Nini kilimuua Mehmed II aliyetaka kuufuta ukristo/dola ya kirumi ulaya ??

Nini kilimuua Mehmed II aliyetaka kuufuta ukristo/dola ya kirumi ulaya ??

Picha ya rangi alichorwa enzi hizo ila hyo kashika upanga ni scene ya movie walio mu act .......

Kuhusu kusambaza dini kwa upanga ni dini zote zimefanya hivyo hata ukristo ulitumia panga kubatiza watu ulaya ya mashariki

Na kuhusu kifo chake inawezekana kweli Mungu alimchukua sababu bila hivo leo hii huenda historia ingebadilika sana penginepo ulaya ingekuwa bara la waislam watupu
Tofautish kati ya dini na watu wenye dini
 
Tofautish kati ya dini na watu wenye dini
Ila kuna ushahidi wa ukristo na uislam kuuliza swali la UNABADILI DINI AMA LAH na ukigoma mnachinjwa au mnapelekwa utumwani

Waislam walifanya hivo miaka ya 900 AD huko mashariki ya kati na wakristo pia walifanya hivyo miaka ya 1100 huko poland na sio wakristo tu bali walitumwa na viongozi wa juu wa dini zao Papa kwa wakristo na Calipha wa waislam aliyekuepo syria/iraq ya kale
 
View attachment 722372 View attachment 722373 Habari za mchana wakuu kama kichwa cha thread kinavyosema kwenye historia ya ulaya na kiislam kulikuwa na mfalme wa Ottoman empire dola ya kiislam hii iliyovamia ulaya kutokea mashariki ya kati na asia kwa sababu za kupanua utawala wao na dini pia.

Katika miaka ya 1400 walifanikiwa kuikamata constantinople iliyokuwa makao makuu ya byanztium empire ambayo ilikuwa ndio tawi la Dola ya kirumi mashariki ya ulaya na ilikuwa chini ya wakristo ila Mehmed II alifanikiwa kukamata mji huu na kufuta ukristo na kuifanya dini ya kiislam kushamiri mpaka leo yaani uturuki ya sasa na nchi za jirani.

Sasa baada ya kumalizana na tawi hili la mashariki Mehmed II hapo kati aliteka miji mingi tu ya ulaya ila mwishoni kabisa alielekea kuvamia makao makuu ya dola ya kirumi yani Rome ili kuitawala na penginepo kufuta ukristo ulaya nzima maana kama makao makuu ya wakatoliki wakisilimu je nchi gani ya ulaya ingebaki na ukristo??

Alianzia mji wa Otranto hapo italia kwa kuwavamia na kutaka wasilimu walivyogoma alichinja mji mzima na alikuwa amepanga sasa kuelekea Roma na alikua ameagiza majeshi zaidi yatiririke ili kufanikisha adhma yake.... ila usiku mmoja kabla ya kuanza vita ya kuelekea Roma alifariki ghafla na hivyo mpango huo ukafia naye na tokea hapo hakuwahi patikana mtawala wa ottoman mwenye dhamira na uwezo wa kuvamia Roma tena.

Sasa wajuvi wa mambo naomba mtujuze je nini hasa kilimuua Mehmed II aka Mehmet the conqueror shujaa huyu wa kiislam je aliwekewa sumu?? Alisalitiwa?? Aliuawa na wakatoliki ?? Na kivipi jemedari huyu masaa machache kabla ya tukio la kihistoria afariki ghafla maana wajuzi wa mambo wanasema kma sio kifo chake leo hii ulaya nzima ingekuwa imesilimu

Naomba kuwasilisha

Cc Palantir Malcom Lumumba Eiyer MSEZA MKULU na wanajukwaa wote

NB: Mods naomba uzi huu msiufute maana huwa mnazimoderate then mnazifuta hii inavunja moyo sana watu kuanzisha thread za kufikirisha jukwaa hili maana wanatumia muda kutafiti alafu tafiti zao zinaishia kutupwa kapuni.....
Siku zote mnaandika,waroma ndio walioanzisha uislamu,leo mbona mmebadilika,hawa hawa walioanzisha uislamu,wanataka tena,wauwane wenyewe kwa wenyewe.
 
Ila mkuu haya mambo sio ya kuangalia upande mmoja hata hao wakatoliki walivamia nchi za ulaya mashariki kama poland hungary na bulgaria wakiwataka wabatizwe waliokataa walichinjwa hiyo ni miaka ya 1000 hivi hivyo miaka zamani dini zote zilitumia mbinu hii

Ila huyu kidogo ilishtua wengi maana alifariki masaa machache kabla hajaenda kufuta dola ya kirumi ndio maana nimekuja kuuliza huku tupate habari za chini ya kapeti isije kuwa alipigwa kipapai na papa
Mbona hamueleweki,kuna nyuzi nyingi,humu zinazosema kuwa Roma,ndio walianzisha uislamu,leo naona mmebadilika,walioanzisha uislamu,waroma,wauwane wenyewe kwa wenyewe.
 
