Vitambi kwa wanaume ni jambo ambalo linajulikana limekuwepo karne zote lakini wimbi la wanawake kuwa na vitambi kote duniani lilianza takribani miaka ya 2000's. Nini hasa imechochea wimbi kubwa la wanawake kuwa na vitambi mijini na vijijini?
Kuna mmoja nilikutana nae she was uncomfortable!, maana alifikia mpaka akaanza kunionyesha picha zake za zamani alivyokuwa hana kitambi!.
ni kama mtu anakwambia "usiniache zamani sikuwa na kitambi!"..🤣
Okay ipo hivi, life style ndo imekuwa changamoto kubwa sana watu tunakula kwa ratiba kwasababu ndo umeshakuwa mfumo!, yani asubuhi unakula, mchana unakula na usiku unakula! haijalishi umesikia njaa ama hujasikia!. hiyo sio tabu sana japo ni mchawi pia, mchawi mkubwa ni huyu "Tunakula sana vyakula vya wanga!".
Asubuhi
chapati na supu
Mchana
Ugali, maharage,mboga ya majani,nyama na coca baridi..😅
Usiku
Wali na broiler ama biriani au tambi na minyamanyama!.
Tuje kwenye kazi, huyu mtu kazi anayofanya sio ya purukushani yakumtoa jasho na hana ratiba ya mazoezi, unategemea hizo sukari zilizoingia hapo zitaenda wapi..??
ulaji unatakiwa utegemee na kazi na ndio maana ni ngumu kukuta mtu anaefanya kazi ngumu kuwa na likitambi!.
watu tibadilishe life style zetu.