Nini kifanyike kupunguza au kuondoa kero ya upepo mkali wenye vumbi Dodoma?

Dodoma ni jangwa, watu wa Dodoma wanapaswa kupanda miti

Tazama jiji la Arusha, kuna miti mingi tena ya green mpaka kandokando ya Barabara

Pandeni miti, miti ni uhai...mtaendelea kuumwa macho, shauri zenu.
 
Lete picha vinginevyo majungu
 
Ile kampeni aliyozinduaga PM ya kupanda miti elfu 5 kila mkoa iliishia wapi?
 
Muda huu nipo Iyumbu satellite center upepo unaopiga ni balaa unaweza ukakupeperusha ukatua Chidachi west. Usipopaka mafuta yenye mchanganyiko wa glycerin hutoboi

Ushauri wangu; Kampeni ya kupanda miti tena isimamiwe na Walimu wakuu Kila mwanafunzi awe na mti, Balozi wa nyumba kumi kila nyumba iwe na miti zaidi ya miwili kila ofisi ya kiserikali na isiyo ya kiserikali iwe na miti ya kutosha, Utekelezaji uambatane na faini.
 
AI
 
Dodoma ipigwe uzio (fencer] kuzuia upepo na vumbi
 
Wazo zuri sana, hii vita ni yakupigwa na kila mwana dodoma
 
Ile kampeni aliyozinduaga PM ya kupanda miti elfu 5 kila mkoa iliishia wapi?
Muulize kuhusu salaam alizoagizwa na boss wake kwa wana Njombe msikitini
 
Dodoma ni jangwa, watu wa Dodoma wanapaswa kupanda miti

Tazama jiji la Arusha, kuna miti mingi tena ya green mpaka kandokando ya Barabara

Pandeni miti, miti ni uhai...mtaendelea kuumwa macho, shauri zenu.
Serikali ihakikishe maji yanapatikana muda wote, hamasa/ya upandaji miti ielekezwe then no problems
 
Urban forestry ndio suluhisho pamoja na kuweka artificial aquarium na wind mills.p
 
It is hard to tame Nature.

Nafikiri jibu Rahisi lipo huko juu.

Ni kupanda majani, miti na mimea mingi tu sehemu zilizo wazi, na katika ujenzi wa kujenga ile Ring road, wafikirie na kujenga mitaro ya maji ambayo itasaidia umwagiliaji wa maji sehemu za Umma-miti, majani na mabustani. Yaani mitaro hiyo iende sambamba na hiyo ring road, maji yanayo kusanywa wakati wa mvua barabarani, yaende kwenye irrigation scheme.
 
Dodoma ni semi arid, kama jangwani tu, vumbi linatokea kwenye barabara za vumbi, sayansi itumike, wala sio nuclear science, unaweza kuiga walichofanya wa arabs, Dubai, Saudis, nk, nchi ya Maldives, walifsnya Rand recreamation, wakachukua eneo LA bahari, wakasukuma maji,wakajenga mijengo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…