISSU bali vita ya Chadema ni CHUMIA TUMBO hali ambayo haikuwepo miaka mingi nyuma and it seems Viongozi wengi hawana source of income baada ya kukosa Ubunge, imebakia ndani ya Chama kuna vijisenti vinatembea. That's my perception na huu utakuwa mwisho wa Chadema kama Chama Kikuu cha Upinzani.