Nini hasa maana ya utu?

Nini hasa maana ya utu?

Mimi sina tafsiri wala definition ya utu. Siijui. Na siondoi uwezekano wa kuwa huo utu wenyewe sina au ulishapotea kitambo.

Napenda sana mtu anapojibu swali moja kwa moja laivu bila ya chenga. Nimelipenda hili jibu lako!

Utu ni nini?

Kwa ufahamu wangu mimi, utu ni ubinadamu na yale yote (ya kistaarabu na kiungwana) yanayotufanya binadamu tuwe tofauti na wanyama wengine (kuna mtu aliwahi kuniletea ligi eti binadamu siyo wanyama - nje ya JF lakini).

Na ndiyo maana, kwa mtazamo wangu mimi, fasili (definition) ya utu inaweza kuwa tofauti baina ya mtu na mtu, watu na watu, na muktadha na muktadha.

Kwa hiyo sidhani kama utu una fasili iliyosimama. Fasili yake iko kimuktadha zaidi.

Kwa ufahamu wangu mimi, utu ni ubinadamu na yale yote (ya kistaarabu na kiungwana) yanayotufanya binadamu tuwe tofauti na wanyama wengine (kuna mtu aliwahi kuniletea ligi eti binadamu siyo wanyama - nje ya JF lakini).

Mkaribishe asome 'The third Chimpanzee' ......lazima akasirike na mtunzi :]
 
Naomba jibu hapo toka kwa members for i am interested on how different or Similar itakua for most members hapo.... Hasa wewe mwenyewe Cathode Rays....

Hello AD, samahani kwa kuchelewa kurespond nilikuwa safarini these last two days and it was for some busy thing hata laptop sikuweza kuigusa

All in all, unaweza kunisaidia kulifafanua hili swali vizuri kujua ni nini unataka kufahamu?

Thanks
 
@RussianRoulette,

This is one of the best things i have read here at Jf.
Cannot agree with you more. Utu ni Utu,...the lesser we define it, the more sense it makes.
It is something we feel and have a positive contribution to whoever the Utu is exercised on. Period!
 
Mkuu APRIL

Baada Ya RR, Wewe ni Mtu wa Pili ambaye naguswa kabisa na maono yenu!

Kwani by the time MTU anapoouliza SWALI ... UTU NI NINI!! Hicho kinachouliza ni NINI? Huo ufahamu wa kuelewa hadi kujenga hilo swali ni nini? Hilo swali litatoka wapi kama sio kwa UTU wenyewe?

Ndio maana mwanzoni kabisa nikasema ....Tumbili anaweza kuuliza utu ni nini, lakini sio Mtu. Mwanadamu ataulizaje asili yake? Tumbili hakuumbwa kuwa na Utu, hivyo anaweza kuushangaa, kuulizia na kutaka kuujua. Mtu anayeuliza maana ya UTU ina maana amesha upoteza kwa kuusaliti..yaani amesha upoteza Utanzania!!! ...

Nikatoa pendekezo, Kama is the just for the matter of contemplation and brain storming ... Lets take particular CASE .. and we discuss it ... with respect na dhana ya UTU ... Maana UTU wenyewe is no problem ...Its the one which is discussing!! Its YOU, Its ME!!

Ndio maana huko nyuma nikahoji ...Mfumo mzima wa AZIMIO LA ARUSHA (NI AZIMIO LA UTU??) ..Kama ulikuwa kuujenga UTU kiuchumi, kisiasa na kustawisha jamii.??? That I can dare to discuss. Kwenye Thread nyingine Nikahoja ...KIPI CHA MUHIMU NA MSINGI ZAIDI, Usalama wa Taifa? au Usalama wa UTU wa Taifa!??

