Nini kifanyike ili kiongozi asipendelee kwao kama Hayati Dkt. Magufuli alivyoipendelea Chato?

Hii ni nzuri sana. Serikali kuu inashughulika na miradi na mambo ya kitaifa yaliyopitishwa na bunge tu. Hili suala lingekuwa na faida sana kwa nchi na kuharakisha maendeleo. Bahati mbaya, kama ulivyosema kuna watu mfumo huu unawafaidisha, hawawezi kubadilika hata kama gharama ni maendeleo ya nchi.
 
Zanzibar kujengwa hotel za kitalii za bilions of dollar, kiwete kipindi anapendelea pwani kwenye uwekezaji wa viwanda pamoja na mashule hamkuona? Acheni ngebe
Inaonekana ni ugonjwa wa siku nyingi. Membe alipokuwa wizara ya maji, alipelekaga karibu bajeti nzima ya maji kwao, watu walipiga mno kelele.

Mifano kama hii ni mingi, unafikiri ni coincidence kwa maduka ya MSD kuanzishwa Chato na Ruangwa? Kumekuwa na utaratibu kuwa mkipata Rais au Waziri basi mmeula, maana mnajua atapendelea kwenu. Ndiyo tunajadili tiba ya hilo.
 
Mkuu miradi mingi ya Chato haikujadiliwa kabisa bungeni. Ni kama Rais mwenyewe aliamua kuitekeleza. Na si Magufuli tu. Huu utaratibu wa Marais kupendelea kwao upo siku nyingi, sema tu Magufuli aliupeleka next level, hadi uvumilivu wa watu ukavunjika.
 
Hakuna cha kufanya mkuu,hata wewe mwenye vihela vyako mbuzi huwezi kuacha kujenga kwenu,sembuse Rais...
 
Sema nini kifanyike kiongozi mzalendo kama Dkt Magufuli asije kuuawa? Maana furaha yenu ya kumuua Dkt Magufuli sasa hamfichi, mnajiachia kama vile watanzania ni vilaza hawajui, just wait 2025!
 

Katiba mpya.
 
Acheni Nongwa na Uswahili Kiongozi asipopendelea Kwao apendelee wapi? Kupendelea Kwao ni Dhambi?

Hivi siyo nyie nyie ambao leo mnamcheka Hayati Nyerere kuwa hakupajenga Kwao Butiama?

Watanzania tuna PhD's nzuri za Unafiki.
Kwani chato kuna nn cha ajabu ambacho unaweza sema alipendelea?
 
Kwa katiba hii hata aje nani mambo yatakuwa yale yale tu maana katiba ina mpa nguvu nyingi sana kiongozi na hapo hapo inampa hakikisho la ulinzi(kutoshtakiwa).kwa katiba hii kukitoa chama tawala madarakani ni ngumu sana,labda tuombe msaada wa jeshi kukitoa chama tawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa katiba hii hakuna wa kumgusa Rais. Rais wa Tanzania ni mtu mkubwa mno baada ya Muumba mbingu na nchi. ushahdi huo upo waziwazi.

Ili kuepusha chochoko zote hizo watanzania wanatakiwa kwa mara ya kwanza kupewa katiba yao waliyoiandika kupitia kwa Tume ya Jaji Warioba.
 
Sema nini kifanyike kiongozi mzalendo kama Dkt Magufuli asije kuuawa? Maana furaha yenu ya kumuua Dkt Magufuli sasa hamfichi, mnajiachia kama vile watanzania ni vilaza hawajui, just wait 2025!
Kwa hatua aliyofikia ilibidi tu watu watengeneze mipango ya kifo maana alitaka kutawala milele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna cha kufanya mkuu,hata wewe mwenye vihela vyako mbuzi huwezi kuacha kujenga kwenu,sembuse Rais...
Rais pesa siyo zake. Mimi nikitaka kujenga kwetu ni pesa zangu.
 
Wewe ni mpumbavu kwelikweli,huyu mzee hakika alikuwa mwamba Tanzania Africa na duniani
 
Hii nchi huwa inaongozwa na vichaa na hawana uzalendo wa kweli maeneo potential yanaachwa kwasababu ya chuki wakikimbilia kuwekeza sehemu ambazo hazichangii kwa chochote kwenye pato la taifa tunapoelekea kutakuwa na matigray mengi hapa nchini.
 
Mkuu miradi mingi ya Chato haikujadiliwa kabisa bungeni. Ni kama Rais mwenyewe aliamua kuitekeleza. Na si Magufuli tu. Huu utaratibu wa Marais kupendelea kwao upo siku nyingi, sema tu Magufuli aliupeleka next level, hadi uvumilivu wa watu ukavunjika.
Hapana tembelea Msoga uone maajabu yaliyopo pale hutarudia kusemea wengine ovyo

Maraisi wengine walipendelea kuishi mijini hasa DSM na kutelekelza walikotokea, kwahiyo hilo ni takwa la wananchi sio rais kama mtu binafsi.

Mbona ujenzi huo upo maeneo yote.

Mtwara kuna soko la kisasa pale Chuno karibu na kituo cha mabasi ya mikoani lakini wafanyabiashara ni kama wamegoma kuhamia sokoni huko
 
Ni katiba mpya, kuwajibisha viongozi wakikiuka katiba na pia kupatikana bunge lenye wabunge waliochaguliwa na wananchi kidemokrasia ili wawe na uwezo wa kuidhibiti serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…