Mbona hamueleweki,kuna nyuzi nyingi,humu zinazosema kuwa Roma,ndio walianzisha uislamu,leo naona mmebadilika,walioanzisha uislamu,waroma,wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Kila mtu ana theory zake hivyo ni wewe kudadisi ipi ina ukweli na ipi ni uongo ila ukweli ni kwamba ukristo na uislam wote ulichinja waliokataa kubadili dini.
 
Siku zote mnaandika,waroma ndio walioanzisha uislamu,leo mbona mmebadilika,hawa hawa walioanzisha uislamu,wanataka tena,wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Hata marekani ilianzisha ISIS ila leo hii wanatunguana.... Vilevile kagame alianzisha M23 ila bado walikuja kutwangana na laurent nkunda..... Buhari alidhamini Boko haram kipindi akiwa mpinzani ila leo kawa Rais wanatwangana

Kwenye dunia hii lolote lawezekana
 
Siku zote mnaandika,waroma ndio walioanzisha uislamu,leo mbona mmebadilika,hawa hawa walioanzisha uislamu,wanataka tena,wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Maslahi mapana hukuona Nnauye anapigwa chini asiingilie maslahi
Lowasa slipigwa chini sababu mslah
 
huyu jamaa yawezekana waroma walimuua kwa kutumia ma spy wao..
kuna adui wao mwingne mkubwa kutoka spain alikua anaitwa HANNIBAL.naye aliwatesa hadi ikabidi kutumia akili kupambana naye koz kijeshi alikua kashindikana
 
Ila kuna ushahidi wa ukristo na uislam kuuliza swali la UNABADILI DINI AMA LAH na ukigoma mnachinjwa au mnapelekwa utumwani

Waislam walifanya hivo miaka ya 900 AD huko mashariki ya kati na wakristo pia walifanya hivyo miaka ya 1100 huko poland na sio wakristo tu bali walitumwa na viongozi wa juu wa dini zao Papa kwa wakristo na Calipha wa waislam aliyekuepo syria/iraq ya kale
Narudia tena ya kuwa tofautisha dini na watu waliopo ndani ya dini,
Uislam hausemi au haulazimishi mtu kuingia ktika uisalam, hizo ni tamaa na itikadi za watu wenyewe ila uislam hausemi hivyo
 
Mbona hamueleweki,kuna nyuzi nyingi,humu zinazosema kuwa Roma,ndio walianzisha uislamu,leo naona mmebadilika,walioanzisha uislamu,waroma,wauwane wenyewe kwa wenyewe.
Kuwa na akili hata punje moja, kati ya Roma na Uislam, ipi ilianza na kuota mizizi zaidi ya mwenzake????
 
huyu jamaa yawezekana waroma walimuua kwa kutumia ma spy wao..
kuna adui wao mwingne mkubwa kutoka spain alikua anaitwa HANNIBAL.naye aliwatesa hadi ikabidi kutumia akili kupambana naye koz kijeshi alikua kashindikana
hannibal alikuwa anatoka tunisia ya lero,wakati huo ilikaliwa na watu wa rangi mchanyiko.weusi walikuwa wengi ,wagiriki na warumi.
 
Narudia tena ya kuwa tofautisha dini na watu waliopo ndani ya dini,
Uislam hausemi au haulazimishi mtu kuingia ktika uisalam, hizo ni tamaa na itikadi za watu wenyewe ila uislam hausemi hivyo
Narudia tena ya kuwa tofautisha dini na watu waliopo ndani ya dini,
Uislam hausemi au haulazimishi mtu kuingia ktika uisalam, hizo ni tamaa na itikadi za watu wenyewe ila uislam hausemi hivyo
Mkuu both quran na biblia kwa nyakati tofauti zinasema yeyote asiye wa dini yako mchinje unless nieleweshwe mkuu sasa je hapo utasemaje ni msimamo wa watu binafsi??

Quran 9:5

9:5 - Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

2 Nyakati 15:13
13 na ya kwamba ye yote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, kwamba ni mwanamume au mwanamke.
 
Duh naweza kukubaliana na jibu lako hili lakini je kwanini iwe wakati wa kwenda kuifuta Roma?? Kwanini kijana asingesubiri baba yake amalize ulaya nzima ili hata akija kutawala asipate upinzani kipindi akipata madaraka ?
Nini kinakuhakikishia kuwa wngefanikiwa kuishinda dola ya Rumi mpaka udhani kuwa ile ilikuwa siku muhimu sana kwa mehmet.
Na kwanini kifo chake katika siku hiyo usikipe huo umuhimu kwake?
Ikiwa una kiu ya kufuta jambia useme!
 
