Nini kifanyike kwa Upinzani tunapojiandaa na Uchaguzi wa 2025

Nini kifanyike kwa Upinzani tunapojiandaa na Uchaguzi wa 2025

Mkakati mzuri Sana
Nikuhakikishie ukifika mezani kwa Mbowe ataomba hela za wafadhili na kuchangisha wananchi na at the end atazipiga [emoji23][emoji23]
Tusafishe chama kwanza
 
Umeongea point ya muhimu sana..................

Ikiwa mfumo Wa utawala utabaki kama ulivyo, hata kama atatokea kiongozi Wa upinzani, akapendwa na watanzania wote na CCM ikachukiwa na kutopewa kura na mtanzania yeyote..............

Bado tu CCM atapewa ushindi, dawa ni moja tu kwa sasa, tutumie nguvu zetu zote na wakati wetu wote katika kudai KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI

Muhimu kutambua mleta mada ni wale maofisa nanihii katika kupima maji.

Ni vizuri wakajua it is not over yet.

Ngoja Pompeo amalize ya kwake.
 
Maoni yako ni mazuri, lakini ni lugha nyepesi sana kwa mahala CCM ilipofika kwa matumizi makubwa ya pesa na vyombo vya dola!

Lazima tutambue kuwa kudaia katiba mpya mbele ya CCM hii sio sawa sawa na kudai deni ulilomkopesha mtu fedha!

Suala hili Kwa sasa ni vita ya kupata na kupoteza! CCM tayari ilishapiga hesabu ndefu, ikagundua kuwa mapungufu yaliyomo ndani ya katika ya sasa ndio mishipa mikuu inayopeleka damu na pumzi kwenye moyo wake, hivyo kuyashugulikia hayo katika namna inavyostahili ni sawa na kukata tawi la mti uliokalia! Ni sawa na kukata uhai wake yenyewe!

Hii ndio sababu ya ule mvurugano wote uliotokea wakati wa ule mchakato wa Rasimu ya Warioba na bunge la katiba, ambapo mwisho wa siku tume ilivunjwa kimyakimya na suala likapotezwa!
Sasa kwa hawa waliopo sasa madarakani wanaopenda kushinda kwa ASILIMIA 100% hili suala kuliingiza panahitajika pressure ya ziada tena kutoka nje hasa kwa wahisani, lakini wapinzani peke yao hapa nchini watathibitiwa kwa kila namna!

Hizo warsha na semina ulizopendekeza watafanyia wapi wasikamatwe kwamba wamefanya kusanyiko bila kibali??

Kwa hakika sidhani kama kuna vikao vyovyote vinavyolenga kujijenga kisiasa au kuhatarisha anguko la CCM vitaruhusiwa na hili jeshi tulilo nalo, Tumeona hadi vikao vya ndani vinazuiwa, hivyo haitakuwa rahisi!

Tunapozungumzia wapinzani kutoa madai yao, lazima pia tukumbuke uwepo wa vyama ambavyo kwakweli ni kikwazo sana katika kupigania demokrasia, mfano ni hivi vyama 9 ambavyo pamoja kuibiwa kura mchana kweupe tayari vimeshajitokeza na kutoa matamko yanayoonyesha wazi kuwa hivi ni kenge walioko kwenye msafara wa mamba!

Wapinzani watachukuwa muda mrefu sana iwapo hawatakuwa na umoja wenye nguvu, na mazingira haya ya kutoruhusu umoja huo kwa bahati mbaya yanajengwa na CCM, hivyo hata wakitangaza kutoshiriki uchaguzi wowote kushinikiza katiba, hivi vyama 9 vitashiriki tu na hivyo kuhalalisha ubatili uliopo!
 
Uchaguzi huu umekwisha na Upinzani unapaswa kucheza karata zake vizuri ili kuepusha majanga mengine mwaka 2025. Kelele za kutaka uchaguzi urudiwe hazitozaa matunda sasa ambapo hata maandamano tu ya kupinga Mbowe kupewa kesi nzito yamefail.

Nini kifanyike
1. Wale Wapinzani wawili walioachiwa majimbo waachwe waingie Bungeni wakapiganie haki. Hii haitakuwa kubariki wizi uliofanyika.

2. Viti maalumu kutoka CHADEMA nao waende bungeni. Haki itendeke kwenye kuteua nani aende ili kuepuka kukipasua Chama zaidi.

