Kwanza ni kujua aina ya wanaolalamika na uwezo wao kiuchumi. Hii itakuwa rahisi kuwapa location kadili ya ukubwa wa mfuko wao.
Aidha kwa haraka haraka, kama ulikuwa unakula kwa Mama Lishe kabla ya mfungo, ni Mama huyo huyo ambaye hutoa location kwa wateja wake ni wapi atapatika wakati wa mfungo.
Kwa wanywaji, Baa zinazokuwa wazi zinajulikana na zaidi unaweza kupata msosi kama kawaida. Hivyo hili sio tatizo kwao.
Kwa wageni, unapofika bandarini au airport ulizia kwa bodaboda, taxi driver na Bajaj... Hapa hapana guarantee ya kupelekwa sehemu salama.
Zaidi kambi zote za Jeshi zenye Officers Mess wanakuwa wazi, baadhi ya Baa zilizo chini ya CCM, Hotel za kitalii n.k
Kubwa zaidi ni ukubwa wa mfuko wako na Cha muhimu kabisa ni kiheshimu waliofunga.