Nini hatma ya Shilingi ya Tanzania baada ya kuporomoka dhidi ya Dola ya Marekani?

Nini hatma ya Shilingi ya Tanzania baada ya kuporomoka dhidi ya Dola ya Marekani?

Kinachotakiwa ni kuuza zaidi nje kuliko kununua kutoka nje.
Kama unauza sana Nje kiuchumi hela yako ikishuka thamani ni faida,

Mfano China wanashusha thamani hela yao kimakusudi sababu wana Export sana

hapo mbona bado. itafika elfu 4000. huu mwaka mpaka ukiisha itafika 3200.
 
Kenya wanazalisha na kuuza kwa wingi nje, uswahilini tunaagiza zaidi nje kuliko kuzalisha na kuuza
 
ukiwaza mambo ya ukimani tanzania unaweza kuwehuka. huko nitarudi nishazeeka au maiti yangu.
 
Shilingi ya Kenya na ya Tanzania hazina tofauti kwa miaka mitano iliyopita.
Mwezi February Shillingi ya Kenya ilidondoka kwa asilimia karibu 30 na kufanya GDP ya Kenya na Tanzania kuwa na thamani sawa kwa takriban wiki moja.
Shilingi ya Kenya imedondoka sana, ni basi tu inalazimishwa kukaa ilipo.
"Inalazimishwa"...tz hatuwezj lazimisha?
 
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
Mkuu kushuka ama kupanda thamani hela ni panga linalokata pande zote mbili.

Hela ikipanda thamani assume leo hii dola kutoka 2700 iwe 1000, wafanyabiashara wanaoleta mizigo toka nje ya Nchi watafaidika, kama mtu alikua ananunua Jeans dola 1 ilikuwa inamsimamia 2800 then anauza 5000 faida yake ni 2200 ila ikipanda jeans ya dola 1 akiuza 5000 faida inakua 4000.

Ila hela ikipanda thamani ni mzigo kwa wanaouza nje ya Nchi, mfano wakulima, umelima zako mahindi gharama umetumia 2700 kwa kisado unategemea ukiuze dola 2 nje upate 5400 ghafla hela imepanda thamani imekua 1000 kwa dola ina maana mkulima atapata 2000 ambayo ni Hasara.

So kwa Wafanyabiashara hizi Currency exchange na bei za masoko wanacheza nazo sana kujiongezea faida.
 
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
Kweli kabisa, kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ni changamoto kubwa kiuchumi. Hali hii inaweza kuwa na athari mbaya kwenye gharama za maisha, biashara, na uwezo wa nchi kuagiza bidhaa za nje. Hapa kuna baadhi ya mambo yanayoweza kuchangia hali hii na hatua ambazo zinaweza kusaidia kurekebisha hali:

1. Mfumuko wa Bei na Uzalishaji Mdogo wa Ndani

  • Moja ya sababu kubwa ya kushuka kwa thamani ya sarafu ni mfumuko wa bei. Ikiwa uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi ni mdogo, Tanzania inalazimika kuagiza zaidi kutoka nje, na hii inahitaji dola za Marekani. Upungufu wa bidhaa ndani ya nchi huongeza bei na kuathiri thamani ya shilingi.
  • Suluhisho: Kuwekeza kwenye uzalishaji wa ndani, hususan kwenye kilimo, viwanda, na teknolojia. Tanzania ina ardhi yenye rutuba na rasilimali nyingi ambazo zinaweza kukuza uchumi. Serikali inapaswa kuimarisha viwanda ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kuanza kuuza nje bidhaa nyingi zaidi ili kuongeza dola za kigeni.

2. Uwekezaji na Uchumi wa Nje

  • Ikiwa wawekezaji wa kimataifa wanapunguza uwekezaji wao nchini, hii huathiri pia mtiririko wa dola nchini. Bila mtaji wa kigeni, shilingi inazidi kuporomoka. Wawekezaji wanapenda nchi zenye uchumi imara, miundombinu mizuri, na sera za ushuru zinazovutia.
  • Suluhisho: Tunapaswa kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vya kisera, kuhakikisha miundombinu ya kisasa kama nishati na barabara, na kutoa motisha kwa wawekezaji wa ndani na wa nje.

3. Uchumi wa Mauzo ya Nje (Exports)

  • Tanzania inategemea bidhaa chache za kuuza nje, kama vile madini na mazao ya kilimo. Thamani ya bidhaa hizi inaweza kubadilika kutokana na soko la kimataifa, na hivyo kuathiri mtiririko wa dola nchini.
  • Suluhisho: Kuimarisha sekta nyingine za kuuza nje kama utalii, bidhaa za kilimo, na viwanda. Hii itasaidia kuleta dola nyingi zaidi na kuimarisha shilingi yetu.

4. Sera za Fedha na Kodi

  • Udhibiti wa fedha za kigeni na sera za kodi pia huathiri thamani ya sarafu. Ikiwa sera za kodi na fedha hazina uwazi au hazijapangiliwa vizuri, huweza kuwaondoa wawekezaji na kupunguza mtiririko wa dola.
  • Suluhisho: Serikali inahitaji kutathmini sera zake za fedha na kodi ili kuhakikisha zinaendana na kuimarisha uchumi. Pia, ni muhimu kuwa na sera zinazoendana na sera za kifedha za nchi jirani kama Kenya ili kuepuka ushindani mbaya.

