Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Nini kilipelekea 1 Us dollar kubadilishwa kwa shilingi za kitanzania 7 mwaka 1960 mpaka shilingi 2600 mwaka 2024 ?

Nawaonea huruma sana watoto wetu maana miaka inavyo enda hii nchi inazidi kua ya ovyo amna ajira..amna uwekezaji amna viwanda, mazingira ya uwekezaji niya ovyo ovyo
Wataandamana wajikwamue
 
Wachina wanajitahidi sana pesa yao isipande thamani.

Ikipanda wanaishusha kwa makusudi.

Kimkakati, ili uchumi wao unaotegemea exports ufanye vizuri.

Wanaona pesa yao ikiwa na thamani ndogo ndiyo itachochea uchumi wao kuwa mzuri. Kwa kuchochea exports zaidi.

Pesa kuwa na thamani kubwa au ndogo si tatizo.

Tatizo ni, una mkakati gani wa kuitumia thamani yoyote ya pesa yako ili uwe na uchumi mzuri.

Tatizo hatuna strategy hata ya kutumia hiyo pesa isiyo na thamani kuwa na uchumi mzuri.

Tungekuwa na strategy kama ya China, tungeweza kuipigania pesa yetu isipande thamani na vile vile kujenga uchumi mzuri wa export.

Tatizo si thamani ya pesa, thamani ys pesa hata Benki Kuu inaweza kuibadilisha siku moja tu.

Tatizo ni uzalishaji, tatizo ni mkakati.

Hapa umenena kweli kabisa nakunukuu in red

Tatizo hatuna strategy hata ya kutumia hiyo pesa isiyo na thamani kuwa na uchumi mzuri.
 
Back
Top Bottom