Sorry guys, I haven't ignored you. I have been offline for the last few days due a reason beyond my control. Asanteni nyote kwa kuendeleza mjadala. Mtaani nilijikuta niko kwenye dabate na wanamtaa wakibishana kuwa kitendo cha wabunge wa Chadema kutoka nje ya bunge wakati wa majadiliano ya ule mswada wa Katiba, kulikuwa sio kitendo cha utu.
Niliwauliza baadhi ya maswali aliyouliza Gaijin kwenye hii thread lakini sikupata jibu. Walionyesha kuutambua utu lakini ku-udefine walishindwa. Wapo waliosema kuwa mtu ni utu. Wengine walisema kazi ni utu na kwa vile wabunge wa Chadema walisepa kazi yao, then walikosa utu. Wengine walisema Chadema wameonyesha utu kwa Watanzania, lakini CCM hawakufanya hivyo kwa vile waliweka mbele interests za chama chao badala ya watu ambao ndio utu.
EMT
Kuhusu Mjadala wa dhana ya UTU kwa Kuchambua Tukio hali la kijamii kama la CDM kutoka nje ya Mjengo ... Navutiwa na mjadala huo sana na nafikiri kwa namna hiyo ni kutendea haki ... Mjadala unao endelea hapa wa UTU NI NINI! Nasema hivyo kama contrast ya Kuchambua dhana ya UTU kwa kama CONCEPT! Utakumbuka huko nyuma nilipendekeza .. tusione aibu ... na tuwe wazi kabisa ..Kila mchangiaji ajitambulishe kuwa yeye yuko kambi gani.
1. Kutaka kujua UTU kama
CONCEPT .. Mifano ni hizo definition nyingi kuanzia post ya kwanza hadi tutakapofikia Post ya Mwisho ..Na Gaijin ... atasikilizaaa atachangia na mwisho atauliza ..UTU NI NINI?
au
2. Kutaka kujua
TUKIO fulani limejengwa na UTU au halikujengwa na UTU ... mfano ni kama huo wa CDM kutoka mjengoni.
Tujadili tukio hilo ili kufafanua dhana ya UTU ...
Na Kama Utaona inafaa Unaweza kutuogoza siku zijazo tukachambua kwa undani Dhana ya UTU Kupitia Watu mashuhuri na matukio muhimu ya kijamii. Kwa mfano
1. Katia ya Id Amin na Nyerere ..nani alikuwa na sifa ya Utu zaidi ya mwingine ...Na kwanini?
2. Kwa Hivi sasa Ni Kiogozi gani wa Tanzania anaweza kuchukuliwa kutekeleza kwa dhati Dhana ya UTU .. Kisiasa na Kiuchumi
3. Ni Kweli hawa ni mifano mizuri ya Utu? Nelson Mandela, Mahatma Ghandi, Osama Bin Laden, Jakaya Mrisho Kikwete, Edward Ngoyai Lowasa
4. Matukio haya ya Kitaifa yamesimamia dhana ya Utu na Ubinadamu: Siasa ni Kilimo, Fagio la chuma, Azimo la Arusha, Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania, Vua Gamba, Tuweke Mwenge wa uhuru Kilimanajaro, CDM kukutanan na Rais wa Jamhuri Ya Muugano wa Tanzania Kuhusu Katiba.
5. Tujadili Kati ya
JAMBO FORUMS na
JAMII FORUMS ... Ipi .. Imejikita Kwenye Dhana ya UTU zaidi na kwa nini?