Nini kifanyike kupunguza au kuondoa kero ya upepo mkali wenye vumbi Dodoma?

Serikali iwekeze kwenye umeme wa upepo na sio kulalamikia upepo hiyo ni fursa!
 
Ipandwe miti mingi ndani na nje ya mji.
 
Miti mkuu ndiyo mwisho wa upepo,vumbi,ukame,joto, mpaka vimbunga tunahitaji Sana miti kwenye miji na majiji yetu
 
Unaijua capetown ina upepo tena mkali mbona haina vumbi uondoa ccm madarakani ndiyo dawa
Huo upepo tena ni mali sana
Kwel tungeweka Wind mill for electricity. Leo mgao wa umeme usinge kuwepo.
 
Shida n upepo au Vumbi.............?
Huwez kupoteza/kuondoa upepo sababu upepo n natural. Upepo huu 2naweza kuutumia kama njia ya kuzalisha umeme kwa kutumia Windmill turbine.
Tunaweza kuondoa vumbi kwa kujenga nyumba nying na kupanda miti, majani na maua.
 
Huo mpango wa kupanda miti utasaidia sana lkini pia kuwe na mpango wa kulinda miti iliyopo hivi sasa. Kulikuwa na mti kando ya barabara, karibu na chuo cha Mipango ulitumiwa na Bodaboda na wafanyabiashara ndogo ndogo kujikinga na jua na kupata kivuli. Ulikuwa na mti mzuri sana unatoa matunda na kivuli. Lakini inasemekana tajiri mmoja alitoa fedha kwa Boda na kuwajengea banda la mabati na hatimaye kukata mti huo, sababu rasmi haijulikani!! Huku Africa ni shida, ingekuwa Ulaya na hali ya Dodoma ilivyo pangechimbika pale lkn wapi, watu wametulia tuli. DOGO matatani kwa kudhaniwa kukata mti ==> https://www.france24.com/en/live-ne...itain-s-most-famous-trees-deliberately-felled
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…