5. Utulivu wa Kisiasa

  • Utulivu wa kisiasa ni muhimu kwa uchumi imara. Ikiwa kuna hali ya wasiwasi wa kisiasa au kutokuwa na uhakika, wawekezaji wa nje wanaweza kuogopa kuwekeza, jambo ambalo linaweza kuathiri sarafu.
  • Suluhisho: Kuweka mazingira mazuri ya kisiasa, haki, na demokrasia kutawavutia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa nchi.
Kwa jumla, ili kuimarisha shilingi ya Tanzania, tunahitaji kuongeza uzalishaji wa ndani, kuvutia uwekezaji, na kuhakikisha sera za fedha na kodi ni nzuri na zenye utulivu. Pia, kukuza sekta za mauzo ya nje na kuhakikisha utulivu wa kisiasa kunaweza kusaidia sana kuongeza nguvu ya shilingi.
 
Chini ya awamu ya 6 itaendelea kuporomoka kwa kasi zaidi.

GOD BLESS TANGANYIKA
 
Hao wachumi wengi ndio tunao humu jf ujuaji mwingi Wala hawana faida katika Taifa.
 
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini k
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
Viongozi waache kukopa na kuiba kwa dhamana ya rasilimali za inchi.

Imagine trion karibia 30 zimekopwa kwa kivuli cha kukamilisha miundo mbinu inayojengwa na watu wanajimegea tu huku zinazoingia kwenye ujenzi ni some % tu, afu utegemee Sarafu yako iwe na Nguvu kivipi.

Suruhisho, Viongozi waache kuiba , kukopa wakope lkn kwa maslahi ya taifa kweli sio longo longo za washenzi waliojivika kofia za Uongozi.
 
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
Tuna PhD uchwara ndo zimekalia maamuzi ya nchi unategemea nini. Hawa watu walifukuzwa na JPM kipindi chake Mama kawarudisha kwenye chungu Cha maamuzi na PhD za mchongo za mwendo kasi. IQ ya Mwigulu, Prof Kitirya Mkumbo na wengine lazima thamani ya shilling ishuke sana. Na mkuu mwenyewe hajui chochote kinachoendelea hawa wa chini yake kufanya madudu.
 
Sijasoma Uchumi lakini ningekuwa Rais wa hii nchi ningefanya yafuatayo:-

1.Ningepiga Marufuku Ngano kutoka nje,wananchi wetu wangelima Ngano Kwa wingi Kwa ajili ya kuiuza nje ya nchi na kuviuzia Viwanda vya ndani!

Kukaa hata mwaka bila kula mkate au maandazi tusingekufa

2.Ningepiga Marufuku kuagiza Sukari kutoka Nje ya nchi,wananchi wangelima miwa na kuzalisha Sukari Kwa wingi na kuiuza nje!

3.Ningepiga Marufuku mafuta yeyote ya kula au mali ghafi zake kutoka nje,mafuta yote yangezalishwa ndani,alizeti zingelimwa Kwa wingi na mali ghafi mbalimbali za utengenezaji wa mafuta ilipaswa zilimwe hapa nchini,Arehi tunayo,watu tunao wakutosha,mvua zipo za kutosha,maji juu ya ardhi na chini ya ardhi yapo ya kutosha!

Yaani tungejifunga kibwebwe kama nchi ndani ya miaka 3 tu na Kuwa serious,mambo yangejipa!

4.Ningepiga Marufuku kuagiza na kununua magari ya serikali nje ya nchi,Tungeimarisha Viwanda vya ndani kama Nyumbu Ili magari yote ya Serikali yatengenezwe hapo!
 
Wazeee wakila kitu China i think we need to step up tupunguze import tuwashawish waje wafungue huku viwonder hizi importation zitatuua naskitika kuoba waziri wa fedha akicheka cheka na kuja assupmtion za kis3bg3 uchumi umekua watu wanunua sana vehicles
 
Hapana ni namna ya kuondokana na huu uvamizi uliotugharimu mno wazanzibari toka uhai wa watu mpaka nci yenyewe kuvamiwa na Tanganyika.

kama hamjatuwachia huru nchi yetu ya Zanzibar , karma itazidi kuwaumiza
 
Maoni yangu serikali ikubali ushoga tu ,,thaman ya pesa kazima ipande
Ukweli ni kwamba tokea mwaka 2023 shilingi ya tanzania imeporomoka kutoka 2330 mpaka 2730 kwa dola moja ya marekani ukilinganisha na shilingi ya majirani zetu KENYA ambao shilingi yao inazidi kupata nguvu dhidi ya dola ya marekani hasa mwaka huu wa 2024

Nini maoni yako, wapi tunakosea turekebishe nini au tufanye nini kama nchi.
 
Wachambuzi wenye vimelea vya uchawa wanasema " hakuna uhusiano wowote kati thamani ya shilingi na ukuaji wa uchumi" na mifano yao ni thamani ya shilingi ya Kenya na Tanzania.
 
Back
Top Bottom