John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Ni ngumu Sana kurekebisha hali Kama hiyo, ni suala mtambuka.Kwa hiyo ndiyo kusema Wachumi wote waliojazana serikalini wamekosa kabisa suluhu ya kuirejesha thamani ya shilingi yetu!! Yaani miaka inavyozidi kwenda na thamani nayo inazidi tu kushuka!!
Je, Wananchi wenyewe kwanza wanazo akili (elimu) nzuri na zilizo stable sawa sawa katika kufanya Utafiti, Ugunduzi Mpya, Uvumbuzi na Bunifu mbali mbali zitakazosaidia katika kuzalisha bidhaa mbali mbali ambazo pia zitasaidia kuongeza Pato la fedha za kigeni hapa Tanzania????
Nguzo Kuu kabisa ya Uchumi wa nchi yoyote ile hutegemea zaidi na Ubora wa akili (elimu) walizonazo Wananchi wake katika nchi husika.
Kama Wananchi/Watu wengi katika nchi Wana AKILI NZURI Zaidi, basi upo uwezekano mkubwa sana wa nchi husika kuwa na Uchumi mkubwa, and vice versa is also true.