Kwangu mimi,nimekuwa na itikadi za mrengo wa kushoto dhidi ya serikali,nimesoma sana magazeti ya ya MwanaHalisi na Tanzania Daima yalikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya serikali. Wanasiasa kina Slaa,Zito Kabwe,Kafulila,Mnyika,Mchungaji Msigwa,Prof Kitila Mkumbo,Prof Mwesiga Baregu na wengineo walikuwa wananikosha sana Na Agenda kubwa ya Ufisadi katika Serikali. Mara tuliyeaminishwa ni fisadi mkuu akaingia Chadema,akawa mgombea uraisi,tulioamini wanajua zaidi tukawasikiliza wakabadili kauli,Lowasa sio Fisadi. Kwangu ilikuwa ngumu kumeza,nilikataa kuwa bendera fuata upepo. Imani yangu kwa Chadema na itikadi zao ikaishia hapo.