Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

Kila tukikutana badala ya kufurahi yeye ni kuelezea matatizo kila siku ana matatizo yeye tu hana hela yeye tu kukopa kopa nikakaa mbali nae maana alikuwa hanipi furaha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilitembea na mama yake,akajua urafiki ukafia hapo[emoji23]
 
Zipo sababu nyingi za kutengana na marafiki ila kwa upande wangu ni

Ubinafsi na dharau plus kujisikia flani hivi....

Yani mshikaji wako anajali mambo yako yaende wewe ukwame.


kuna mmoja huyo toka alivojipatia kazi sehemu akaanza kujikuta busy nikampunguza.
 
Ubinafsi,yan kwenye shida zake unapambania kadiri ya uwezo wako ila zako hazimuhusu,unamshirikisha mambo yako ila yeye yake ni siri,mwisho wa siku kuna changamoto ilitokea kazin kwangu,so utaratibu ikawa ni upate mdhamini au uende rumande,jamaa nikamwelekeza akanambia nakuja fasta halafu akazima kabisa simu,uzuri kuna jamaa alikuwa nae mda huo ndio akanijuza kuhusu mpango wa jamaa,Mungu mwema,ndani ya saa moja nililopewa nitafute mtu anidhamini nikakutana na bro mmoja aliwaipata shida halafu mfukoni hana kitu nilimsaidia tu kama mwanaume mwenzangu,yule bro ndio akaja kuniwekea dhamana,police wakamaliza uchunguzi wao,wakawapata waarifu wao wengine kazini maisha yakaendelea fresh,ukaribu ulifia hapo,lakini nilipata somo kuwa unapokuwa na nafasi we saidia tu hata kama mtu humjuwi maana hujuwi kesho yako itakuwaje,yule jamaa huwa tunaonana mara chache sana,ila Mungu ni fundi sana kudadeki
 
Duh, si sngekwambia tu ukweli
 
Japokuwa mwabmba alizingua, ila amekupa somo kubwa sana Mkuu na wengine tuchukue notes
 
Unamtafutaje mtu anayekukwepa Mkuu, ukipiga simu haishikwi?
 
Nliua nilipoona jamaa kantumia message KANIMISS
Sasa kuna ubaya gani wa kukumiss Mkuu, au ulitaka akwambie kibishi.... "We mjinga (au tusi kubwa zaidi) kitambo sana.... hapo ingekuwa freshi?
 
Umenikumbusha rafiki yangu mmoja, huyu jamaa atakucheki muda wa kula bata tu, yuko radhi hata akutumie usafiri ukaungane nae, ila ukiwa na shida uombe msaada hata wa elf 10 humuoni. Kuna muda alikwama sehemu akata hela ya mafuta kwa wakati huo sikuwa nayo ila kulikuwa na hela yafanyia jambo lingine nikamwambia naichomoa huku ila unirudishie kesho, maana alidai mtandao umemsumbua ameshindwa kutoa hela, alikausha mazima hakurudisha ile hela mpaka kesho, na ilinihangaisha kidogo sababu nilichomoa sehemu ambako ilikuwa na kazi nyingine. Nikasema freshi atapata tu shida siku nyingine

Baada muda kupita siku akarudi na pigo zile zile, this time nilikuwa nayo ila nikakausha, akalalama wee ndio ikawa imetoka hiyo!
 
Jinga kabisa 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…