3. Agenda kuu Bungeni kila mpinzani anaposimama iwe ni kudai KATIBA MPYA/marekebisho makubwa ya Katiba pamoja na kuifumua NEC.

4. Wapinzani waliopo nje ya Bunge watumie platforms zote kuimba wimbo mmoja: KATIBA mpya na NEC iliyo huru.

5. Ikitokea akafa Mbunge, Upinzani uwe umeshadeclare mapema kutokushiriki marudio yoyote ya Uchaguzi kwa NEC hii ya sasa.

6. Warsha mbalimbali ziandaliwe na kuibua mijadara ya umuhimu wa Katiba mpya/muundo wa NEC iliyo huru. Wanaweza kualikwa wadau mbalimbali hasa wale development parners (a.k.a mabeberu) ambao wana mchango mkubwa kwenye bajeti ya Serikali na hivyo wakikohoa kidogo tu Jiwe anaweza kuwasikia na kutii.

7. Wapinzani wajipange na kufungua matawi mpaka kwenye ngazi za kata. Mafunzo yaanze kutolewa mapema ili by 2025 kuwe kuna misingi imara na hata iwe rahisi kupata mawakala bora kuliko ilivyokuwa mwaka huu.

Kususa haitakuwa strategy nzuri. Sanasana itawapa nafasi CCM kujiandaa vizuri mwaka 2025 na wao wakaja na system ya “kura za mapema” kama ilivyokuwa Zanzibar mwaka huu ili waibe kiulaini na kufunga hesabu mapema.
Kwa jinsi tulivyofika nadhani hatuhitaji tena vyama vya siasa, bora tuingie kwenye mfumo wa nonpartisan, hivi vyama ndivyo vinavyotuchelewesha maendeleo kama taifa. Wanaondelea ni wanachama wa CCM na ukiwa mpinzani utaona joto ya jiwe. Hivyo tufanye mchakato wa kuviondoa vyama vyote vya siasa.

Lengo la vyama vya siasa kwetu sisi waafrika vilikuwa kudai uhuru, sasa tumeshakuwa huru hivi vyama si tuvifute tu? Ikiwa tumeweza kufanya uchaguzi na chama kimoja tu ndicho kilichopata ushindi mkubwa, kwa nini tunapoteza pesa na wakati kwenye jambo lisilo na tija?
 
Wapinzani wajipange pia kwenye sera nzuri zenyemvuto.
sera za haki,wajibu na uhuru wa kutoa maoni,risasi 16 zimefeli pakubwa sana.
Unamaanisha uchaguzi ulikuwa huru na haki wameshindwa kwa kuwa sera zao hazikueleweka?
 
Haya
mambo mnayaongea mkiwa wapi, mbona barabarani hatuwaoni?
Tunataka mtoke mgongeshwe mpungue humu JF ili wabaki watu wenye kusimamia maneno yao.
Umeshiba damu za watu wewe.
 
sera za haki,wajibu na uhuru wa kutoa maoni,risasi 16 zimefeli pakubwa sana.
Ni kweli. Watanzania walio wengi wanapenda zaidi kusikia ahadi za ‘vitu’ kabla ya kuambiwa watapewa kwanza haki na ‘maendeleo’.
 
Ushauri wako hawawezi kuchukua Hata kidogo kifupi Ni chama ambacho akipendi Ushauri wao wanaamini chama Chao Ni kisafi na kinaongozwa na Mungu,Wanachama wake Ni malaika na ndio maana akijawahi kujirekebisha
Huu ni muda wa viongozi wote kuacha ujuaji na kusikiliza views kutoka kwa watu wengine nje na ndani ya chama badala ya kushupaza shingo then wachambue mchele na mawe.
 
Maybe we should underpaid politicians and overpaid teachers, then they would be smarter people and less stupid laws...[emoji41][emoji41]
 
Pia wajenge taasisi imara ya chama cha siasa na sio kikundi cha wanaharakati au kampuni ya udalali ya kuuza nafasi za uongozi ndani ya chama ili kujiepusha na tuhuma za watu mbali mbali wanaohama chama kwa mfano wabunge wa viti maalumu waliohama.
 
Umeongea point ya muhimu sana..................

Ikiwa mfumo Wa utawala utabaki kama ulivyo, hata kama atatokea kiongozi Wa upinzani, akapendwa na watanzania wote na CCM ikachukiwa na kutopewa kura na mtanzania yeyote..............

