Nini hatma ya Muba na John wa kipindi cha Mkasi?

Nini hatma ya Muba na John wa kipindi cha Mkasi?

Location inazungumza, salon ni eneo la umbeya, huwezi kutaka kujadili mambo yenye mstakabali wa nchi salon.

Sasa tuseme hiyo ni assumption tu nyinyi mlio tafsiri salon kihivyo
wengine tunaweza kutafsiri salon hasa za kiume ni sehemu ya kujadili sports .
wengine politics na kadhalika...
 
Sasa tuseme hiyo ni assumption tu nyinyi mlio tafsiri salon kihivyo
wengine tunaweza kutafsiri salon hasa za kiume ni sehemu ya kujadili sports .
wengine politics na kadhalika...

Okay!

Sports 100% nakubaliana na wewe, ila politics labda 24%!
 
Kipindi kizima kilikuwa na utapiamlo wa elimu, ndiyo maana hata hao wakaweza kuwepo.

Salama anaweza kuuliza maswali au kusema vitu vya ovyoovyo vinavyoonesha kabisa tatizo la elimu ndogo.

Niliangalia kipindi kilichomuhoji January Makamba, nikategemea maswali magumu, nikawa disappointed.

Nikaambiwa nina high expectations, naangalia Mkasi huku nikitegemea maswali ya "Hard Talk" na "60 Minutes".Nikaambiwa hiyo ndiyo style yao.

Kuanzia hapo sijaangalia tena.
Mkuu mbona hata wewe unafahamika kama kilaza mjanjamjanja tu, au sio?
 
Ngabu kuna vitu sio lazima viandikwe kwenye sheria

Naam, hapo wala sina ubaishi. Au upo? Kuna sehemu nimebisha hilo?

Mkasi kwa sababu ya umaarufu wake na kuwa kipindi kinachotazamwa na watu wengi
kujadiliwa 'hakuepukikwi' na ndo maana hapa tuko tunajadili

Kabisa. Pia hapo sina ubishi.

Sasa yaweza kuwa hakuna walichokosea lakini watu ku demand the best na ku demand quality
haita epukika.....

Hilo nalo nalielewa vizuri kabisa. Na nakubali kuwa there is always room for improvement, hata kwa watu binafsi kama mimi na wewe.

Binafsi naona kama walitaka kuwa kipindi cha 'masikhara' basi wangekuwa wana interview wasanii zaidi
huwezi kum interview mbunge wa Africa mashariki au waziri...halafu 'useme tu' 'hiki kipindi cha masikhara'
watu mbalimbali watakuwa na expectations zao.....kulingana na watu husika wanao hojiwa

Hapo ndipo ninapopishana na wewe.

Kwa nini isiwezekane kwa mbunge au waziri kwenda kwenye kipindi ambacho si cha serious issues za kisiasa, kiuchumi, na ki sera?

Ushawahi kukiangalia kipindi cha Churchill Live cha Kenya? Hebu mwangalie hapa Uhuru Kenyatta kipindi akiwa waziri wa fedha na naibu waziri mkuu. Wanaongelea nini hapo?



Huyu hapa Kalonzo Musyoka...makamu wa rais wa zamani wa Kenya. Anaongelea mambo gani hapo?



Huyu hapa Hillary juzi alienda kwa Jimmy Fallon...ni vicheko vicheko...hakuna u serious wowote ule.



Ubaya wa mbunge kwenda kwenye show kama Mkasi na kuongelea mambo ya kawaida yasiyo ya siasa uko wapi?

Kuna ubaya gani kwa mtu kama mbunge kuonyesha other side yake apart na hiyo nafasi yake ya ubunge?

Halafu hivi wapi walisema kipindi chao ni cha 'masikhara'?

Hiyo nimesema mimi kulingana na setting ya kipindi chenyewe. Kipindi kinarekodiwa kwenye barber shop/ beauty salon.

Kila kitu kiko laid back...kuanzia content hadi attire za hosts.

Ni wazi kipindi kama hicho si cha majadiliano ya hoja motomoto za kisiasa.

Ndipo nilipofikia hitimisho la kwamba ni cha kimasikhara [jambo ambalo wala si baya].
 
Nilichoandika juu ya wewe kuwa na Superiority Complex ni mtazamo wangu, na huwezi kuubadilisha.

Sijawahi kukuona ukijadili mada kwa mtazamo chanya, mara zote uko upande pinzani, labda huwa ukiona iko positive na mawazo yako unaona huna cha kuchangia.
Wewe hujafikia kwenye umuhimu wa kutakiwa ubadilishe mtazamo wako.

Kama hujawahi kuniona nikijadili mada kwa mtazamo chanya, ama hujanisoma vya kutosha, ama hujui kusoma.

Hayo si matatizo yangu, ni matatizo yako.
 
Mkuu mbona hata wewe unafahamika kama ****** mjanjamjanja tu, au sio?
Umetukana, JF ime ku censor, hujaeleweka umetaka kuandika nini.

Kutukana ni ishara ya frustrations zilizochanganyika na kushindwa kujieleza.

Punguza frustrations, ongeza uwezo wa kujieleza.
 
Wewe hujafikia kwenye umuhimu wa kutakiwa ubadilishe mtazamo wako.

Kama hujawahi kuniona nikijadili mada kwa mtazamo chanya, ama hujanisoma vya kutosha, ama hujui kusoma.

Hayo si matatizo yangu, ni matatizo yako.

Nakuelewa mkuu, sana tu.

Itakuwa matatizo yangu ndo yameleta huu mtazamo wangu.
 