Ninaamini kama anavyoamini RR na APRIL ... Kuwa UTU ni UTU na Hakuna asiyekuwa nao ILA kwa Kuamua KUUASI NA KUUTUPILIA MBALI!! Na matendo ya kuuasi Utu wetu ..AU.. Kuuenzi Utu wetu .. HAYO? Yajadiliwe.. Wewe umeusaliti UTU ... Utakuwaje mfanyakazi ndani ya Timu ya USALA WA TAIFA!!? Utasimamiaje UONGOZI wa Taifa wakati umeukana uasili wako? Kwa nini watu waliosaliti Uasili wao ambao ni UTU waachiwe sehemu nyeti kwenye jamii? ... TAFADHALI/Nisiulizwe UTU ni nini ...maana ..Jibu ni kuwa ni hicho kinachouliza ..ndio Utu. Labda tatizo ..muuliza Swali ameusaliti Utu wake huo anaotumia kuulizia ..Utu ni nini ..ndio maana kunakuwa na kutoelewana, Kwani swali limeulizwa kupitia UTU ULIOSALITIWA.. Lakini muuliza swali anao na anaujua ndio maana akachagua kuusaliti!! Utasaliti kitu usichokijua? .. Pale ambapo muuliza swali Utu Ni nini Hajausaliti UTU wake kwa makusudi mazima... Hatakuwa na haja ya kusubiri jibu la UTU ni nini ..kwani .. Swali ndio JIBU!.. Yaani MSUKUMO wa kuuliza swali UTU ni nini, MSUKUMO HUO NDIO UTU!
 
Nimesoma posts zoote, na I like the answers ya most hasa tokana na constructive questions za Gaijin,

@Gaijini hata mimi ningependa your Definition of Utu ....

ADII, ... Looh.. Hongera kwa kusoma Post Zote ..!!
 
Mfano rahisi,
Rejea jinsi nafsi yako ilivyo na utambuzi wa jema na baya. Ukidondosha hela kwa bahati mbaya, mtu akaziokota akakuletea utajua kafanya jambo jema, lakini ukipita mtaa fulani, matharani kariakoo, mtu akakuchomolea hiyo hela mfukoni, unajua kafanya jambo baya. Alichochukua si chake, hajapewa, si halali yake n.k. Wawili hawa waweke katika mizani ya uadilifu na utu.

Kahangwa

Nimeshukuru sana kwani hakika uko kwenye kundi la kuwa UTU ni Utambuzi wa MTU Binafasi. Na Kimsingi MSUKUMO unaohoji UTU ni NINI ..Msukumo huo ndio UTU wenyewe ..!

Najua hatujamaliza kujadili kanununi ya UMUHIMUWAKE ..Lakini hilo litafanyika tu Mkuu! Ila tumalizie kuweka MISIGI yake! ..Nauliza huu msukumo wa WATU kuuliza na kuonekana kutokuulewa UTU NINI ... unafikiri .. Hili ni Tatizo linalojitegemea au .. KHERI!!?
 
Hello AD, samahani kwa kuchelewa kurespond nilikuwa safarini these last two days and it was for some busy thing hata laptop sikuweza kuigusa

All in all, unaweza kunisaidia kulifafanua hili swali vizuri kujua ni nini unataka kufahamu?

Thanks

AshaDii

You wont mind kukumbusha kufafanua!!
 
Kwa ufahamu wangu mimi, utu ni ubinadamu na yale yote (ya kistaarabu na kiungwana) yanayotufanya binadamu tuwe tofauti na wanyama wengine (kuna mtu aliwahi kuniletea ligi eti binadamu siyo wanyama - nje ya JF lakini).

Nahoji. Nani asiyejua hicho kilichosemwa hapo juu ... hadi kiliposemwa ndiopo akajua!?

Unachotaka kusema ni nini sasa?
..
FLY,

Nilitumia matamshi yako kusisitiza dhana kuwa kila mwanadamu ana UTU. Kila mwanadamu anaujua UTU kama ulivyouelezea kwenye matamshi yako. Na ninaamini kuwa kila mwanadamu anauwezo kuusaliti UTU wake kama anataka... na Yule aliyeamua kuweka kando Utu wake , yule aliyeamua kuusaliti UTU wake .. Atatafsriwa kwenye Matendo yake, fikra zake na matamshi yake ..Kama MTU asiye na UTU. .. na Labda kufananishwa na Mnyama.

Nilipo hoji nani haelewi ulichosema .. nilikuwa namaanisha kuwa hakuna Mtu mwenye UTU ambaye haoni na kuelewa kama ulivyojieleleza dhana nzima ya UTU.... kwani huo ndio ukweli. Ambaye haoni hivyo ni nani? Na kwa nini asione hivyo? Kwa mtizamo wangu, Jibu langu ni kuwa ni kwa sababu ..ameusaliti Utu wake tayari ..kwani ... Ulichoandika kinasimami ni asili ya kila mwanadamu mweneye UTU. Na Kuelewa ulichoandika kingekuwa kitu cha kawaida tu!!
 
