Nini kilikua chanzo cha ugomvi wa Afande Sele na O Ten?

Afande ni mtu wa wivu, anagombana na kila mtu. Alipopewa lile taji la mchongo la mfalme wa rhymes basi hakutaka mtu mwingine awike ama akubalike.
Afande wala hakugombana na watu ila alipotoa lile goma lake la kioo cha jamii aka darubini kali basi kila mwenye kujistukia akajistukia.. Yeye O ten akaruka na kipengele cha "Mnasifu ngono na pombe, pumbavu hamna soni eeh" Jamaa akaona kadisiwa hadi kuitwa pumbavu akaanzisha bifu. All in all wasanii wengi walitumia mabifu bandia kama njia ya kutokea
 
Kama ni uongo kaimba AFANDE SELE ktk DARUBINI KALI, Mm nimemQuote Afande! Uwe na adabu kwa Mtu ambaye hujui anasomekaje ktk phone book ya Bi Mkubwa ako
Ingependeza kama ungetaja wimbo wa O ten ambao ametajataja Majina tu..
Mimi nafikiri nyimbo zinazotaja Majina tu Ni Kama wimbo wa bwana misosi nitoke vipi..
 
Nyimbo ya kutaja taja majina alikua bwana misosi, na ngoma yake nitoke vipi
 
Kama ni uongo kaimba AFANDE SELE ktk DARUBINI KALI, Mm nimemQuote Afande! Uwe na adabu kwa Mtu ambaye hujui anasomekaje ktk phone book ya Bi Mkubwa ako
Mkuu ni kweli umejibiwa kuwa huo mstari haukuwa dis kwa o ten bali ulikuwa dis kwa bwana misosi wakati ule katoa wimbo wa nitoke vipi, sele alimdis misosi kuwa wimbo mzima anatajataja majina tu tena kwa mistari isiyo na vina, remember ule wimbo wa misosi haukuwa na vina
 
Enzi hizo wanavaa ma rain coat. Lile beat la nicheki nalielewa hadi leo. Ila nezi hizo east coast nlikuwa nawaona kama mbele chini ya kama gwamaka... Mimi nadhanj Oten ndiye aliyenunua ugomvi tu kwa kutafuta bifu kwa afande ili atengeneze story
 
Wewe ni muongo.

Afande alikua anam-refer Bwana Misosi na wimbo wake wa Nitoke Vipi.

Hata halioni aibu... Lione!
Yaani wewe uko deep na muziki wa zama hizo. Ni kweli afande alikuwa namsema bwana misosi
 
Yeah upo sahihi,siku hiyo waliotia fora pale ukumbini ni watoto wa Temeke waliokuja na inspector Haroun na Nature na watoto wa Moro ilikuwa bonge la mtiti

Afande aliua na ngoma ya Darubini kali enzi hizo ndio inatoka shangwe kama lote afande akakabidhiwa gari ambalo alipanda yeye na Dito mpaka Moro

Wapo waliosema Professa Jay alistahili ya kwamba eti Afande kushinda ilikuwa ni mchongo wa Shigongo kwakuwa siku za nyuma kuna makala ya kumpamba afande iliandikwa kweny gazeti lake nadhani la KIU(Japokuwa sina uhakika kama lilikuwa ni hili na kingine sina uhakika kama KIU ni part ya GLOBAL PUBLISHERS)..

Enzi hizo nilikuwa meneja wa kampuni fulani ya mabasi pale Ubungo siku hiyo watu wa Moro waliua route ya mabasi yetu maana waliyakodisha asilimia 80..
 
Enzi hizo wanavaa ma rain coat. Lile beat la nicheki nalielewa hadi leo. Ila nezi hizo east coast nlikuwa nawaona kama mbele chini ya kama gwamaka... Mimi nadhanj Oten ndiye aliyenunua ugomvi tu kwa kutafuta bifu kwa afande ili atengeneze story
G.k
Ana rap Kwa kigugumizi....
Itikadi zetu...

Watoto wa 2008 hawawezi kuelewaaa🤣🤣🤣😂😂
 
Kuna interview fulani Master J anasema wasanii wa zamani walipata pesa sana ilaziliishia kwenye starehe. Sasa naanza kuamini
 
G.k
Ana rap Kwa kigugumizi....
Itikadi zetu...

Watoto wa 2008 hawawezi kuelewaaa🤣🤣🤣😂😂
Hawawezi kuelewa na mkali wa chorus zake bi paulina zongo. Nakumbuka naona ama zangu ama zao niliona ile video iko level za destiny child ile ya survivor.
Gk alikuwa anajiona kama mbele na style yake ya kigugumizi aliimaster. Halafu ilikuwa vijana tangulia kuimba mimi kamanda namalizia kwa kufunga kazi kwenye nyimbo zote
 
Kuna interview fulani Master J anasema wasanii wa zamani walipata pesa sana ilaziliishia kwenye starehe. Sasa naanza kuamini
Ndio hata wenyewe wanakiri hilo,Mr Nice aliwahi kusema alipokea Billion 1 taslimu mwaka fulani kipindi anawika lakini zilivyopukutika hata yeye hajui,

Zamani wasanii kununua ndinga za maana kama Prado,Jeep ilikuwa kawaida sana tofauti na sasa msanii anawika miaka kibao hata kagari anashindwa kununua anaishia kufake tu instagram
..
 
aliechanwa ivo sio O TEN ni bwana misosi naye akaja kumjibu kwa wimbo wa "nikitunga nyimbo inavina ooyeeaa nataka weka heshima na jina oyeeaa Yuganda Bongo na Kenyaaa natoa ladhaa bila kubanaa.. alimshirikisha redsun wa kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…