SoC04 Nini kifanyike Kumaliza tatizo la maji na ubovu wa miundombinu hasa ya Barabara vijijini na mijini kuelekea Tanzania tuitakayo

SoC04 Nini kifanyike Kumaliza tatizo la maji na ubovu wa miundombinu hasa ya Barabara vijijini na mijini kuelekea Tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Rajieh01

New Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
4
Reaction score
3
Kwa miaka mingi hadi Sasa Tanzania imeendelea kukabiliwa na changamoto katika utoaji huduma ya maji Kwa wananchi pamoja na ubovu wa miundo mbinu hasa ya Barabara nchini. Changamoto katika maswala haya zimechangia Kwa namna Moja ama nyingine kufifisha Kasi ya uzalisha Kwa ghrama nafuu, kufeli Kwa baadha ya mikakati ya kusidia wananchi kama "mtue mama ndoo kichwani", changamoto Kwa akina mama wajawazito, changamoto katika usafirishaji marighafi na bidhaa kufwatia ubovu wa miundo mbinu na athari zingine nyingi zinazo wakabili wananchi Kwa ujumla. kufikia mandeleo kama nchi yatupasa kuwa na uwezo wa kumaliza changamoto mbalimbali badala ya kukabiliwa na changamoto zile zile Kila uchwao. Kufwatia maelezo haya, nini kifanyike ili kutatua changamoto hizi kuelekea Tanzania tuitakayo miaka kumi hadi 20 ijayo.

Kuongeza mamlaka katika serikali za mitaa. Mamlaka katika vyanzo vya mapato, uwezo wa kuanzisha, kusimamia na kufadhili miradi, uwezo wa serikali za mitaa kuajiri na kadhalika. Changamoto hasa katika sekta ya maji imekua ikiongezeka siku hadi siku Kwa kuitegemea serikali kuu katika uanzishaji, ufadhili na utekelezaji wa miradi hali kadhalika ubovu wa miundo mbinu na ucheleweshwaji wake umeathiriwa na uwezo hafifu wa serikali za mitaa hasa Kwa ngazi ya halmashauri kuwa tegemezi Kwa serikali kuu. Ni Kwa namna gani Sasa ongezeko la mamlaka Kwa serikali za mitaa kupitia halmashauri nchini kunaweza leta utatuzi katika sekta ya maji na miundo mbinu kuelekea Tanzania tuitakayo.

Kufwatia ongezeko la mamlaka serikali za mitaa Kwa kushirikiana na serikali kuu kupitia wizara ya maji, zinaweza kufanya tafiti kupitia wataalamu Kila halmashauri kutafiti uwepo na kiwango Cha maji yaliyopo ardhini kuwezesha uchimbaji wa visima katika Kila halmashauri nchini. Iwapo halmashauri zitakua na uwezo wa vyanzo vya mapato vya kutosha, Kila halmashauri Kwa kushirikiana na serikali kuu kupitia wizara ya maji wanaweza kuagiza Magali ya kuchimba visima mawili hadi matano, yatakayo ingizwa nchi bila kutozwa Kodi ivo kua na gharama nafuu. Kila Kijiji, ama mtaa vikichimbwe visima na matenki ya kujazwa maji yajengwe, na wananchi watalipia gharama ya kuvuta maji majumbani mwao Kwa gharama zao kama kawaida na kulipa bili kama kawaida na ivo kua chanzo Cha mapato katika halmashauri ama Serikali za mitaa nchini. kufanya ivo kunaweza kutatua changamoto ya maji katika miaka 10 hadi 20 ijayo, kwani gharama za ujenzi wa miundo mbinu kutoka katika vyanzo vilivyo mbali itapungua kwani gharama ya mabomba kutoka vyanzo vya maji vilivyo mbali itapungua, Kwa mfano gharama ya mabomba kutoka ziwa Viktoria hadi Tabora ni kubwa ikilinganishwa na ikiwa visima vitachimbwa hapohapo Tabora na matanki kunyengwa ili kufanikisha usambazaji wa maji Kwa wananchi, uwepo wa magari ya kuchimba visima, kutazifanua halmashauri Kwa kushirikiana na serikali kuu kubakiwa na jukumu Moja tu ambalo ni kufadhili uchimbaji na ujenzi wa matenki na kusambaza maji.

Ongezeko la mamlaka katika halmashauri hasa katika vyanzo vya mapato vinaweza saidia kutatua kadhia mbalimbali zitokanazo na ubovu wa miundo mbinu hasa Barabara. Mamlaka ya vyanzo vya mapato katika halmashauri, vinaweza kusaidia uboreshaji wa Barabara Kwa namna ifuatayo, Kwa mfano, Kila halmashauri inaweza kununua vifaa vya ujenzi wa Barabara kama, kijiko(excavator), Gari la kubeba mchanga (tipper au dumper), shindilia (Role compactor), mwagilia maji (water bozzer), gari la kuchonga Barabara (Grader), lakini pia halmashauri zikiwa na uwezo kifedha zinaweza toa ajira Kwa muda mfupi au za kudumu katika uendeshaji vifaa vya ujenzi wa Barabara na waandisi wake ili kuwe na maboresho ya mara Kwa mara ya miundo mbinu ya Barabara katika halmashauri kama sio kuzijenga Barabara izo Kwa kiwango Cha lami, kufwatia uwepo wa vifaa Kila halmashauri vya ujenzi wa Barabara, kazi itakua Moja tu, kutenga bajeti ya ukarabati wa Barabara Kila mwaka. kufanya ivo kunaweza saidia uboreshaji miundo mbinu na kusaidia uzalishaji Kwa gharama nafuu, usafirishaji wa bidhaa mbalimbali na kadhalika, hivyo basi, serikali kupitia TARURA inaweza kuongeza nguvu Kwa serikali za mitaa ili kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya Barabara Kwa kuongeza fedha itakapo bidi, lakini pia TANROADS, ibaki kusimamia Barabara kubwa zinazounganisha wilaya na wilaya na mkoa Kwa mkoa. Hivyo basi, tunaweza kufanya Tanzania izidi kua ni yenye kufikika Kila pahala kirahisi kufwatia uboreshaji wa miundombinu kama ya Barabara.

Serikali za mitaa, zinaweza kushirikiana na jeshi la kujenga taifa ama la wananchi kuboresha miundo mbinu kama madaraja na kadhalika. Miaka kadhaa iloyo pita jeshi la wananchi ama kujenga taifa, walishiriki Moja Kwa Moja katika uboreshaji wa miundo mbinu kama madaraja, ujenzi wa mitaro, karavati na kadhalika, kuelekea Tanzania tuitakayo kurejesha ushirika uo na kuuendeleza kutachochea uboreshaji wa miundombinu Kwa Kasi hasa katika barabara na hivyo tutaweza kufanya Tanzania kua ni yenye kufika kirahisi Kwa gharama nafuu za maboresho.

Uboreshaji wa miundo mbinu hasa ya Barabara na maji kuelekea Tanzania tuitakayo ni muhimu katika safara ya maendeleo ya Tanzania. Utofauti kati ya Tanzania wakati wa uhuru, baada ya uhuru, ivi Sasa na Ile Tanzania tuitakayo ni muhimu kua tofauti katika muktadha wa maendeleo, changamoto za wakati wa uhuru , ivi Sasa na ule ujao hazipaswi kua sawa na iyo ndio dhana Pana ya mandeleo.​
 
Upvote 4
Back
Top Bottom