Sorry guys, I haven't ignored you. I have been offline for the last few days due a reason beyond my control. Asanteni nyote kwa kuendeleza mjadala. Mtaani nilijikuta niko kwenye dabate na wanamtaa wakibishana kuwa kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka nje ya bunge wakati wa majadiliano ya ule mswada wa Katiba, kulikuwa sio kitendo cha utu.

Niliwauliza baadhi ya maswali aliyouliza Gaijin kwenye hii thread lakini sikupata jibu. Walionyesha kuutambua utu lakini ku-udefine walishindwa. Wapo waliosema kuwa mtu ni utu. Wengine walisema kazi ni utu na kwa vile wabunge wa Chadema walisepa kazi yao, then walikosa utu. Wengine walisema Chadema wameonyesha utu kwa Watanzania, lakini CCM hawakufanya hivyo kwa vile waliweka mbele interests za chama chao badala ya watu ambao ndio utu.
 
Aisee umefafanua hadi nimefurahi!

Na hivi utu kwa Kiingereza si ndo humanity, humane, na kukosa utu ndo inhumane?
 
Aisee umefafanua hadi nimefurahi!

Na hivi utu kwa Kiingereza si ndo humanity, humane, na kukosa utu ndo inhumane?

Huko nyuma Mkuu Paulss alitafsiri "utu" kama "humaniniy". Nae Mkuu Cathode Rays alitafsiri "utu" kama "dignity".
 
Huko nyuma Mkuu Paulss alitafsiri "utu" kama "humaniniy". Nae Mkuu Cathode Rays alitafsiri "utu" kama "dignity".

Dignity na utu? Daah

Dignity si inahusiana na heshima na taadhima? Au nimekosea?
 
Dignity na utu? Daah

Dignity si inahusiana na heshima na taadhima? Au nimekosea?

Mie nadhani humanity ni ubinadamu.
Wengine wanasema ubinadamu ndio utu wenyewe.
Kwa mfano, crimes againist humany ina maana makosa ya jinai dhidi ya utu?
Dignity sio hadhi?
 
Sorry guys, I haven't ignored you. I have been offline for the last few days due a reason beyond my control. Asanteni nyote kwa kuendeleza mjadala. Mtaani nilijikuta niko kwenye dabate na wanamtaa wakibishana kuwa kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka nje ya bunge wakati wa majadiliano ya ule mswada wa Katiba, kulikuwa sio kitendo cha utu.

Niliwauliza baadhi ya maswali aliyouliza Gaijin kwenye hii thread lakini sikupata jibu. Walionyesha kuutambua utu lakini ku-udefine walishindwa. Wapo waliosema kuwa mtu ni utu. Wengine walisema kazi ni utu na kwa vile wabunge wa Chadema walisepa kazi yao, then walikosa utu. Wengine walisema Chadema wameonyesha utu kwa Watanzania, lakini CCM hawakufanya hivyo kwa vile waliweka mbele interests za chama chao badala ya watu ambao ndio utu.

Kweli Mkuu you left suddenly ... and we needed someone to chair KIGODA CHA UTU!! .. Glad you have come back!!
 
Mie nadhani humanity ni ubinadamu.
Wengine wanasema ubinadamu ndio utu wenyewe.
Kwa mfano, crimes againist humany ina maana makosa ya jinai dhidi ya utu?
Dignity sio hadhi?

Hmm...mengine yatakuwa lost in translation hapa lol..

Ukianza kutafsiri neno kwa neno toka Kiingereza kwenda Kiswahili unaweza usipate maana sahihi. Na nadhani ndicho ulichofanya kwenye hiyo tafsiri yako ya crimes against humanity. Angalia hata muundo wake ulivyo.

Hadhi siyo status? Kwangu hadhi inakaribiana zaidi na status kuliko dignity.
 