Bado tu CCM atapewa ushindi, dawa ni moja tu kwa sasa, tutumie nguvu zetu zote na wakati wetu wote katika kudai KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI
Hilo ndio tatizo lenu hamtaki kupokea maoni ya watu na kufanyia kazi sasa kwa mfano Chadema ni chama,kampuni binafsi au Ngo? mkindelea hivyo kila uchaguzi mtashindwa, mtalalamika mmeibiwa kura na mtadai tume huru, katiba mpya maana ndo kichaka chenu cha kujificha.
 
Hii ni point muhimu sana, Mbowe na Lissu wana siasa za kilaghai ambazo hazina uhalisia wala kugusa maisha ya mwananchi wa kawaida, Zitto na Dr Slaa wapo vizuri na ndio walioweza kupandisha upinzani mbele ya umma, kama Mbowe na Lissu wanataka kuendelea na siasa wabaki nyuma wawaaachie vijana kina Mnyika na Zitto wafanye siasa za hoja.
Kiukwel Bora zitto kuliko Lissu , zitto ana hoja na ni psychological killer , Lissu mropokaji Sana na anaji-expose kirahsi Sana ndo mana anaonekana ni mnafiki na msaliti ....
 
Uchaguzi huu umekwisha na Upinzani unapaswa kucheza karata zake vizuri ili kuepusha majanga mengine mwaka 2025. Kelele za kutaka uchaguzi urudiwe hazitozaa matunda sasa ambapo hata maandamano tu ya kupinga Mbowe kupewa kesi nzito yamefail.

Nini kifanyike
1. Wale Wapinzani wawili walioachiwa majimbo waachwe waingie Bungeni wakapiganie haki. Hii haitakuwa kubariki wizi uliofanyika.

2. Viti maalumu kutoka CHADEMA nao waende bungeni. Haki itendeke kwenye kuteua nani aende ili kuepuka kukipasua Chama zaidi.

3. Agenda kuu Bungeni kila mpinzani anaposimama iwe ni kudai KATIBA MPYA/marekebisho makubwa ya Katiba pamoja na kuifumua NEC.

4. Wapinzani waliopo nje ya Bunge watumie platforms zote kuimba wimbo mmoja: KATIBA mpya na NEC iliyo huru.

5. Ikitokea akafa Mbunge, Upinzani uwe umeshadeclare mapema kutokushiriki marudio yoyote ya Uchaguzi kwa NEC hii ya sasa.

6. Warsha mbalimbali ziandaliwe na kuibua mijadara ya umuhimu wa Katiba mpya/muundo wa NEC iliyo huru. Wanaweza kualikwa wadau mbalimbali hasa wale development parners (a.k.a mabeberu) ambao wana mchango mkubwa kwenye bajeti ya Serikali na hivyo wakikohoa kidogo tu Jiwe anaweza kuwasikia na kutii.

7. Wapinzani wajipange na kufungua matawi mpaka kwenye ngazi za kata. Mafunzo yaanze kutolewa mapema ili by 2025 kuwe kuna misingi imara na hata iwe rahisi kupata mawakala bora kuliko ilivyokuwa mwaka huu.

Kususa haitakuwa strategy nzuri. Sanasana itawapa nafasi CCM kujiandaa vizuri mwaka 2025 na wao wakaja na system ya “kura za mapema” kama ilivyokuwa Zanzibar mwaka huu ili waibe kiulaini na kufunga hesabu mapema.
Tumeshasema, uchaguzi umeisha kinachofuata ni kazi tu! Mda wa porojo umeisha kitambo.
 
Moja tuimarishe ngome, viongozi wasiwe harrased kila siku kupelekwa kulala selo,,, kesi zisizoisha,,,,, kama serikali ilivyoteua Attorney General, na Chadema iwe na counterpart 😊😊😊,we need strong lawyers atakaezuia intimidation kutoka kwa serikali, yes ni intimidation serikali inafanya ku destroy image yenu viongozi wa upinzani kuwa nyinyi ni aggressive, msiofuata sheria, hakuna mtu stelae vote for you kama hauko trustworthy
 
Tujipange kuanzisha chama kipya cha upinzani chenye malengo ya kujali mahitaji halisi ya wananchi (siyo ushoga), chenye kufanya siasa za kistaarabu, na kuenzi umoja na mshikamano wa kitaifa.
 
Kikubwa Wapinzani Tanzania wakubali tu kwa CCM ndiyo 'Baba Lao' na kwamba Rais wa JMT ni Ndugu John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mkemia.
 
Back
Top Bottom