Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 5,168
- 8,982
Kijana akija kuomba kazi anakuja kwa unyenyekevu mkubwa tena akiwa kaweka mikono nyuma utafikiri ana staha na nidhamu ya kweli🙆♂️, kumbe hiyo ni zuga tu.
Sasa itokee umwamini umpe kazi ndo segedansi zinapoanza. Hakuna picha utakaa usiione. Kama alitakuwa awe anafanya marejesho atakuletea zile siku za mwanzo na pesa utaiona ila atapunguza kadiri siku zinavoenda na mwishowe haleti kabisa au pengine hata yeye usimuone tena!.
Kama ulimpa chombo mfano pikipiki usipokaa sawa anaiuza na kukuletea lost report ya mchongo ya polisi. Kama umemuamini kwenye biashara mfano restaurant au baa na zingine kama hizo mwendo ni huohuo anakuaminisha pale mwanzoni ili ukae kwenye kilengeo baada ya hapo unapigwa tukio zito mtu anapotea humuoni tena japo wengine huwa wanarudi bdae wakishamaliza salio na kupigwa juakali huko waliko.
Cha ajabu watu hawa wanafanya haya bila hata kujali kama biashara inaweza kufilisika na hatimaye kufa kabisa kwa hayo anayofanya na yeye akapoteza kazi mazima.
Ni hivi wakuu wizi umekuwepo siku zote toka enzi izo ndomaana hata ilisemwa "ukila na kipofu...." hapo mtamalizia wenyewe. Sio kama wazee wenu walikuwa hawaibi laahasha, maana sio malaika. watu wamekuwa wakiiba kwa dahari ya miaka ila sio kwa staili hii ya sasa. Iba kwa akili usiue kampuni.
Tukumbuke kuna kesho ya kuishi na kamwe hauwezi kuyamaliza matatizo kwa siku moja. Kama unaiba tumia akili. Sio unaiba hadi biashara inakufa hlf kesho unaanza kulialia ajira hazipo. Tulinde na kuziheshimu sehemu zetu za kazi maana ndo zinazotupatia kesho yetu.