Kuna jambo bado kulielewa kuhusu hizi barber shops za kibongo.

Ukienda kunyoa ukimaliza ni kama wanakulazimisha ufanyiwe ile sijui ndo wanaita scrub wenyewe.

Mimi huwa naweka bayana kabisa kuwa sitaki mengine zaidi ya kunyoa tu.

Lakini huwa naishia kuonekana mshamba. Huwa wananishangaa sana.

Matokeo yake nami huwa nawashangaa!

Tunabaki tunashangaana tu.
Wanakuona mshamba kwani hiyo scrubing wao wameijua lini?

Kwanini wanalazimisha? Ili waonekane wajanja wa mjini wakati pia wao wameiga/ wameletewa tu?

Je kuanzia mwaka 2010 kurudi nyuma walikuwa wanafanya scrubing kwny barber shops au hata kuajiri watoto wa kike?
 
Mkuu tu assume kweli Kiranga ana 'superiority complex'
je wewe utampinga kitu unachoona kina make sense kwa kuwa ni Kiranga?

hutakubali kuunga mkono hoja yake hata kama ni kitu unakikubali simply sababu mtoa hoja
'anajifanya anajua sana'?
Kwanza kumuona mwenzako ana superiority complex ni superiority complex.

Unajiona wewe ndi Zaidi yake na hutaki yeye awe zaidi yako ndiyo maana unasema ana superiorit complex.

Halafu, swali lako zuri sana. Kwa nini superiority complex iwe tatizo?

Kwa nini tusijadili mada, huyu mtu mwenye superiority complex anachotuletea kama ni sawa au si sawa, tulumbane kwa mada, kama huyu mtu mwenye superiority complex si lolote si chochote anajikuza tu, tutamshinda katika mada na kila mtu ataona hilo, kwa mada.

Bila ya majina ya superiority complex wala nini.

Ukianza majina ya superiorit complex unachosema kwa maana nyingine ni kwamba umeshindwa kujadili mada unaanza kufanya name calling.

Churchill once said timid people have much to be timid about.

I don't have much to be timid about, I am not timid.

Why do others want me to adopt their timid style of expression and be like them while I am a different individual?
 
Wanakuona mshamba kwani hiyo scrubing wao wameijua lini?

Kwanini wanalazimisha? Ili waonekane wajanja wa mjini wakati pia wao wameiga/ wameletewa tu?

Je kuanzia mwaka 2010 kurudi nyuma walikuwa wanafanya scrubing kwny barber shops au hata kuajiri watoto wa kike?
Nadhani wanafanya hivyo [kulazimisha kiujanja] ili mteja ulipe zaidi.

Kwa uzoefu wangu, ukinyoa tu bei inakuwa ndogi zaidi.
 
Umeonaee mkuu[emoji23] [emoji23] [emoji23] halaf bora mubah, huyo john maswali yalikuwa yanatia kichefuchefu cha moyo, inshort nilikuw simpend
Yule John akiwa muigizaji then akaigiza kama mfungwa atapata 100%
 
Huyu anasema, hili ni jambo la mtazamo tu, halina maamuzi nani yuko sahihi.

Mtu akisema twende kumuua Freelancer, akakusanya watu wakaenda kumuua, na hapo aseme tu ni sahihi, huo ni mtazamo wao tu.

Kimsingi mabishano hapa ni kama kuna namna ya kupima mambo haya tukaona kipi ni sahihi na kipi si sahihi na kama hamna namna hiyo.

Hata kama hukumu ya OJ watu wengine waliikataa, hilo tu halina maana kwamba haikuwa sahihi.

Hata kama mahakama huwa zinaamua kesi kwa makosa, hilo halina maana kwamba hakuna njia ya kuhukumu kisahihi

Huyu Freelancer ananiambia huwezi kumhukumu mtangazaji wa kipindi kwa sababu hii ni sayansi ya jamii, haina namna sahihi au mbaya ya kufanya mambo, inategemea tu na unayemuuliza.

Ni njia ipi hiyo ya kuhukumu kisahihi ukiacha mahakama?

[/[emoji108] ][[emoji108] ]
 
Kama kiranga akikubali kupokea hoja za upande wa pili mjadala unaweza kuwa wenye manufaa sana.

Mtu kuamini kile anachoamini ni jambo zuri sana lakini pia ruhusu hoja kadhaa za upande usiouamini kama changamoto uone kama zinaweza kukujenga kwa namna moja ama nyingine
Well said...fine advice
 
Huyo muba anapenda recognition maskini kuna siku nlikua niko Kwa sele bonge kakaaa anapiga stori yani ukimpita yeye ndo anakushangaa sijui ili akamate ur attention umshangae af ujue huyu si flani!Jana posta tena naingia stationary namkuta anapiga stori na wadada wa pale akaacha akaanza kunikazia macho wala sikushtuka kama namrecognize.Nadhani anataka ukimuona ushangae kumuona staa.
Kuna dizain ya wasanii washamba wa namna hizo hasa bongo.

Au labda alikupenda huwezi jua
 
Huyo muba anapenda recognition maskini kuna siku nlikua niko Kwa sele bonge kakaaa anapiga stori yani ukimpita yeye ndo anakushangaa sijui ili akamate ur attention umshangae af ujue huyu si flani!Jana posta tena naingia stationary namkuta anapiga stori na wadada wa pale akaacha akaanza kunikazia macho wala sikushtuka kama namrecognize.Nadhani anataka ukimuona ushangae kumuona staa.
That psychic ish you got aint gonna work out well trust me.......how do you tell that he wanted your recognition maybe you had a booger in your nose
 
Back
Top Bottom