Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Tulia ufikirie vizuri kuna kitu utaelewa
Hujajieleza unakusudia nini. Inawezekana unachofikiri unanieleza nakielewa vizuri kuliko unavyofikiri.

Kwa nini hutaki kukitaja?

Hukielewi? Unaogopa? Una nature ya kichawichawi ya kujifichaficha?

Sijatoa hoja yoyote inayohusu pesa kutumiwa kwenye nchi nyingi. Habari ya pesa ya China kutumika nchi ngapi inakuja vipi kwenye hoja zangu?

This question is totally invalid, it is not related to my point at all.

You are making a logical non sequitur fallacy. Unaingiza hoja tofauti na ninayoiongelea mimi.

Hoja yangu ni kwamba, thamani ya pesa ya nchi si lazima iendane na uzuri wa uchumi wa nchi hiyo.

Hoja hii nimeitokea mfano wa Kenya na Japan.

Shilingi moja ya Kenya in athamani kuliko Yen moja ya Japan.

Shilingi moja ya Kenya ni sawa na 1.19 Japanese Yen.

1 Japanese Yen ni 0.85 Kenyan shillings.

Je, hilo linamaanisha Kenya ina uchumi mzuri kuliko Japan? Hapana.

These are hard numbers, not some blah blah about "tulia ufikirie vizuri utaelewa".
 
Kwanza Elewa kwamba katika Masoko yote ya Bidhaa,huduma na hata Fedha yanasimamiwa na Sheria za Masoko.Sheria ya Msingi ya SOKO inasema kwamba Supply ikiwa Ndogo kuliko Demand bei huwa na Tabia ya Kupanda.

Sasa swali la kujiuliza Je Demand ya Pesa ya Kitanzania ni kubwa kiasi gani?Je Demand ya Dolar ni kubwa kiasi gani?

Ila pia napenda nikugusie kidogo kuhusu kitu kinaitwa Purchasing Power Parity.Hapa Unapaswa Ujiulize Je Kwa Sasa hivi Dola Moja Ya Marekani ni Sawa na Shiling 2600 na Mwaka 1960 ilikuwa sawa na shiling 7 Je Shilingi saba ya mwaka 60 huku Tanzania ilikuwa na uwezo wa kununua sukari kiasi gani na Je Dola Moja huko Marekani ilikuwa na uwezo wa kununua Sukari kilo Ngapi? Na Je kwa mwaka huu 2024 ambapo dolar 1 ni Sawa na 2600 inatosha kununu sukari kilo ngapi Marekani na Tanzania?

Pili Unataka utazama GDP ya Tanzania na Ya Marekani kwa Mwaka 1960 na 2024 na ya Tanzania vivyohivyo Je Ratio ikoje?Imebadilika kwa kiwango gani?

Ukishatazama hayo yote utaelewa ni nini kiilipelekea Hayo.

Cha MUhimu ni uelewe tu kwamba Unaweza kuchagu bidhaa yoyote hata Petrol.hata soda n.k.Nimechagu sukari kwa ajili ya ulinganisho tu,ila tafuta bidhaa ambayo unaweza pata bei yake kwa urahisi na uhakika.

Kila la heri
 
Kuna sababu kadhaa kama vile;
1. Ushauri wa
IMF wa kushusha thamani ya shilingi (ambao Mwalimu na washauri wake wa uchumi waliukataa katakata) wakati wa SAP.
Kuna economist mmoja alinieleza kuwa uchumi wa Tz ulianza kushuka kuanzia 1974 na baadae ndiyo ulipiga mbizi kabisa baada ya vita vya Idi Amin. Kumbuka 1972-3 ndiyo ile sera ya vijiji vya ujamaa ilipamba moto kwa hivyo kilimo kiliathirika sana na matokeo yake njaa ilikumba nchi. Sijui kama kile kitabu cha Rev C. K. Omari bado kinapatikana au la, alieleza vizuri sana kuhusu hili.

Hapo ndipo walikuja IMF na sera zao za devaluation na Nyerere aliwatimua, wakakorofishana na Mtei naye akautema uwaziri wa Fedha. Tulifanya maandamano kusupport fikra sahihi za `Mwalimu Nyerere za kutogeuka nyuma ili tusigeuke mawe. Vita ya Idi Amini ilikuja kugongea msumari kwenye jeraha kwa kutumaliza kabisa, kila kitu kilikuwa foleni hata sabuni ya mawingu ilikuwa inauzwa kwa foleni. Huko mikoani hata nguo za kuvaa zilikuwa shida.

Na huku tulikuwa na kambi kibao za wakimbizi wa Zimbabwe, Afrika ya Kusini, Angola..... kwa hivyo wazungu nao waligoma kutusaidia isipokuwa wachache waliokuwa wanasupport ukombozi wa Afrika.

Tulipobanwa ukutani na kuishiwa pumzi IMF walikuja tena na Structural Adjustment Program yao, Nyerere akaona bora zigo la misumari amrushie Mwinyi na hapo hdiyo fedha ilianza kupiga mbizi lakini kidogo tulipata afweni ya maisha. Vitu vikaanza kupatikana na tulianza kurudi katika hali ya kibinadamu.

Nyinyi GenZ munaojifanya wajuaji nchi hii imetoka mbaaaaaali sana!
 
Hujajieleza unakusudia nini. Inawezekana unachofikiri unanieleza nakielewa vizuri kuliko unavyofikiri.

Kwa nini hutaki kukitaja?

Hukielewi? Unaogopa? Una nature ya kichawichawi ya kujifichaficha?

Sijatoa hoja yoyote inayohusu pesa kutumiwa kwenye nchi nyingi. Habari ya pesa ya China kutumika nchi ngapi inakuja vipi kwenye hoja zangu?

This question is totally invalid, it is not related to my point at all.

You are making a logical non sequitur fallacy. Unaingiza hoja tofauti na ninayoiongelea mimi.

Hoja yangu ni kwamba, thamani ya pesa ya nchi si lazima iendane na uzuri wa uchumi wa nchi hiyo.

Hoja hii nimeitokea mfano wa Kenya na Japan.

Shilingi moja ya Kenya in athamani kuliko Yen moja ya Japan.

Shilingi moja ya Kenya ni sawa na 1.19 Japanese Yen.

1 Japanese Yen ni 0.85 Kenyan shillings.

Je, hilo linamaanisha Kenya ina uchumi mzuri kuliko Japan? Hapana.

These are hard numbers, not some blah blah about "tulia ufikirie vizuri utaelewa".
Nani anaitumia hiyo Japanese yen ?
 
Nani anaitumia hiyo Japanese yen ?
Umuhimu wa swali lako ni upi?

Kwani hoja ya mada hii ni pesa inayotumiwa na wengi au pesa yenye thamani kubwa?

Mbona unaondoka kwenye hoja ya uzi huu, thamani ya pesa, halafu unaleta hoja yako tofauti, wingi wa watu wanaoitumia pesa?

Unaelewa kuwa hizo ni mada mbili tofauti?
 
Ok sawa
 
Back
Top Bottom