Sorry guys, I haven't ignored you. I have been offline for the last few days due a reason beyond my control. Asanteni nyote kwa kuendeleza mjadala. Mtaani nilijikuta niko kwenye dabate na wanamtaa wakibishana kuwa kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka nje ya bunge wakati wa majadiliano ya ule mswada wa Katiba, kulikuwa sio kitendo cha utu.

Niliwauliza baadhi ya maswali aliyouliza Gaijin kwenye hii thread lakini sikupata jibu. Walionyesha kuutambua utu lakini ku-udefine walishindwa. Wapo waliosema kuwa mtu ni utu. Wengine walisema kazi ni utu na kwa vile wabunge wa Chadema walisepa kazi yao, then walikosa utu. Wengine walisema Chadema wameonyesha utu kwa Watanzania, lakini CCM hawakufanya hivyo kwa vile waliweka mbele interests za chama chao badala ya watu ambao ndio utu.

EMT

Kuhusu Mjadala wa dhana ya UTU kwa Kuchambua Tukio hali la kijamii kama la CDM kutoka nje ya Mjengo ... Navutiwa na mjadala huo sana na nafikiri kwa namna hiyo ni kutendea haki ... Mjadala unao endelea hapa wa UTU NI NINI! Nasema hivyo kama contrast ya Kuchambua dhana ya UTU kwa kama CONCEPT! Utakumbuka huko nyuma nilipendekeza .. tusione aibu ... na tuwe wazi kabisa ..Kila mchangiaji ajitambulishe kuwa yeye yuko kambi gani.

1. Kutaka kujua UTU kama CONCEPT .. Mifano ni hizo definition nyingi kuanzia post ya kwanza hadi tutakapofikia Post ya Mwisho ..Na Gaijin ... atasikilizaaa atachangia na mwisho atauliza ..UTU NI NINI?

au

2. Kutaka kujua TUKIO fulani limejengwa na UTU au halikujengwa na UTU ... mfano ni kama huo wa CDM kutoka mjengoni.

Tujadili tukio hilo ili kufafanua dhana ya UTU ...

Na Kama Utaona inafaa Unaweza kutuogoza siku zijazo tukachambua kwa undani Dhana ya UTU Kupitia Watu mashuhuri na matukio muhimu ya kijamii. Kwa mfano

1. Katia ya Id Amin na Nyerere ..nani alikuwa na sifa ya Utu zaidi ya mwingine ...Na kwanini?
2. Kwa Hivi sasa Ni Kiogozi gani wa Tanzania anaweza kuchukuliwa kutekeleza kwa dhati Dhana ya UTU .. Kisiasa na Kiuchumi
3. Ni Kweli hawa ni mifano mizuri ya Utu? Nelson Mandela, Mahatma Ghandi, Osama Bin Laden, Jakaya Mrisho Kikwete, Edward Ngoyai Lowasa
4. Matukio haya ya Kitaifa yamesimamia dhana ya Utu na Ubinadamu: Siasa ni Kilimo, Fagio la chuma, Azimo la Arusha, Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania, Vua Gamba, Tuweke Mwenge wa uhuru Kilimanajaro, CDM kukutanan na Rais wa Jamhuri Ya Muugano wa Tanzania Kuhusu Katiba.
5. Tujadili Kati ya JAMBO FORUMS na JAMII FORUMS ... Ipi .. Imejikita Kwenye Dhana ya UTU zaidi na kwa nini?
 
Mtizamo wangu kuhusu CDM kutoka Mjengoni!

Kwa hakika kabisa lazima kutakuwa na MITIZAMO ya aina mbili!

Wale amabo hawana tatizo na Utu wao , watautabua na kuuenzi hivyo watautumia kuchambulia matukio ya maisha. Wata dhubutu kuona ukweli kuhusu tukio lile kwa misingi ya Utu na matokeo yake katika kustawisha jamii.

Kundi la Pili, kama alivyosema RussianRoulette (kama nilimuelewa vizuri) .. Kundi hili linaamua kuuweka Utu wao kando na sio kwamba haliujui Utu ..lakini kwa sababu ambazo labda zitakuwa wazi baadae wanaamua kuusali Utu ambao ndiyo asli yao inayowataofautisha na wanyama na vitu vingine vyote..hawa wataliona tukio lile kwa namna yao!!

Kwa sasa naishia HAPA!!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom