**-KUPENDANA
My 1st love alikua anaitwa Latifa, bonge moja pisi (baba yake alikua mhindi mama yake mzanzibar mwenye asili ya kiarabu) huyu mtoto alikua kisu shule nzima, nakumbuka nilikua nimemtangulia madarasa kadhaa.
Wakati huo nilikua bonge la domo gundi, nilikua siwezi kabisa kumsalimia mtoto yoyote wa kike "Mambo" wala kuongea nae kama sijamzoea.
Enzi hizo mpira wa miguu, volleyball then kutumikia misa kanisani na zile mambo za kupiga chetezo ndio vilikua kama demu wangu, kifupi ndio vilikua vitu vilivyonipa furaha sana wakati huo.
Zile mambo za ukauzu na kujikuta mgumu mimi na wanangu ndio tuliona dili, yani ukiacha mpira ukawa una deal na issue za wanawake tunakuona kama snitch, mchumba, boya flani hivi uliyepotea njia, kumbe maskini ya Mungu wote circle nzima tulikua madomo gundi [emoji23]
Ikatokea kama zali tu nikafahamiana na Latifa kupitia volleyball, yeye akawa amenizoea na confidence ya kuongea na mimi anayo lakini mimi nikawa sina, kwanza nilikua m/kiti wa madomo zege Afrika mashariki na kati, pili nilijidharau nikaona kabisa huyu mtoto sio type yangu halafu mimi ni mgumu siwezi kuwa snitch wanangu kisa demu.
Cha ajabu nikikaa peke yangu najiona kabisa kua nampenda dogo, nikimuona au nikiwa karibu nae kuna furaha fulani ya ajabu naipata.
Moyo ukawa radhi ila mdomo ni dhaifu, nikawachana wanangu kua nampenda T, hawakushtuka sana sababu walijua domo zege mimi mission tu itakua failed. Na kweli ikawa hivo, kila nikipanga kumwambia T kua nampenda naona mdomo unakua mzito kama nimeshindiliwa mkate mgumu mdomoni.
Bahat nzuri T nae akajiongeza, akaona kabisa weakness yangu ni ipi, ndo ile wanasema mwanamke akipenda amependa kweli. Mtoto alinitengenezea mazingira akarahisisha kila kitu lakini nilivo fala nikawa naona mapicha picha tu ka nimelogwa, yeye mwenyewe hadi watu wengine wakawa wanaiambia we fala kusoma hujui hata kuona picha.
Kwa effort zake, wanangu japo walikua madomo zege kama mimi wakajikuta wamemzoea sana hapo ndipo waka gain confidence nao waka play part yao kama wana wakaniitia mtoto kibishi hivo hivo nikajikuta nimetongoza kwa kujiuma uma na jasho jingi, nadhani mtoto alivoondoka alinicheka sana maana nilipigwa na kigugumizi cha michongo [emoji847]
Mapenzi yetu yalianzia hapo, tulipendana sana aiseh, she was so beautiful, walimu walimtongoza, wale mabishoo wa shule lakini wapi mtoto alitokea kunipenda mimi tu boya flani hivi, hapo ndio nikagundua kua love is priceless you can't buy it (If it cost you anything that is not love)
Haya mahusiano wanangu walikua wanayaita zali la Titanic.
Latifa alinipenda sana sijui nilimpa nini, furaha yake ilikua ni kuniona tu na kua na mimi karibu, aliniambia akiwa around me kuna amani fulani hua anaipata, kuhusu pesa kwake haikua big deal kwao wanazo za kutosha, sijui alizizoea au ndio upendo.
Mtoto alikua tayari nimuoe, she was a muslim na mimi ni mkatoliki but hakujali kuhusu hilo, alikua aniambia lazima unioe, ilifika stage shuleni akaacha kuvaa hadi zile hijab japo mimi sikumkataza. Walimu wanoko hasa wale walioshindwa kumpata wakapeleka taarifa kwao mzee wake akataka kumuhamisha shule lakini aligoma katakata akasema mkinihamisha shule nyingine mimi sisomi.
Ikabidi ticha mmoja aje kuongea na mimi akanichimba mkwara kuhusu dogo kua nikae nae mbali na wala nisimharibie maadili yake kwa sababu wazazi wake wamesema wata deals na mimi, sema sikujali sana sababu na mimi mzazi wangu mmoja yupo huko huko kwenye system.
**-KUACHANA
Nilikua nampenda sana T lakini bahati mbaya sana sikua romantic, kwangu mpira wa miguu ndio ulikua kila kitu, japo nilimpenda ila yeye kwangu alikua ni ziada. Sikufanya makusudi ila ni vile tu nilikua bado beginner kwenye sekta ya mapenzi.
Muda mwingi tuliospend pamoja na effort zake mwenyewe, ikitokea akanibana nikawa nae muda wote hadi nikakosa kwenda mpirani au kwenye volleyball basi moyoni ningeumia sana kupita kiasi.
So sikujua umuhimu wa kumpa muda, hapo tulikua shule, nilipomaliza nikamuacha shule, kama mwaka hivi mapenzi yakaendelea, uzuri tulikua sehemu moja hivo tulipopata nafasi wakati wa likizo tulionana na tukaendelea hivo.
Baada ya muda ule umbali wetu na kutowasiliana mara kwa mara ukabadilisha mambo, Pole pole Latifa akaanza kubadilika, kwanza nadhani alichoka kutumia effort kubwa, pili distance ilimfanya azoee ile hali kua she can survive without me.
Hapo na mimi akili ikafunguka nikajikuta sasa ndio nampenda zaidi kuliko awali, nikaanza kutumia muda mwingi kumtafuta, kumjali lakini kwake nahisi it's was over, nikaanza kusikia juu juu kua kapata jamaa mwingine.
Ikaenda ikawa tupo tupo tu hatujui hata mahusiano yetu yanahusiana na nini, mwisho wa siku ikabidi tu aniambie ukweli kua, "I Loved but for now naomba kila mtu aendelee na maisha yake, I want to be free zaidi na mambo yangu binafsi"
Niliumia sana lakini sikua na jinsi ndio hapo nikajifunza kua (forever doesn't exist) everything in this life comes with an expire date.
I miss those days