Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Fungua kiwanda Cha midoli,makasha ya sabuni,tooth pick nk.. unasubiri nani afungue!?
Serikali ndiyo mbia wa kwanza. Anatakiwa kuwezesha mazingira ya hili kufanyika. Kutoa nafuu ya kodi, kuwezesha kupatikana mtaji, kulinda soko nk nk. Nchi zote zilizoendelea kwa viwanda serikali zao zimeplay part kubwa kuliko wenyewe waliofungua viwanda.
 
Ile vita ndio ilituletea shida zaidi ndipo mabeberu wakawa wamempata Mwalimu pale walipomtaka awepo !

Wakubwa wa magharibi walikuwa wanajua kama sera za Ujamaa zitapata mafanikio Nchi nyingi Africa zitafuata zile policy na wao mirija yao ya unyonyaji itakuwa imefikia mwisho wake !!

Baada ya ile vita wakajua sasa Mwalimu hana tena ujanja mwingine na ndipo wakashikilia hapo hapo, kwamba kama unataka mikopo shusha thamani ya pesa yenu !

Ujanja wetu ukaishia hapo 😳🙌
ujamaa ni mtamu kwenye makalatasi tu..
nje hivyo vita kufeli kulikiwa pale pale.
 
1. No balance of Trade: Much higher import than export, with almost zero export.
2. Money devaluation and higher inflation rates.
3. Bad if not worse Politics Regime within the Country, ambazo kwa upande mwingine zimesababisha 'uncertenities' katika nyanja zote kabisa za maisha ya Wananchi.,
4. Elimu duni na isiyokuwa sahihi kwenye masuala ya Uchumi, ikiwemo na Financial Economics, n.k, n.k.
Tatizo ni kwamba kumekuwepo dharau kubwa za professions hapa Tanzania hasa kwa wakurugenzi wa juu
Mtu ni kada wa ccm huko kasoma sociaology anakuja kuwa Waziri wa fedha.

Katiba mbovu kwamba Waziri lazima awe mbunge. Je kama wabunge ni vilaza? Ndo majibu haya sasa
 
Mfumo wa uongozi [Political instability], Utofauti kwenye Interest rates.. NI moja ya visababishi
 
Wachina wanajitahidi sana pesa yao isipande thamani.

Ikipanda wanaishusha kwa makusudi.

Kimkakati, ili uchumi wao unaotegemea exports ufanye vizuri.

Wanaona pesa yao ikiwa na thamani ndogo ndiyo itachochea uchumi wao kuwa mzuri. Kwa kuchochea exports zaidi.

Pesa kuwa na thamani kubwa au ndogo si tatizo.

Tatizo ni, una mkakati gani wa kuitumia thamani yoyote ya pesa yako ili uwe na uchumi mzuri.

Tatizo hatuna strategy hata ya kutumia hiyo pesa isiyo na thamani kuwa na uchumi mzuri.

Tungekuwa na strategy kama ya China, tungeweza kuipigania pesa yetu isipande thamani na vile vile kujenga uchumi mzuri wa export.

Tatizo si thamani ya pesa, thamani ys pesa hata Benki Kuu inaweza kuibadilisha siku moja tu.

Tatizo ni uzalishaji, tatizo ni mkakati.
Pesa ya China inatumika nchi zipi na zipi kama official currency for payment ?
 
Serikali ndiyo mbia wa kwanza. Anatakiwa kuwezesha mazingira ya hili kufanyika. Kutoa nafuu ya kodi, kuwezesha kupatikana mtaji, kulinda soko nk nk. Nchi zote zilizoendelea kwa viwanda serikali zao zimeplay part kubwa kuliko wenyewe waliofungua viwanda.
Subiri mdau mkuu serikali kukuwekea mazingira mazuri na kukusaidia kupata mtaji
 
Five years after independence in 1961, the Tanzanian shilling replaced the East African shilling as the nation's official currency.
Sawa kabisa, AlhamduliLlah nilikuwepo.

Sasa post namba moja ametaka kutupiga porojo, watu tuliotumia za King george na za mmasai.
 
Ndio hiyo dola kubadilika wao ndio wanauchumi wa nchi tangia uhuru
 
Back
Top Bottom