Twilumba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 12,576
- 14,522
Salamu wakuu,
Nimeamua kuanzisha huu uzi kwa lengo la kuhamasishana kufanya mazoezi ambayo kimsingi ni suala mtambuka na jambo linalotakiwa kufanywa na kila mmoja wetu hasa kwa wale ambao kazi zao ni za ofisi kwa maana ya kwamba hazihusishi movement ambazo zinafanya mwili kuwa Active.
Mazoezi yamesaidia wengi hasa kuepuka magonjwa yasiyoambukiza, kuboresha muonekano wa kiumbo na Ngozi lkn pia kuongeza umri wa kuishi if kila kitu kipo constant!
Mazoezi ninayofanya mimi ni yale ya kukimbia, Jogging lkn kwa muhtadha huu mazoezi tunayotakiwa kufanya ni viungo, Gym ingawa kwa kweli kwa Gym sijaona output nzuri Zaidi ya kulipia tu na sifanikiwi kama ambavyo nimefanikiwa kwenye kukimbia yaani Jogging!!
Safari yangu ya Kuanza mazoezi
Nakumbuka Mwaka 2017 nikiwa Arusha kuna Boss wangu alinambia nimsindikize Hosp sikio linamuuma, kama kawaida tulipofika Hosp mapokezi walipokea kadi yake ya Bima, na kumkaribisha kwa Nurse kwa vipimo vya awali, baada ya kupima uzito, urefu alipimwa Pressure, lkn yule nurse alionekana kurudia kipimo cha Pressure Zaidi ya mara 2 na Boss akataka kungaka kwamba yy hajaenda pale kwa issue yyt Zaidi ya sikio.
Muuguzi aliumwuuliza yule Boss wangu kuwa umekuja na Nani, Boss akajibu na huyu Dogo, basi Muuguzi akaenda Moja ya Chumba ha Madaktari, baadae yule Boss wangu akaja chukuliwa na yule Nurse akaiginzwa chumba kile cha Daktari……. Mimi pia nikaitwa Daktari akauliza ni nani yako huyu, nikamwambia ni Boss wangu basi akawa amezungushiwa yale mapazia ya kijani na madaktari kama 6 wakaongezeka, kumbe Boss pressure ilikuwa ipo 200, wakampa vidonge viwili akaweka kwenye ulimi vikawa vinayenyuka baada kama ya dak 30 wakampima pressure ikawa inaendelea kushuka baada ya dak 30 tena ikawa iko 140 hapo tayar amehamishiwa chumba kingine cha mapumziko.
Baadae akakaa sawa na hapo akaja Dr akawa anaongea nae lkn kikubwa akamuuliza lifestyle yake na akaeleza kuwa yeye normally anatoka nyumbani asbh na gari anaingia kazini anatoka saa 11 jioni anaenesha gari hadi nyumbani, kuhusu ulaji akasema yy kawaida asbh anakunywa chai au sup una chapati au any Ngano Bites. Mchana ni Ugali/ wali/ndizi etc, Usiku ni wali etc…..
Yule daktari alimweleza wazi kwamba kama hatobadilika hatotoboa miaka 3 mbele, kwa sababu hiyo aliyoipata ni alarming kwamba afya yake sio salama hasa kutokana na aina ya Maisha anayoishi, na alimweleza wazi kwamba yeye ni mwenye bahati sana wapo wengi hawana hiyo bahati ya kupata alert ya hatari iliyopo katika afya zao!!
Kutoka Pale Boss alibadilisha kabisa aina ya Maisha yake, akawa amefuta kwa asilimia kubwa vyakula vya wanga, vyakula vya kukaanga, Junk food etc, matumizi ya soda yakakatwa, sukari ikawa kwake ni nadra sana kutumia, chakula cha usiku kiligeuzwa kuwa matunda pekee….. Boss akawa mtu wa mazoezi, Jogging asbh au jioni kulingana na Muda wake, akisafiri safari ya mikoani cha kwanza nguo zake za mazoezi na viatu anavi-park
From that day nikasema kumbe tunaweza tunaumwa tusijue kama tunaumwa, leo ni yule Boss wangu, je kesho haiwezi kuwa mimi, na mm nikaanza mazoezi mwezi huo huo baada ya kushuhudia ile sitofahamu aliyoipata Boss wangu.
Mwanzo ilikuwaje
Kwenye kuanza ilikuwa ngumu sana hasa kwa lile baridi la Arusha, kidogo kidogo nikawa tu nipo committed najikaza naamka nakimbia 1.5Km, nikaendelea kukua kimazoezi mara 3Kms, 7Kms, 10Kms nakumbuka my longest race was Kili Marathon 2018 nilikimbia 21.1Km hadi nilishwa kuendesha gari krudi Arusha. Nikaendelea kukimbia kama mazoezi yangu Primary …… Namshukuru Mungu nikawa Nguli sasa naweza kwenda Zaidi ya 42.2 Kms nonstop.
Kwa upande wa vyakula nakula healthy kwa kweli, wanga, sukari, Mafuta, na kwa usk I only take fruits au mbogamboga pekee wakati mwingine I can change kwa kunywa mtindi plan, I only take wine kama nahitaji kinywaji otherwise ni maji au fresh Juice ya ukwaju mix na Ubuyu!!
Hali ilivyo sasa
Hii kwangu imeshakuwa tabia, na nina enjoy sana Maisha ya kufanya mazoezi, kwa kweli siwezi kukata 3 days sijakimbia km 10 huwa najiona sipo sawa ana hayo ndio Maisha yang una Zaidi nimejiunga na running club nyingi za mikoa mbalimbali kama Arusha runners, Kigamboni Runners, Iringa Runners na The Runners Tanzania ambapo mkoa wowote nitakaoenda Napata washkaji wa kukimbia nao lkn pia wa kubadilishana nao mawazo hapa na pale na declare kuwa mimi ni Sosho Runner ambaye target yangu kwa mwezi ni kukimbia si chini ya Km 200 na nimefanikiwa Zaidi ya miaka 3 sasa!!!
Kila mmoja anaweza kufanya haya ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, naamini ukiweza kuwa inspire wengine utakuwa umewasaidia. Tufanye mazoezi lakini pia tule kwa afya, mwili wako siyo Dampo la kumwaga chakula, kula vizuri lkn kwa uchache naambiwa kuwa mwili kupungua asilimia 80 ni chakula, asilimia 20 ni mazoezi, so kula kuna nafasi kubwa Zaidi kwenye suala la kupunguza uzito.
Usisite kuniuliza swali hata PM, nitakusaidia, lengo wewe pia ubadili mfumo wa maisha yako kwa kufanya mazoezi na kula kwa afya!!