Pole sana. Kumchapa kibao ilikuwa sawa , lakini baadae ulitakiwa urudi kwake binti pia umwombe msamaha halafu hapo hapo piga nasaha kwa lugha ya hekima na upole sana.
Mimi nina binti wawili. Mdogo nilimnunulia smartphone umri miaka 14 akiwa kidato cha pili. Yuko Chuo Kikuu sasa na Dada yake pia sijawai pata usumbufu.
Utapiga utauumiza ongea nae tu amesha komaa. Na hasa kuhusu maisha yake ya baada ya masomo. Sasa sio kila wiki darasa la Nasaha. Tafuta nafasi nzuri tu mko wawili na mwaga nasaha. Huko mbele akija kujikwa atakumbuka na atajirekebisha. Akiwa na tabia chafu darasani awe vizuri atajirekebisha ataona uhuni unakatisha malengo. Ila kote kote akiwa 0 hapo hasara yake ni kubwa. Mungu akupe hekima.
Jirani yangu kule Oysterbay alikuwa na binti malaya sana. Yaani tukiskia gari tu na honi basi anapigiwa yeye. Na ni kila siku jioni
Kilichonishangaza pamoja na tabia zake chafu alifaulu kidato cha 4 na sita akaenda mlimani, pale akaona hapafai akaenda ulaya hajarudi mpaka leo. Nakumbuka mara ya mwisho yule binti alituma gari BMW kwa familia yake ila hajarudi mpaka leo. Alikuwa fuska ila darasani na kichwani alikuwa vizuri pia.