Nini hatima ya Wakristo walio Zanzibar kwenye sherehe za Pasaka baada ya zuio la kula mchana wakati huu wa Ramadhan?

Nini hatima ya Wakristo walio Zanzibar kwenye sherehe za Pasaka baada ya zuio la kula mchana wakati huu wa Ramadhan?

Utamaduni wa dini, kufanywa sheria ya nchi, na inabidi ifatwe na kila raia hata ambaye sio mfuasi wa dini,! Na hapa zenj,ni kwa vile wenye dini hiyo ni 90%!
Bara haiwezekani, kwa sababu walee sio majority, na hata wakitaka kuanzisha, upinzani utakuwa mkubwa Sana.
 
Kumbuka tu huo muungano ni wa nchi mbili znz wana katiba yao wana sheria zao kwa znz kula hadharani mchana wa Ramadhani ni kosa la jinai
Why watumike Polisi ambao ni mali ya muungano kwenye kutekeleza sheria zao...?

Katiba ya Jamhuri yasema, hii nchi haina dini...haikutamka Tanzania bara tu
-Sasa je, ipi ni Katiba ya Jamhuri haina nguvu hiyo ndogo...?
 
Wewe kweli ni mtu wa Ajabu sheria zipo za znz wenyewe wazanzibari ndio wameamua hivo unakereka wewe Mkenya ? Pole sana

Zanzibar ni kisiwa cha waafrika, kiko ndani ya nchi ya Afrika na wanaoishi ni Waafrika, hauwezi kutumia pumba za kiarabu kutesa waafrika wenzako, sio kila mtu pale anaabudu huyo muarabu, kuna Watanzania wametokea bara ambao hawahusiani na muarabu.
Ona hii video mlivyo majinga, mnamcharaza mtu viboko kisa kakula chakula ambacho kajinunulia kwa hela yake na jasho lake.

https://www.jamiiforums.com/data/video/5674/5674814-a14818219092ff5b8b26258ca67a71da.mp4
 
Huyo Samia na mwinyi wafanyeje? Hizo sheria zipo znz toka karume mkubwa tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
Lengo ni kuimarisha muungano,
Sasa unafkiri Rais ajaye akiwa wa bara, na akaamua kuvuta kamba huku, itakuwaje kwenu...?
 
Huyu naye mweupe kichwani hajui mambo ya muungano

Polisi Zanzibar wamevunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Polisi ni jeshi la muungano wa Tanzania na linaongozwa na kusimamiwa ba katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye kazi zao.Katiba ya muungamo inatamka wazi. Kuwa mambo ya dini yatakuwa nje ya mambo ya serikali. Hao waliokamatwa wakila hadharani mwezi wa Ramadhani hawajavunja katiba yeyote kipengele chochote cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Polisi Zanzibar ambao ni jeshi linalosimamiwa na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio wamevunja katiba na PGO ya polisi.

Wanatakiwa hao Polisi waburuzwe mahakamani kwa kuvunja katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ambayo ndio wanatakiwa kuisimamia na ambayo ndimo jeshi hilo liko chini yake ya wizara ya mambo ya ndani ya muungano

Wamevunja katiba ya Jamhuri ya muungano hao Polisi.Wamewakamata hao watu kinyume cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania wawaachie
Polisi hawakuwa na mamlaka ya kuwakamata wala kuwashikilia wala kueafungulia mashtaka ya kula urojo hadharani au kutafuna big ji hadharani

Hawana nguvu hiyo kwa katiba ya Jamhuri ya muungano iliyowapa huo upolisi
 
Polisi ni Jambo la Muungano...ina maana wanafuata sheria za Jamhuri.
Je,wana usikaje kukamata watu kwa makosa ambayo kwenye Katiba hayapo...?
Ufafanuzi tafadhali.
Kimsingi hao polisi wanaokamata wananchi kwa sababu tu wamekula chakula wanavunja Katiba, na Katiba ipo juu ya sheria zote..

polisi tanzania njooni huku mtoe ufafanuzi
 
Taifa la Mungu wakati tukijiandaa kusherekea Pasaka siku ya jumapili. Wakirsto waliopo Zanzibar wapo kwenye mtihani mkubwa.

Zanzibar kwa sasa ukila mchana unakamatwa na polisi na kuwekwa ndani.

Je itakuwaje kwenye siku ya Pasaka ambayo inatakiwa waumini wachinje na kula na kusherekea pamoja?

Wameambiwa watu wasile hadharani je kwenye hadhara ni wapi? Ukipika pilau lako unawekwa ndani?

Tumeshuudia watu wamekamatwa sababu wanasafirisha chakula walichoagiza kwa siri kutumia bodaboda hawakuwa wakila barabarani, je sasa hadharani ni wapi?

Ukiwa nyumba za kupanga za kushea huduma je hutakiwi kupika?
Watanzania wenzetu wapo kwenye mtihani mkubwa sana kipindi hiki na kosa lao ni moja tu kutokuwa waamini wa islamic religion. Tuwaombee maana hawana mtetezi huko.
Kumtumikia shetani kwa nguvu....
 
Huyu mama anaota hasomi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala kujua kazi za polisi kwa mktadha wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambalo ni chombo cha muungano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na PGO yao ya Polisi kama chombo cha muungano na kazi zao kitendo cha polisi kukamata hao wala mchana hakiko sahihi kikatiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Huyu mama anaota hasomi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala kujua kazi za polisi kwa mktadha wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambalo ni chombo cha muungano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na PGO yao ya Polisi kama chombo cha muungano na kazi zao
Wizara ya mambo ya ndani ilikuwepo kwenye vile vipengele 11 vya muungano alivyosaini karume,au mliingiza kwa Hila baadae?
 

Attachments

  • IMG_20240205_172029_175.jpg
    IMG_20240205_172029_175.jpg
    36.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom