Roger Sterling
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 13,012
- 23,633
Mzee hapo umetudanganya Ngoma ya crazy GK na Pauline Zongo imetoka lini?
Keyword * nadhani *. Kumaanisha sina uhakika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee hapo umetudanganya Ngoma ya crazy GK na Pauline Zongo imetoka lini?
Haahaaa 😊🤓🤓🤓😊😆Umezingua unawezaje kutaka Ngoma za O ten bila kuitaja MKUU WA MKOA...
Hilo Pini lilikua n balaa...
Mi ni mkuu wa mkoa
Niko juu za meya
Mi kama Baba mwenye familia nalea
Mi kama king Niko juu zaidi ya queen.....
baba abdul futa hapo.Kipindi bifu limeiva Oten alimuimba Sele
Kwenye wembo wa Mimi, Oten anaimba kwamba!
Nilizaliwa Morogoro, hata siku nikifa maiti yangu iende Mor.
Naweka wazi adui yangu asinizike, hata muhuni yoyote asiyenipenda asisogee.
Kama vipi itupeni maiti yangu porini wale tai, muone mimi sifai.
Kama hujui naitwa Filipo nyandindi, na adui yangu mkubwa ni Selemani Msindi(Afande Sele)
Lakini baadae Sele na Oten walitoa ngoma pamoja inatwa Tusahau.
Oten anaimba kiitikio...
"Mimi na wewe kumbuka ni kitu kimoja, tena tumetoka moro mkoa mmoja.
Tusahau yote yaliyopita, na tugange mapya yanayokuja"
Verse 1: Oten anaimba kwamba..
Naepusha mbawa zangu kwa kuonekana mjinga, naamini mti mwema ndio unaopigwa mawe.
Kila kukicha nyandindi ndio naonelewa, nakabidhi roho yangu kwa baba aliye Mbinguni. Rafiki yako mkubwa anaweza kua adui, ila adui yako mkubwa hawezi kua rafiki ila Oten nimesamehe, ninapotoka napajua, ninapoenda sipajui, ndio maana kila siku napunguza maadui,
Verse 2: Afande akaimba..
....Na nywele ni kama akili, yule ana nywele ndefu na yule kipilipili,
Au mwingine nyekundu, na mwengine nyeusi tii
Ilimradi kuna toafauti, kati yetu ndani ya jamii
Hivi nani angetambua, kwmaba kuna kipindi mwezi unapatwa na jua
Ndio mambo yalivyo duniani, vitu kama sunami sio vigeni
Zinagongana meli, magari na ndege juu angani
Hata vidole vyetu mkononi havifanani
Hujawahi ona mama na mwana mda fulani hawaelewani, Sembuse mimi na Oten, Amkeni.
Acheni bifu za kiuni, kama kuanzisha bifu tuanzishe bifu na ukimwi
Yaliyopita sinndwele, sasa tugange ya mbele
Watu hatuna makucha vipi tunaomba Upele, hatueleweki zipi ni pumba zipi ni mchele
Wote ni walewale, kutwa kunyosheana vidole.
...Hilo halipo na kama halipo, basi nakula kiapo
Mnionapo na filipo, popote amani iwepo
Japo shetani hapendi, ila wote tuamini kwa Mungu ni zaidi ya ushindi!
Leo filipo nyandindi, yuko pamoja na mtu pori baba abdul na selemani msindi
Wajuzi naombeni mnijuze nini kilikua chanzo kati ya Mfalme wa vina Afande na Oten wa East Cost! Je nini kiliwapatanisha..?
Enzi wanatamba hawa watu magari ya kubeba mkaa yalikua hayajaanza kufika kijijini kwetu, stori zao hatukua tunazipata!
PamojaKeyword * nadhani *. Kumaanisha sina uhakika.
O tena anaa kola hill....O Ten Mtoto wa Kilakala
Afande Sele Mtoto wa Misufini
Ugomvi wao kimsingi ni Pomposity ya Sele baada ya kushinda MFALME WA RHYMES.
