Mkuu hapa nakuunga mkono upande mmoja na upande wa pili sikuungi mkono.Kama umri umeshapita miaka 40 ni jambo zuri sana kupima pressure kila baada ya muda fulani,kwani kawaida hua ina tabia ya kuongezeka kutokana na umri ingawa hua haizidi vile viwango hatarishi,lakini aina ya maisha tunayoishi pia husababisha ipande kupita vile viwango ambavyo ni hatarishi.Swala ambalo nakuunga mkono ni tabia ya madaktari au wahudumu wa afya ambao huwa wanakurupuka na kumwambia mgonjwa pressure iko juu na kuanza kumtisha na hata wengine kumuanzishia mgonjwa dawa za pressure bila ya kufuatilia hiyo pressure imepandishwa na nini, au kutofanya uchunguzi wa kina kuhusu chanzo chake kuwa juu nini,mfano kuna watu hawana tatizo la pressure kabisa ila akiwa na infection yoyote kwenye mwili wake ina panda mf.Malaria,Typhoid n.k.Pia kuna baadhi ya hospitali vipimo vyao haviko sahihi kabisa,unaweza kupima hospitali hata 4 ukashangaa kila hospitali inatoa jibu lake tofauti,sasa hii pia ni hatari sana....