Nini kifanyike kupunguza au kuondoa kero ya upepo mkali wenye vumbi Dodoma?

Nini kifanyike kupunguza au kuondoa kero ya upepo mkali wenye vumbi Dodoma?

Wataalamu wa mazingira wana mkakati gani au mapendekezo gani kwa serikali na wananchi kwa ujumla kujaribu kupunguza au kuondoa kabisa hii kero ya upepo mkali unaoambarana na vumbi hapa jijini ili paakisi status ya makao makuu ya nchi. Wengine wanasema hii ni balaa ya milele, wengine wanasema inaweza kurekebisika.

Kuna miji kama Mwanza, Tabora, Morogoro, Kibaha, Tanga, Njombe, Mtwara na Lindi, Kigoma, Bukoba na Musoma haina hali kama ya hapa

Karibu tujadili huenda wana mazingira aakaokota mawili ama matatu ya kusaidia kuboresha jiji

Angalizo:
Tuache mizaha, tujikite kuandika mawazo yenye kujenga
Si afadhali sasa hivi mkuu!Zamani miaka ya 90vumbi lilikuwa linatoka Kongwa unaliona ukiwa Dodoma mjini,Dawa ni serikali kusisitiza upandaju miti na bili za maji zipungue ili watu wahamasike kumwagilia.
 
Ni kupanda miti mirefu tu tena mbali kidogo na mingine ikiwa imepandwa pembezoni mwa barabara
Bila miti labda ukuta sasa 😄
Hatuna tabia ya kupanda mpaka mlazimishwe
Agrey mwanri aliiweza mkoa wa Tabora watu walipanda kwa amri na ambae mti wake utakufa ataona
Leo mkoa wote wa Tabora na wilaya zake miti imestawi vizuri sana na upepo umepungua
 
CDA ilikuwa na bustani ya miche ya miti na maua eneo la Mailimbili kuelekea Msalato, sijui kama bado iko hai, binafsi niliwahi kwenda kununua miche enzi za CDA.
Ipo bado na kuna kipindi walikuwa wanatoa miche 5 bure kabisa ila dodoma ukitaka kibali cha ujenzi kwenye ramani yako ili ipitishwe na kupewa kibali lazima upande miti
 
Back
Top Bottom