Nini kilikufanya uachane na mpenzi wako wa kwanza (first love)?

Nini kilikufanya uachane na mpenzi wako wa kwanza (first love)?

Alikuwa age mate.... Wakati Yeye anataka kuolewa mimi wala sina hata wazo.basi akatokea mnyakyusa mmoja akatangaza nia akachukua jimbo. Daaa!! Mnyakyusa yule Ana bahati Sana amepata mwanamke bora sana. Siku mind but niliumia Sana.
Hii ni challenge kubwa sana kwa wapenzi wanaopendana na walioanza pamoja tangu utoto wao, unakuta mmependana kuanzia utotoni ila kutokana na wanawake kuwahi kukua inafikia hatua anahitaji kuanzisha familia wakati huo wewe ni bado unajipanga (unahitaji kama miaka mitano mbele), akitokea jamaa unapoteza mwanamke hivihivi hata kama bado anakupenda.

Dawa ya scenario kama hii ni kuhakikisha unapambana kutafuta maisha mapema na wahi mapema kumpa mimba kama kweli una malengo nae.

Mimi nilipofika form four nilifaulu afu mwanamke wangu hakupata matokeo mazuri kwahiyo wakati naenda advance nilimuacha kitaa, aaaah niliona kila dalili za kupoteza jimbo maana nilisikia eti kuna jamaa linataka kupeleka posa[emoji28], nilichokifanya ile form six tu nikampiga kibendi...afu nilipomaliza six nika cancel miaka miwili kwenda chuo ili nipambane na life. Mambo yalika vizuri nikasoma Chuo huku nikiwa nae na sasahivi ukinikuta tunaisha kishua tu.


She was my age mate , wakati anapata mimba alikuwa na miaka 22 wakati mimi nilikuwa na 23.
 
Alikua ananipenda sana.

Alipoanza chuo mala ya kwanza kwanza akaninunuliaga na smartphones

Alipofika mwaka wa pili akawa ameshaanza kuijua UDSM Vizuri


Basi hapo ndio na mimi nkaanza kusikiliza nyimbo za marioo
 
Nilienda kuishi mbali nae akapewa vishawishi akaanza kucheat(kumbuka hapo ana mtoto ananyonyesha), baadae akaanza akaniambia "mm nataka kuolewa" nikamuuliza vip kuhusu mwanangu? akanijibu "nitamwambia baba yako alishakufa"

Hii kauli iliniuma lakini bado sikuwaza kumuacha, niliporudi (hii ni baada ya kama miaka miwili) nilienda kwao kumuona mtoto (alitoka nyumban kwetu akarudi kwao) nikamkuta ana ujauzito wa mtu mwingne bado sikufikiria kumuacha,

Nilikuwa tayari kubeba huo mzigo kama wangu mambo yakikaa sawa ila hakuwa muwazi na bado sikufiria kumuacha, alikuja nitamkia siku moja kwenye sim nisimtafte tena yeye sahv ni mke wa mtu bas hapo hapo nikafuta no zake na ndio ikawa mwisho wangu mm na yeye.

Sijui kwann huwa napenda kiasi hiki
 
Back
Top Bottom