Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,566
Kwanini mushauri upinzani wakati lengo lenu ni upinzani ufe?Mimi nashauri wapinzani wote wakae kando na watafute shughuli nyingine za kufanya ili muwe wenyewe!Hii ni point muhimu sana, Mbowe na Lissu wana siasa za kilaghai ambazo hazina uhalisia wala kugusa maisha ya mwananchi wa kawaida, Zitto na Dr Slaa wapo vizuri na ndio walioweza kupandisha upinzani mbele ya umma, kama Mbowe na Lissu wanataka kuendelea na siasa wabaki nyuma wawaaachie vijana kina Mnyika na Zitto wafanye siasa za hoja.
Hakuna uchaguzi umefanyika Tanzania zaidi ya CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani, mda si mrefu uchaguzi utarudiwa hakuna kusubiria mpaka 2025 Mbati sanaUchaguzi huu umekwisha na Upinzani unapaswa kucheza karata zake vizuri ili kuepusha majanga mengine mwaka 2025. Kelele za kutaka uchaguzi urudiwe hazitozaa matunda sasa ambapo hata maandamano tu ya kupinga Mbowe kupewa kesi nzito yamefail.
Nini kifanyike
1. Wale Wapinzani wawili walioachiwa majimbo waachwe waingie Bungeni wakapiganie haki. Hii haitakuwa kubariki wizi uliofanyika.
2. Viti maalumu kutoka CHADEMA nao waende bungeni. Haki itendeke kwenye kuteua nani aende ili kuepuka kukipasua Chama zaidi.
3. Agenda kuu Bungeni kila mpinzani anaposimama iwe ni kudai KATIBA MPYA/marekebisho makubwa ya Katiba pamoja na kuifumua NEC.
4. Wapinzani waliopo nje ya Bunge watumie platforms zote kuimba wimbo mmoja: KATIBA mpya na NEC iliyo huru.
5. Ikitokea akafa Mbunge, Upinzani uwe umeshadeclare mapema kutokushiriki marudio yoyote ya Uchaguzi kwa NEC hii ya sasa.
6. Warsha mbalimbali ziandaliwe na kuibua mijadara ya umuhimu wa Katiba mpya/muundo wa NEC iliyo huru. Wanaweza kualikwa wadau mbalimbali hasa wale development parners (a.k.a mabeberu) ambao wana mchango mkubwa kwenye bajeti ya Serikali na hivyo wakikohoa kidogo tu Jiwe anaweza kuwasikia na kutii.
7. Wapinzani wajipange na kufungua matawi mpaka kwenye ngazi za kata. Mafunzo yaanze kutolewa mapema ili by 2025 kuwe kuna misingi imara na hata iwe rahisi kupata mawakala bora kuliko ilivyokuwa mwaka huu.
Kususa haitakuwa strategy nzuri. Sanasana itawapa nafasi CCM kujiandaa vizuri mwaka 2025 na wao wakaja na system ya “kura za mapema” kama ilivyokuwa Zanzibar mwaka huu ili waibe kiulaini na kufunga hesabu mapema.
Hakuna cha mapungufu ya chadema wala nini wananchi wametenda haki vizuri wakaichagua chadema kwa Amani na upendo kilichofanyika ni CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi kwa njia haramu za kishetani, CCM haina baraka idhini ya wapiga kura laana itawaandama tuSiasa wanazofanya wapinzani ndio zinazowafanya warudi nyuma hatua kumi huo Ushauri wako hawawezi kuchukua Hata kidogo kifupi Ni chama ambacho akipendi Ushauri wao wanaamini chama Chao Ni kisafi na kinaongozwa na Mungu,Wanachama wake Ni malaika na ndio maana akijawahi kujirekebisha au kujitathimini na ndio maana walishindwa uchaguzi wanajifichia kwenye kichaka Cha kuibiwa kura.CCM pamoja na kuwa Ni chama tawala lakini kina tabia ya kujitathimini na kufanyia kazi mapungufu yao Sasa CHADEMA ambacho hata madaraka akina lakini wanajiona malaika hiv unazani kitakuwa kina maisha marefu?
Hii ni pipedream...and you know it is!mda si mrefu uchaguzi utarudiwa hakuna kusubiria mpaka 2025 Mbati sana
Lipumba yupo tangu 1994 huko. Maalim yupo sijui tangu lini. Jamii ya hawa watu ndio matatizo yenyewe. Vyama wamevigeuza kuwa NGOs binafsiKusema ukweli we need new faces huko upinzani, sio sura Zile zile,successions plan na recruitment of new, talented politicians should be given a chance/way
Nafikiri watakaa kikao na waamue tu kupeleka kinamama viti maalumu bungeni ili angalau ruzuku ije na kuwe na some form of representation ndani ya BungeMbowe ameng'ang'ania madarakani mpaka chama kinafia mkononi mwake, sasa hela hakuna, ruzuku hakuna billicanas pia hakuna baada ya miaka mitano kina Esther Bulaya sijui Matiko watakuwa washaolewa kwa ukata mkubwa na kupotea kwenye siasa James Lemberi
sahihi kabisa.NEC haina shida, na udhaifu wake huo huo washindi halali wanaweza kupatikana. Tatizo lipo sehemu tofauti kabisa.
Muda ni mwalimu mzuri sanaHuwa najiuliza kwa nini CCM wengi wanawashauri chadema kutosusia bunge? Na maalim akubali kuwa makamo wa rais? Wanaogopa nini?
Ule ushauri bado unasimama hadi kesho. Tutafanya makosa makubwa sana na Oct 2025 tutarudi huku kulialia huku tukisema "it is not over yet". Tunapaswa kuepuka kufanya makosa yaleyale kila mwaka wa uchaguziMuhimu kutambua mleta mada ni wale maofisa nanihii katika kupima maji. Ni vizuri wakajua it is not over yet. Ngoja Pompeo amalize ya kwake.
Nafikiri upinzani uje na sera za kimukakati ili tusonge mbeleIzo pesa za kufungua matawi kisha wayalinde watatoa wapi wakatai hawana pesa?
Walipokuwa na pesa mliwashauri waka kataa sasa iweje leo ambapo hawana pesa.
Ili iweje? Una maanisha wafunge na ofisi zao kabisa na wamwambie Msajiri awafute?Kwanini mushauri upinzani wakati lengo lenu ni upinzani ufe?Mimi nashauri wapinzani wote wakae kando na watafute shughuli nyingine za kufanya ili muwe wenyewe!