Aliamini yeye ni Mfalme wa Nchi na hivo pia ni Mfalme wa Moro.
O Ten aliamini yeye Mkali na kile alichopata Afande ni ktk MFALME WA RHYMES ulikuwa ni Mchingo wa akina Erick Shigongo ambao hawakutaka Taji liende kwa wakali wa DAR wakiwemo Prof. Jay, Jay Mo & Solo.
Biff likichangamka baada ya Afande kumdiss OTen kuwa "Nyimbo nzima unataja taja majina tu
Tena kwa mistari iso na vina"
Cha kufurahisha wote hao ni Walevi! Mmoja wa Pombe za Kienyeji na mwengine Majani
hapo Afande alimdiss Bwana Misosi,Misosi ntoke vipi!Kama ni uongo kaimba AFANDE SELE ktk DARUBINI KALI, Mm nimemQuote Afande! Uwe na adabu kwa Mtu ambaye hujui anasomekaje ktk phone book ya Bi Mkubwa ako
O ten yupo moro hata kwenye party ya mtoto wa afande tunda kugraduate SUA alikuwepo na wana wa sele kibaoAhsante kwa maelezo mkuu, daah Wengine tulikua ndanindani huko.
Vipi Oten sasa hivi yupo wapi??
Naomba uniwekee picha zake tafadhali za sasa na zamani
Ila vile vile kuna ngoma moja ya Gk nae anataja taja majina ya djs na watu wengine maarufuhapo Afande alimdiss Bwana Misosi,Misosi ntoke vipi!
mule ndo kataja watu kibao!
watu wengi walijua kamtaja o ten lakini ilikuwa diss kwa mtoto wa kitanga.
'unataja taja tu majina nyimbo nzima tena kwa mistari isiyo na vina'
wakati huo gk mwenyewe baba ake mkubwa jeshini ndo maana hata ishu ya magwanda aliimaliza.Hawakudakwa.
Kuna wimbo nadhani ule unaitwa ITIKADI
Kuna dogo aliimba"" Wana Usalama wananisaka kunitarget,hata Waitara anafahamu kuwa mi ni Most wanted"
Waitara alikuwa Mkuu wa Majeshi
Yaani Kama hapa juzi Kati msanii aimbe anasakwa na Mabeyo
Au Bilnas aimbe anasakwa na Huyu CDF wa Sasa.
I miss those days when Music was Music and Bars were Bars
Sikuwa nafahamu hili.wakati huo gk mwenyewe baba ake mkubwa jeshini ndo maana hata ishu ya magwanda aliimaliza.
Kama ni uongo kaimba AFANDE SELE ktk DARUBINI KALI, Mm nimemQuote Afande! Uwe na adabu kwa Mtu ambaye hujui anasomekaje ktk phone book ya Bi Mkubwa ako
endorsement ya Sugu nayo ilichangia sana. Aliingia na darubini akawa anamcheki Afande wakati anapiga darubini kali. Jay aliingia kwenye wheel chair na ile Usinitenge. kwa kweli Jay alistahili.Yeah upo sahihi,siku hiyo waliotia fora pale ukumbini ni watoto wa Temeke waliokuja na inspector Haroun na Nature na watoto wa Moro ilikuwa bonge la mtiti
Afande aliua na ngoma ya Darubini kali enzi hizo ndio inatoka shangwe kama lote afande akakabidhiwa gari ambalo alipanda yeye na Dito mpaka Moro
Wapo waliosema Professa Jay alistahili ya kwamba eti Afande kushinda ilikuwa ni mchongo wa Shigongo kwakuwa siku za nyuma kuna makala ya kumpamba afande iliandikwa kweny gazeti lake nadhani la KIU(Japokuwa sina uhakika kama lilikuwa ni hili na kingine sina uhakika kama KIU ni part ya GLOBAL PUBLISHERS)..
