Nini kilikua chanzo cha ugomvi wa Afande Sele na O Ten?

Nini kilikua chanzo cha ugomvi wa Afande Sele na O Ten?

Kuna NGOMA za O_ten,
Nilizo zipenda,

1.Mimi
hii ilikua dis track Kwa afande Sele directly.
2.sifa kumi za demu
3.akipendacho Binti
4.nicheki
5.kisa Sina gari
6.nyandindi
7.uvumilivu
8.nakaza roho
9. Tusahau (remix)
10.nipo huru

Hizi ni baadhi ya kazi za O_ten
11. Mkuu wa Mkoa (Regional Commissioner)
 
Afande wala hakugombana na watu ila alipotoa lile goma lake la kioo cha jamii aka darubini kali basi kila mwenye kujistukia akajistukia.. Yeye O ten akaruka na kipengele cha "Mnasifu ngono na pombe, pumbavu hamna soni eeh" Jamaa akaona kadisiwa hadi kuitwa pumbavu akaanzisha bifu. All in all wasanii wengi walitumia mabifu bandia kama njia ya kutokea
alimuongezea mstali mwingine " bamdogo acha upambe kujifanya una benzi wakati kwenu jumba la udongo duu!!" apo afande alimdiss tena o ten ambaye kwenye albamu yake ya kwanza amepiga picha na gari aina ya benzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu ilikuwa vijana tangulia kuimba mimi kamanda namalizia kwa kufunga kazi kwenye nyimbo zote
Sio zote.

Mfano: Komaa Nao

Verse ya kwanza kabisa ameanza GK.

Verse zimepangana hivi:
Verse 1:
  • GK.
  • Mwana FA
  • A.Y

Verse 2:
  • (Simjui)
  • (Simjui)
  • Snaire.
 
Kama hunijui naitwa philipo nyandindi na adui yangu mkubwa ni selemani msindi

Nimekulia muhimbili lakini nilikua naenda sana maskani East coast, tulikua proud sana na ECT. Hakukua na beef la maana sana. Ni michano tu
Kama ilivyokua kwa east coast yote na tmk. Wala haikua bifu ya maana japo east coast ndio walianza
 
Kama hunijui naitwa philipo nyandindi na adui yangu mkubwa ni selemani msindi

Nimekulia muhimbili lakini nilikua naenda sana maskani East coast, tulikua proud sana na ECT. Hakukua na beef la maana sana. Ni michano tu
Kama ilivyokua kwa east coast yote na tmk. Wala haikua bifu ya maana japo east coast ndio walianza
mkuu umekulia kota za madokta?
 
Lile Shindano lilikuwa la SHIGONGO na lilipewa Promo na Magazeti yk yake akina KIU et al... Wasanii walikuwa wanatolewa kwa kura za Mchujo mdogo mdogo lkn nakumbuka Majina makubwa yalofika mpk Funal ni Ptof. Jizze, Juma Mchilopanga, Solo Thang Ulamaa & Sele Mwenyewe!

I stand to be corrected
na cha ajabu zaidi wimbo uliompa ushindi Afande Sele ni darubini jali ambao kamshirikisha Prof Jay na Solo Thang mwenyewe
 
Na mimi kuna mwanangu mmoja mtoto wa mjini, Manzese kitambo,tulikuwa tunamuitaga 0-ten mpaka leo jina ilo alilibeba
O_ten mzee wa pamba bifu lilianza baada ya O_ten kutoa NGOMA ya nicheki....

Heyoo nicheki.....ninavyo ng'araaa enzi izo yupo East coast team....

O-ten alitoa NGOMA za kujisifia, kusifu ngono na pombe....
Kitu ambacho mfalme wa Rhymes [emoji881] Afande Sele hakupenda.....

Umenikumbusha rafk angu tulipenda ku mwita O_ten mzee wa pamba.....
Alikua anakuja skul na cheni shingoni......
Kuna siku akatongoza mdada mmoja mzur mlokole ukawa msala....O_ten ni mtu wa bring bring... cash money [emoji857][emoji857] umarekani mwingi...majigambo.........

Binafsi nili mpenda O_ten na staili yake ya kuflow....[emoji851][emoji851][emoji851]

Afande alikua anawachana wanaimba nyimbo za kuchochea uvunjifu wa maadili.....
 
Kuna NGOMA za O_ten,
Nilizo zipenda,

1.Mimi
hii ilikua dis track Kwa afande Sele directly.
2.sifa kumi za demu
3.akipendacho Binti
4.nicheki
5.kisa Sina gari
6.nyandindi
7.uvumilivu
8.nakaza roho
9. Tusahau (remix)
10.nipo huru

Hizi ni baadhi ya kazi za O_ten

Hapo Namba 4 na 8 ndio ngoma zangu haswaa
 
O Ten Mtoto wa Kilakala
Afande Sele Mtoto wa Misufini
Ugomvi wao kimsingi ni Pomposity ya Sele baada ya kushinda MFALME WA RHYMES.
Aliamini yeye ni Mfalme wa Nchi na hivo pia ni Mfalme wa Moro.
O Ten aliamini yeye Mkali na kile alichopata Afande ni ktk MFALME WA RHYMES ulikuwa ni Mchingo wa akina Erick Shigongo ambao hawakutaka Taji liende kwa wakali wa DAR wakiwemo Prof. Jay, Jay Mo & Solo.
Biff likichangamka baada ya Afande kumdiss OTen kuwa "Nyimbo nzima unataja taja majina tu
Tena kwa mistari iso na vina"
Cha kufurahisha wote hao ni Walevi! Mmoja wa Pombe za Kienyeji na mwengine Majani
Hiyo ya kutaja taja majina alikua anamponda bwana misosi na ngoma yake ya nitoke vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom