Nini Hatma ya MCC na AGOA baada ya Trump kuwa Rais wa Marekani?

Yaani mnaandaa thread ya kumshobokea. Jamaa Hana mpango Na nyie endeleeni na mambo yenu
 
subiri maalim seif apande ndege akampe taarifa za jinsi mchezo mchafu ulivyofanyika.

tena atampa kabla hasira zake za kunusurika kuchakachuliwa na clinton hazijaisha,atatoa amri kwa IMF,World Bank na kutoa travel bans kama 500
 
yaani suala la zanzibar kwa Trump ni sawa na hadithi ya mtoto aliyeiba sukari,akarambaaa wee baadae akasahau kufuta midomo,

ghafla anaona baba anafika nyumbani,

Ngoma ya zanzibar haijapoa bado
 
Yule ndiye rais wa ulimwengu akisema kila mtu kushoto ni kushoto tu hata kama umekunywa gongo na kulewa utakwenda tu
 
Mkuu huu ni wakati wa kujitafakari Sana Kama taifa...... Kuishi Kwa kuomba misaada siyo suluhisho la kuukimbia umaskini...
Hebu tujiulize, hivi miaka 56 ya Uhuru, ccm ilishindwa hata kuwa na viwanda vidogo tu ktk kila mkoa na wilaya vya kusindika hata matunda na nyama?
Kama viwanda hivyo vingelikuwepo, umaskini ungepungua Sana Tanzania.
Umaskini wetu ni wa kujitakia halafu Watawala hawataki kuambiwa ukweli...
Ukiwaambia ukweli basi wewe ni mchochezi.
 
Hana ubavu kufuta program zilizokwisha anza. Institution is not a person.
 
Sidhani kama ni pigo maana Rais wetu alishajiandaa mapema kisaikolojia.

Yah kasahajiandaa, na hata kiuchumi kajiandaa, mapesa yote hayo yanayokusanywa tra, kubana matumizi, pia ukizingatia sisi ni nchi tajiri hatuijari misaada tunaweza kujitegea wenyewe..
 
Halafu huyo Jamaa Muamerikano Nikimwangalia Sana, Maamuzi yake Anafanana Na Mze, hapendi Ujinga Kabisa, Nadhani na yeye Ni Mchaka Mchaka wa Kazi tu.
 
suala la zanzibar lipigiwe mbiu,siku ya kuapishwa Trump nahisi kuna mzanzibari ataenda na bango la kumtaka Trump achukue hatua,na hilo bango alinyanyue juu kabisa mpaka Trump alione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…