Nini Hatma ya MCC na AGOA baada ya Trump kuwa Rais wa Marekani?

Nini Hatma ya MCC na AGOA baada ya Trump kuwa Rais wa Marekani?

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
AGOA na MCC ni nyenzo mbili kuu zinazotumiwa na Marekani katika kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto za ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na masuala ya kiuchumi, kisiasa na hata utamaduni. Kupitia AGOA na MCC, nchi nyingi za Afrika zimenufaika kupitia miradi mingi ya maendeleo na kijamii kwa njia ya msaada na mikopo ya masharti nafuu.

Niwaulize wabobezi wa masuala ya siasa za Marekani, je Ujio wa Trump utaathiri vipi AGOA na MCC hasa ikizingatiwa matamshi aliyotoa hapo awali juu ya Afrika na watu wake?
 
IMG_20161109_195352_496.JPG
Africa siyo priority ya Donald Trump ha! ha anaweza kufunga Ubalozi wa Tanzania.
 
Naona mmeanza kulialia kabla ajaapishwa.

Operation ya kwanza ni kwa wale wote waliojibakisha madarakani kwa nguvu ya Dola.

Mimi nadhani tujiulize hivi....
NINI HATMA YA VISIWANI BAADA YA UJIO WA TRUMP?"
Hilo swali unaweza kuuliza wewe. Trump hana mpango kabisa na Afrika. Sidhani kama ataanza kufukua makaburi yetu
 
AGOA na MCC ni nyenzo mbili kuu zinazotumiwa na Marekani katika kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto za ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na masuala ya kiuchumi, kisiasa na hata utamaduni. Kupitia AGOA na MCC, nchi nyingi za Afrika zimenufaika kupitia miradi mingi ya maendeleo na kijamii kwa njia ya msaada na mikopo ya masharti nafuu.

Niwaulize wabobezi wa masuala ya siasa za Marekani, je Ujio wa Trump utaathiri vipi AGOA na MCC hasa ikizingatiwa matamshi aliyotoa hapo awali juu ya Afrika na watu wake?

Trump mlengo wake sio wa misaada misaada.Hajakulia maisha ya chini wala ya kusaidiwa saidiwa.Yeye ni mfanya biashara tena mkubwa.Ujio wake utakuwa wa kuwa karibu zaidi na makampuni ya biashara ya marekani ili yapanue himaya zao za kibiashara na kutawala dunia kibiashara.Ukiisikiliza hotuba zake anaitaka ile marekani kubwa ya zamani iliyokuwa ikiwika kiuchumi na kibiashara kuliko China AU NCHI YEYOTE.

Trump atajikita zaidi kwenye kujenga biashara zaidi kuliko hizo taasisi za misaada.Hizo zilikuwa sera za viongozi maraisi wa marekani waliokulia kwenye umaskini,waliosomeshwa kwa mikopo ya serikali au misaada na ambao maisha yao ni ya kuunga unga kwa kuwa wengi walikulia katika sekta ya serikali kama waajiriwa kabla ya kuwa maraisi wa marekani.Trump ni raisi wa matajiri ambaye matajiri wamemsimamia kidete ili awasimamie kwenye ubepari kihasa hasa.

Kipindi cha Trump tusahau kuhurumiwa ni biashara kwenda mbele.Hizo MCC na ndugu yake AGOA zinaenda kufa kifo cha mende.
 
Hizo hela za MCC waliinyima Tanzania baada ya kuchakachua uchaguzi wa Zanzibar.

Trump ni simba aliyejeruhiwa,alikuwa anaongelea uchakachuaji wa uchaguzi Marekani,na akaonya wasimchakachue.

Najua briefing kubwa atakayoipata kuhusu afrika mashariki,baada ya al shaabab,mafaili ambayo yatamchukiza sana ni la zanzibar,nkurunzinza,na baadae CongoDR.

Hayo yako mezani kwake kabisa tayari kwa hat
 
Hiyo IlikuwA Inawasaidia Ccm
Sasa Donald John Trump President Elect
Akikata Misaada Kaiuwa Ccm

Police Ndiyo Wamepewa Majukumu Ya TRA Barabarani
Hii Aibu Kubwa Sana
 
Yah, alikuwa anafight Rigged political system ya America ............. sasa nchi za kiafrika tujiandae!!
 
ule mchezo wakuongilia mikataba ya wawekezaji wa marekani kwa gia eti uzalendo umetukolea sasa umefikia mwisho.

yale magwangala ya geita,mchanga wa buzwagi......

the man is a businessperson anajua maana ya mkataba
 
CCM ni ile ile. Mtaisoma number kwani hatujali lolote. Sisi ni ma tajiri bwana
 
Hizo hela za MCC waliinyima Tanzania baada ya kuchakachua uchaguzi wa Zanzibar.

Trump ni simba aliyejeruhiwa,alikuwa anaongelea uchakachuaji wa uchaguzi Marekani,na akaonya wasimchakachue.

Najua briefing kubwa atakayoipata kuhusu afrika mashariki,baada ya al shaabab,mafaili ambayo yatamchukiza sana ni la zanzibar,nkurunzinza,na baadae CongoDR.

Hayo yako mezani kwake kabisa tayari kwa hat

Zanzibar na burundi inawaingizia wamarekani shilingi ngapi mpaka TRUMP ahangaike nao? Trump hujamsikia vizuri hotuba zake wewe.Interest za Marekani kwanza mambo mengine baadaye.Zanzibar kwake ni NON ISSUE ni sawa na kumwambia aingilie kati uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji uliochakachuliwa unadhani atakuja!!!
 
Tutashindwa kuutambu ..utaifa na uzalendo nchi zetu za Africa kama hatutajikubali wenyewe...
na kukaa tukifikiri matokeo ya ushindwa wa rais wa nchi zingine.
 
Back
Top Bottom