Sijasoma Uchumi lakini ningekuwa Rais wa hii nchi ningefanya yafuatayo:-
1.Ningepiga Marufuku Ngano kutoka nje,wananchi wetu wangelima Ngano Kwa wingi Kwa ajili ya kuiuza nje ya nchi na kuviuzia Viwanda vya ndani!
Kukaa hata mwaka bila kula mkate au maandazi tusingekufa
2.Ningepiga Marufuku kuagiza Sukari kutoka Nje ya nchi,wananchi wangelima miwa na kuzalisha Sukari Kwa wingi na kuiuza nje!
3.Ningepiga Marufuku mafuta yeyote ya kula au mali ghafi zake kutoka nje,mafuta yote yangezalishwa ndani,alizeti zingelimwa Kwa wingi na mali ghafi mbalimbali za utengenezaji wa mafuta ilipaswa zilimwe hapa nchini,Arehi tunayo,watu tunao wakutosha,mvua zipo za kutosha,maji juu ya ardhi na chini ya ardhi yapo ya kutosha!
Yaani tungejifunga kibwebwe kama nchi ndani ya miaka 3 tu na Kuwa serious,mambo yangejipa!
4.Ningepiga Marufuku kuagiza na kununua magari ya serikali nje ya nchi,Tungeimarisha Viwanda vya ndani kama Nyumbu Ili magari yote ya Serikali yatengenezwe hapo!