Sio Wakristo Sema Waroman Cathorik ndio waliotisha waliokataa kubatizwa.
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya Wakristo na Waroman Cathorik.
Roman Kathorik ni dhehebu kama walivyo Wa-Shia au Suni katika Uislam.
Sio Wakristo wote ni Roman.
Papa ni Kiongozi wa Waroman na sio Wakristo wote.

Imani ya Ukristo hairuhusu Kuadhibu watu katika kosa liwalo lolote lile. Wanaaambiwa anayeruhusiwa kuadhibu ni Mungu peke yake kwenye Makosa ya Kiroho.
Ukiona kundi la watu linaadhibu watu kwa kujidai lina mamlaka ya kiimani hao watakuwa watu wa dini fulani au dhehebu fulani na wanatimiza malengo ya dini hiyo na sio Ukristo.

Ukristo ni
"Kufanya mambo aliyo agiza Yesu Kristo kuyafanya kupitia mafundisho yake ya namna ya kuurithi ufalme wa Mbingu"

Hao waliochinja watu kwa kukataa kubatizwa sio Wakristo ingawa labda wenyewe walijiita hivyo kwakuwa hakuna agizo lolote toka kwa Kristo Yesu linalosema watu wasiotii maagizo yake wachinjwe.

Endelea kukumbuka kila wakati kuwa kuna Wakristo na wengine wanaoweza kujiita Wambagala, Waebrania, Waufufuo, Waroma, Wasabato, wainjiri nk.
Hayo ni majina tu ya dini na kujitambulisha lakini majina hayo hayawafanyi wawe Wakristo.

Sema Waroma waliwaua watu kipindi fulani kwa kuwalazimisha kubatizwa na sio Wakristo kwani haikuwa ajenda ya Kikristo na haitakuwa.
Mkuu sijaelewa unapinga hicho kitendo walichofanya kwa maana sio katika mafundisho ya ukristo au unapinga hao waroma kuwa sio wakristo? Mfano hata kusema uongo pia sio katika mafundisho ya ukristo,ina maana mtu akiongopa anakuwa sio mkristo?
 
Mkuu both quran na biblia kwa nyakati tofauti zinasema yeyote asiye wa dini yako mchinje unless nieleweshwe mkuu sasa je hapo utasemaje ni msimamo wa watu binafsi??

Quran 9:5

9:5 - Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.

2 Nyakati 15:13
13 na ya kwamba ye yote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, kwamba ni mwanamume au mwanamke.
Atauwawa ina tofauti kubwa sana na "waueni"
 
Umeanza vizuri lakini umeharibu pale unapojaribu kutudanganya Nabii Issa ndiye Yesu Kristo hawa huwezi kuwalinganisha hata kidogo na ukijaribu kuwalinganisha ndio mwanzo wa kupotea kabisa.
Eliza unacho kijua sio kulalamika and wenye kuthamin mapokeo siku zote ni wenye elimu na ujuzi...
 
Nini kinakuhakikishia kuwa wngefanikiwa kuishinda dola ya Rumi mpaka udhani kuwa ile ilikuwa siku muhimu sana kwa mehmet.
Na kwanini kifo chake katika siku hiyo usikipe huo umuhimu kwake?
Ikiwa una kiu ya kufuta jambia useme!
Mkuu sio tu kwamba nimejihakikishia bali mehmet alipiga dola ya kirumi kumbuka ilikuwa ina falme mbele western roman empire ambayo ilikuwa na makao makuu Rome na pia Eastern Roman Empire iliokuwa na makao makuu huko Byzantium (uturuki ya sasa), hivyo kama aliweza kuipiga kabisa dola ya mashariki kivipi angeshindwa kuipiga ya magharibi??

Kumbuka kabla ya hapo alikwisha anza vamia vijiji vya kuelekea Rome ambapo hakupata upinzani wa maana kabisa mfano hapo otranto alichinja almost mji mzima na wengine mateka hivyo kwa hali yeyote Rome ingekutana na kipigo kikali

Nachojiuliza kama kweli aliuawa na mwanae ni kwanini basi mwanae asingesubiri vita iishe ili achukue ufalme mkubwa zaidi maana sielewi kwanini unaona baba yako

Kuna nadhari nyingine inasema aliwekewa sumu na wajakazi kutoka naples waliokuwa mapandikizi wa papa.... Bado najiuliza kivp papa aliweza jipenyeza hadi kwenye ufalme wa kiarabu bila kujulikana tena kwa muda mfupi vile

Ila ukweli unabaki kwamba muda mchache kabla hajaamua kwenda kuivamia Rome ndipo alipofariki na hapo ndipo panaleta maswali mkuu
 
Back
Top Bottom