Nini Hatma ya MCC na AGOA baada ya Trump kuwa Rais wa Marekani?

Nini Hatma ya MCC na AGOA baada ya Trump kuwa Rais wa Marekani?

MCC hujui kuwa imeshakuwa suspended kwa sababu ya wizi wa kura Zanzibar na ile sheria ya makosa ya kimtandao?
sikio la kufa halisikii dawa

wameongeza na sheria ya wanahabari.

ngoja mzee awape kichapo
 
Vipi atawasaidia na chadema pia kuingia madarakani ama vipi?
Kwa ufupi Chadema na vile vi NGO vilivyozoea kuishi kwa kuomba omba kwa taasisi za serikali ya marekani watafute shamba LA kulima.Chini ya Trump hiyo biashara haipo
 
Trump alikuwa anatafuta kura na kazipata alichofanya ni Kujitofautisha na Wenzake kwa kuwa anajua hivi sasa Duniani Nationalism ime prevail worldwide
 
b376d476f58e76e4ace23cd7757c14e6.jpg

Wanaolialia ni hawa walioalikwa na Hilary.
 
Msitarajie makubwa kwakua ni Trump. Marekani inaongozwa na mifumo yao tangu zamani na ni maslahi tu yanafanya waamue kuingilia mahali au nchi. Au kutoa au kutotoa msaada.

So MCC na AGOA ambazo zimeshasainiwa zitaendelea. Kuzihuisha zikifa itategemea tu maslahi yao km bado yanahitaji hizo MCC au la
 
Tujiandae kutawala kidemokrasia.Trump hapendi Ujinga.
 
Trump mlengo wake sio wa misaada misaada.Hajakulia maisha ya chini wala ya kusaidiwa saidiwa.Yeye ni mfanya biashara tena mkubwa.Ujio wake utakuwa wa kuwa karibu zaidi na makampuni ya biashara ya marekani ili yapanue himaya zao za kibiashara na kutawala dunia kibiashara.Ukiisikiliza hotuba zake anaitaka ile marekani kubwa ya zamani iliyokuwa ikiwika kiuchumi na kibiashara kuliko China AU NCHI YEYOTE.

Trump atajikita zaidi kwenye kujenga biashara zaidi kuliko hizo taasisi za misaada.Hizo zilikuwa sera za viongozi maraisi wa marekani waliokulia kwenye umaskini,waliosomeshwa kwa mikopo ya serikali au misaada na ambao maisha yao ni ya kuunga unga kwa kuwa wengi walikulia katika sekta ya serikali kama waajiriwa kabla ya kuwa maraisi wa marekani.Trump ni raisi wa matajiri ambaye matajiri wamemsimamia kidete ili awasimamie kwenye ubepari kihasa hasa.

Kipindi cha Trump tusahau kuhurumiwa ni biashara kwenda mbele.Hizo MCC na ndugu yake AGOA zinaenda kufa kifo cha mende.
Asante kwa maono.
 
Msitarajie makubwa kwakua ni Trump. Marekani inaongozwa na mifumo yao tangu zamani na ni maslahi tu yanafanya waamue kuingilia mahali au nchi. Au kutoa au kutotoa msaada.

So MCC na AGOA ambazo zimeshasainiwa zitaendelea. Kuzihuisha zikifa itategemea tu maslahi yao km bado yanahitaji hizo MCC au la
MCC inaendelea wapi?
hawa wameshafunga ofisi na kuondoka
 
Mleta mada alichoongele ni hatima ya MCC kwa afrika sio Tanzania tu soma vizuri bandiko lake.Ziko nchi MCC bado wapo
wewe ongelea nchi nyingine za kiafrika,mimi nimechagua Tanzania
 
AGOA na MCC ni nyenzo mbili kuu zinazotumiwa na Marekani katika kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto za ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na masuala ya kiuchumi, kisiasa na hata utamaduni. Kupitia AGOA na MCC, nchi nyingi za Afrika zimenufaika kupitia miradi mingi ya maendeleo na kijamii kwa njia ya msaada na mikopo ya masharti nafuu.

Niwaulize wabobezi wa masuala ya siasa za Marekani, je Ujio wa Trump utaathiri vipi AGOA na MCC hasa ikizingatiwa matamshi aliyotoa hapo awali juu ya Afrika na watu wake?
WE UNAFIKIRI KWANINI SIE TUNAOWACHUKIA NYIE CCM NA MIUNGU WATU WENU MTAKOMA TUMEFURAHIA KWA SABABU HUYU TRUM NDIO PAROKO WA DUNIA SASA AKIKATAA KUJA KWENYE MISA YA MAZISHI YAKO HATA KATEKISTA HAKANYAGI HAPO NYUMBANI KWAKO SIKU YA MSIBA WAKO
 
AGOA na MCC ni nyenzo mbili kuu zinazotumiwa na Marekani katika kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto za ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na masuala ya kiuchumi, kisiasa na hata utamaduni. Kupitia AGOA na MCC, nchi nyingi za Afrika zimenufaika kupitia miradi mingi ya maendeleo na kijamii kwa njia ya msaada na mikopo ya masharti nafuu.

Niwaulize wabobezi wa masuala ya siasa za Marekani, je Ujio wa Trump utaathiri vipi AGOA na MCC hasa ikizingatiwa matamshi aliyotoa hapo awali juu ya Afrika na watu wake?
Trump supports agoa... Mcc is already gone
 
Sisi tutachokifanya tutaorodhesha vipengele vyote vya mkataba wa MCC vilivyokiukwa na serikali ya CCM na tunahakikisha waraka wetu wenye ujumbe mzito juu ya hili unafika kwa Mzee Trump achukue maamuzi.
 
Back
Top Bottom