Enzi hizo nilikuwa meneja wa kampuni fulani ya mabasi pale Ubungo siku hiyo watu wa Moro waliua route ya mabasi yetu maana waliyakodisha asilimia 80..
Walikuwa wanavaa maturubai ya nang'aa wanaita leather. Na mtaani yalifika. Nashukruru sikuwa mtu wa fasheni, na hata leo, mambo mengine ni aibu sana.Enzi hizo wanavaa ma rain coat. Lile beat la nicheki nalielewa hadi leo. Ila nezi hizo east coast nlikuwa nawaona kama mbele chini ya kama gwamaka... Mimi nadhanj Oten ndiye aliyenunua ugomvi tu kwa kutafuta bifu kwa afande ili atengeneze story
Mwana FAbaada ya kushinda Ufalme wa Rhymes
Afande akazalisha maadui hawa:
1. Soggy
2. Solo Thang(Ulamaa) - mpaka leo hii bifu bado lipo
3. O-Ten
4. Madee
5. wengineo
Analiimbia jimama lakitanga et kiunon linamishanga, mara oooh duly zima taa uje kupata.... ShubamitHahhaa umenikumbusha kipind hicho Dully sykes wa moto kulikua na wimbo unaitwa Nyambizi.
Nyambizi nakupenda japo mkubwa, mateso nayopata usiku ni makubwa.
Kwakua tulikua bado wadogo huu wimbo kila ulikua ukifikia wakubwa zetu wanaurusha. Sikuwahi kujua kwa nini...na sikuwahi kuusikiliza tena.
2021 nilikua nimeweka playlist ya Bongo old-school ninazo kama 1600+ ndio ukaingia huu wimbo. Nikaukumbuka nikasema ngoja niusikilize. Nikagundua kumbe ilikua ni halali walikua wanaurusha huu wimbo. Full Porn[emoji125][emoji125]
O Ten Mtoto wa Kilakala
Afande Sele Mtoto wa Misufini
Ugomvi wao kimsingi ni Pomposity ya Sele baada ya kushinda MFALME WA RHYMES.
Aliamini yeye ni Mfalme wa Nchi na hivo pia ni Mfalme wa Moro.
O Ten aliamini yeye Mkali na kile alichopata Afande ni ktk MFALME WA RHYMES ulikuwa ni Mchingo wa akina Erick Shigongo ambao hawakutaka Taji liende kwa wakali wa DAR wakiwemo Prof. Jay, Jay Mo & Solo.
Biff likichangamka baada ya Afande kumdiss OTen kuwa "Nyimbo nzima unataja taja majina tu
Tena kwa mistari iso na vina"
Cha kufurahisha wote hao ni Walevi! Mmoja wa Pombe za Kienyeji na mwengine Majani
Wimbo gani O ten alitaja taja majina bila vina?O Ten Mtoto wa Kilakala
Afande Sele Mtoto wa Misufini
Ugomvi wao kimsingi ni Pomposity ya Sele baada ya kushinda MFALME WA RHYMES.
Aliamini yeye ni Mfalme wa Nchi na hivo pia ni Mfalme wa Moro.
O Ten aliamini yeye Mkali na kile alichopata Afande ni ktk MFALME WA RHYMES ulikuwa ni Mchingo wa akina Erick Shigongo ambao hawakutaka Taji liende kwa wakali wa DAR wakiwemo Prof. Jay, Jay Mo & Solo.
Biff likichangamka baada ya Afande kumdiss OTen kuwa "Nyimbo nzima unataja taja majina tu
Tena kwa mistari iso na vina"
Cha kufurahisha wote hao ni Walevi! Mmoja wa Pombe za Kienyeji na mwengine Majani
Lijamaa liongo sana [emoji3]Acha uongo.
O-tena hajawahi kutoa wimbo wa kutajataja majina.