Nini kazi ya hizo Sayari zilizobaki ukiondoa Dunia?

Kila sayari ina aina yake ya viumbe wapo sana ila hatuna uwezo wa kuwagundua....sisi tunategemea oxygen lakini je viumbe wasioonekana tunajua wanatumia hewa gani?

Viumbe walio katika sayari nyingine pia wanaona dunia yetu haina mazingira bora ya wao kuishi kama labda oxygen tunayoitegemea sisi kwao ni sumu(nawaza tu)

Tumeyakubali majibu ya wazungu miaka mingi bila tafiti za kutosha vipo vitu vingi vizuri mbele yetu ila tumekaririshwa miaka mingi kua ni vibaya sana na hatuvigusi na vipo vitu baya tukaaminishwa ni vizuri na tumeishi huko milele
 
Hakuna aliekanyaga ardhi ya mwezini kwanza
 
Basi kama haviko sawa na sisi hivyo sio viumbe tena! Mleta mada ameulizia kama kuna viumbe wengine nami nimemjibu kutokana na alivyouliza....
Sidhani kama ni sawa kusema kama haviko sawa na sisi sio viumbe tena. Nafikiri itabidi utupe maana yako ya viumbe kabla ya mtu kuelewa unachomaanisha.
 
nachokiamin mimi huko nako kuna viumbe ila hatuwez kuwaona na wao wanaendana na mazingira ya huko,sitak kuamin kama pluto,jupiter n.k ni mapambo tu
Hizo sayari zinaleta stability katika mfumo wa Jua katika kuchangia nguvu za uvutano. Ikiondoka hata sayari moja Dunia yetu na mfumo mzima utayumba.
 
Hivi mtu akitaka kujua kitu ina maana hataki Mungu aitwe Mungu? Au hiki kibwagizo kina maanisha nini!
 
Wapo ESA pia wanafuatilia haya mambo, Warusi, wajapani na wachina.
 
Hapo umezungumzia oxygen-carbon based life peke yake. Kuna uwezekano wa kuwepo viumbe zaidi ya hao
 
Umeangalia sana fiction movie, Hiyo theory ipo ila haijathibitishwa kisayansi
 
Acha hewa udongo wa mars unaweza kukuuwa coz unakiwango kikubwa cha kemikali.all in all universe ni mahari ambabo papo very dangerous kwa kiumbe hai.
Sijakuelewa uliposema universe ni mahali dangerous kwa viumbe hai umemaanisha nini?
 
ukifa unahamia sayari ingine,ila hujijua kwani memory za nyuma zinakuwa deleted
Huo ndo ukweli wenyewe, ndo maana mtoto akizaliwa huingia duniani kwa kulia ilhali wale anaowakuta wanafurahi ina maana analia kwa sababu ameacha watu aliokuwa amewazoea nao huko wanalia, kama mtoto hakulia wakati wa kuzaliwa haiwezi kuishi, inabdi afe ili kurudi huko alikotoka.

Lakini, tena mtu akifa, yeye hunyamaza tu ilihali wale waliobaki wanalia, kwa maana nyingine ni kwamba huko anakoenda watakuwa wanafurahi kupokea mgeni ilihali huku anakotoka wanasikitika kuondokewa na mtu waliyemzoea.
 
MBONA MATUKIO KAMA HAYO HAYATANGAZWI WAZI MF. KWENYE DIRA YA DUNIA B.B.C N.K KUNA SIRI GANI?
Ukiona hivyo fahamu ni BIG LIES in the name of Conspiracy Theories kama ilivyo kwa issue za Aliens and UFO!
 
Siamin kama kuna sehemu nyingine zaidi ya dunia tuliyopo sasa
 
Sayari moja tu katika mfumo wa jua ndio ina viumbe hai nyingine zote hazina kutokana na environmental conditions zao!
Mawazo rahisi ya kibinadamu. Miaka elfu moja ijayo mtu akisoma comment yako atashangaa sana jinsi kizazi hiki kilivyokuwa na uwezo mdogo kutafakuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…