Nini hasa lengo la harakati hizi za kumuondoa Mbowe madarakani?

Binafsi sielewi kina Lissu na Heche wana Mpango gani lakini niseme tu kwamba sasa hivi CCM wanatafuna popcorn huku wakisukumiza na juice baridiii kwa mrija. Sinema ya Mdudu ndio kwanza imeanza.
Nilipoona ID yako nikafurahi kwa kujua uwezo wako wa kuchambua hoja tangu enzi zile za 'nondo za moto'....kumbe hola!!

Hili hitimisho limeweka dhahiri wewe ni ccm unayetaka FAM abaki uongozini kwa maslahi yenu mnayoyajua wenyewe.⁹
 
lengo kuu ni ili wapate mtu ambaye hatakuwa analamba asali. uwepo upinzani halisi utakaoiwajibisha serikali inayouza nchi kwa mwarabu.
1. Una hakika Lissu haonji Asali? Kama Lissu hana Biashara, hana Ubunge, hana hata Usafiri wake anaishije mjini? Naomba nambie source ya Imcome ya Tundu Lissu happ mjini.
2. Ya Abdul ukisikiliza kwa makini utetezi wa Lissu unajua wazo alikuwa anamjua ana amekuja nyumbani kwake kufanya nini!
3. Kisha sio Lissu alokutana na Mama Samia Ubelgiji? Waliongea nini hadi karudi Tz, TISS wasimguse maana alisema Usalama wa Taifa walitaka kumuua.
4. Usalama wa Taifa wanaweza kweli futa kesi zao ikiwa kuna hatari ya Usalama wa nchi? Ghafla tunaona Lissu analiamsha ndani ya Chadema muda huu ambao Chadema wanajipanga kuikabiri CCM.
5. Ebu wewe nipe time line yaani pale ashinde au ashindwe Lissu Uenyekiti kutakalika?
 
unauliza swali hilo kwa mtu aliyekuwa mbunge miaka mingi sana, na hela za ubunge alizokuwa amezuia ndugai alilipwa zote, unafikiri aatalala njaa? au unataka tusemeje?
 
Nilipoona ID yako nikafurahi kwa kujua uwezo wako wa kuchambua hoja tangu enzi zile za 'nondo za moto'....kumbe hola!!

Hili hitimisho limeweka dhahiri wewe ni ccm unayetaka FAM abaki uongozini kwa maslahi yenu mnayoyajua wenyewe.⁹
U CCM wala Uchadema niliisha acha siasa siku nyingi maana niliona Siasa za Bongo ni sawa na debe linalovuja. Watu wakipenda hawaoni chongo
 
unauliza swali hilo kwa mtu aliyekuwa mbunge miaka mingi sana, na hela za ubunge alizokuwa amezuia ndugai alilipwa zote, unafikiri aatalala njaa? au unataka tusemeje?
Alaaa alipewa na nani?
 
Wale Team Lisu wanajiona wana uwezo mkubwa sana kifikra kumbe ni kakikundi kadogo kaliko jawa na wivu, na uchu wa madaraka wanayohisi watayapata kupitia Lisu, waliyakosa kuputia Mbowe.

Nashauri kamati kuu ikimjadili Lisu na wapiga kelele wenzake wamfukuze kutoka chamani, ilu wapate fursa kuanzisha na kusajiri chama chao cha harakati.

Wanajivunia chadema kwasababu ya uongozi mahili wa FAM, Wakichukua chama kina kufa, na ndiyo nia yao hawa mahodari wa kuongea bila mipaka.
 
Member since 2006 hajui kwa nini mwaka juzi na mwaka jana hakukua na kumuondoa mbowe kwenye uenyekiti. Sijui wangemuondoa vipi bila uchaguzi

Hata hivyo mbowe mwaka 2021 alisema hatagombea tena uenyekiti
 
U CCM wala Uchadema niliisha acha siasa siku nyingi maana niliona Siasa za Bongo ni sawa na debe linalovuja. Watu wakipenda hawaoni chongo
Kwa maswali yako uliyouliza na hiki umeandika hapa, wewe ni mlongo
 
Lengo chama kirudi katika mstari wake kupitia mawazo mapya , wala sio kwamba mbowe hajafanya makubwa
 
Mzee mkandara umeamua kuja kupima upepeo Kama Mbowe bado anafaa .

Huyo mtu wenu hana nafasi tena
 
hata kama alipewa na samia, si ilikuwa halali yake? unataka afumbe mdomo kwa sababu alipewa haki yake na samia? au
Sheria ya Bunge inasemaje ikiwa mbunge akifutwa Ubunge?
Kabla sijakujibu....nini lilikua lengo la FAM kuhakikisha LISSU anakoswa Umakamu??.
Hayo ni madai ya Lissu anatapatapa tu. isikilize vizuri hotuba yake kisha jiulize what if ni Wenje aloomba ushauri kugombea, ulitaka Mbowe aseme usigombee? Kwani nafasi hiyo imezuiwa kugombewa isipokuwa Lissu peke yake?
Na kwa nini Lissu aseme Mbowe alimtuma agombee nafasi yangu basi na mimi nagombea nafasi ya huyo alomtuma!
Huoni kama ni Uchizi huo?
 
Mbowe kataka mwenyewe kuondolewa madarakani, kwa kujifanya yeye ni Masta wa siasa na propaganda, Anajifanya yeye ndo mpanga safu ya uongozi Chamani

Safari hii kakutana na kisiki
 
Hakuna mpango wowote wa kumuondoa Mbowe madarakani, kinachoendelea ndani ya CHADEMA ni kufanya uchaguzi wa kupata viongozi wa kuendesha chama kipindi kinachofuata baada ya kipindi cha Mbowe kwisha. Hiyo ni fursa inayotolewa kwa mwanachama yoyote yule, sio lazima awe Mbowe au Lissu.
 
Mwamko wa raia dhidi ya hadaa za watawala kupitia kivuli cha vyama kupitia mapandikizi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…