Ngabu kuna vitu sio lazima viandikwe kwenye sheria
Naam, hapo wala sina ubaishi. Au upo? Kuna sehemu nimebisha hilo?
Mkasi kwa sababu ya umaarufu wake na kuwa kipindi kinachotazamwa na watu wengi
kujadiliwa 'hakuepukikwi' na ndo maana hapa tuko tunajadili
Kabisa. Pia hapo sina ubishi.
Sasa yaweza kuwa hakuna walichokosea lakini watu ku demand the best na ku demand quality
haita epukika.....
Hilo nalo nalielewa vizuri kabisa. Na nakubali kuwa there is always room for improvement, hata kwa watu binafsi kama mimi na wewe.
Binafsi naona kama walitaka kuwa kipindi cha 'masikhara' basi wangekuwa wana interview wasanii zaidi
huwezi kum interview mbunge wa Africa mashariki au waziri...halafu 'useme tu' 'hiki kipindi cha masikhara'
watu mbalimbali watakuwa na expectations zao.....kulingana na watu husika wanao hojiwa
Hapo ndipo ninapopishana na wewe.
Kwa nini isiwezekane kwa mbunge au waziri kwenda kwenye kipindi ambacho si cha serious issues za kisiasa, kiuchumi, na ki sera?
Ushawahi kukiangalia kipindi cha Churchill Live cha Kenya? Hebu mwangalie hapa Uhuru Kenyatta kipindi akiwa waziri wa fedha na naibu waziri mkuu. Wanaongelea nini hapo?
Huyu hapa Kalonzo Musyoka...makamu wa rais wa zamani wa Kenya. Anaongelea mambo gani hapo?
Huyu hapa Hillary juzi alienda kwa Jimmy Fallon...ni vicheko vicheko...hakuna u serious wowote ule.
Ubaya wa mbunge kwenda kwenye show kama Mkasi na kuongelea mambo ya kawaida yasiyo ya siasa uko wapi?
Kuna ubaya gani kwa mtu kama mbunge kuonyesha other side yake apart na hiyo nafasi yake ya ubunge?
Halafu hivi wapi walisema kipindi chao ni cha 'masikhara'?
Hiyo nimesema mimi kulingana na setting ya kipindi chenyewe. Kipindi kinarekodiwa kwenye barber shop/ beauty salon.
Kila kitu kiko laid back...kuanzia content hadi attire za hosts.
Ni wazi kipindi kama hicho si cha majadiliano ya hoja motomoto za kisiasa.
Ndipo nilipofikia hitimisho la kwamba ni cha kimasikhara [jambo ambalo wala si baya].