Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
- Thread starter
-
- #21
Kila jambo hujadiliwa Kwa wakati wake. Hizo 30.16% zilizopungua Tanzania na kuingia kupitia Kenya ni Hela hizo.Yaani tuko bize kujadili uingizwaji wa goods ambazo hatujui zimetengenezwa wapi! BADALA ya kuhoji uhalali wa WanyaRwanda waliopenyezwa kwenye idara nyeti za nchi hii
Hizo ni porojo ndefu umeandika. Mojawapo wa vipengele vya mkataba wa DPW ni kuwapa elimu wa wafanyakazi pale bandarini, maana yake ufanisi unakuwa mdogo kwa sababu wafanyakazi hawana viwango vya kisasa vya elimu za bandari.Hizo porojo. Rushwa iko TRA ndio maana wafanyabiashara wa Kariakoo hadi sasa wanalia. Ili mzigo utoke kazime uwe na TRA clearance. Sio DP WORLD
Pili Kabla ya kuja hao DP World kuna uwekezaji mkubwa ulifanyika kwa mkopo wa World Bank na kwa kawaida kabla ya investment huwa tunafanya economic analysis ya projected income kwa miaka kadhaa, sasa kabla hujawasifia tafuta data kwa ule mkopo tuliokopa mapato yangekuwa kiasi gani ( net income) ambayo yote yalikuwa yanaingia hazina kwa asilimia 100. Kisha chukua baada ya kuja DP World mapato ni kiasi gani then ondoa kile wanachochukua DP World na tazama kile kunachoingia Hazina baada ya kugawana na DO World kisha ltoa kile tunacholipa mkopo wa Workd bank then lnganisha kinachobaki na kile ambacho tungepata kutokana na ule mkopo wa Works bank kama tungebaki pwke yetu
Baada,ya hapo ndio useme kama tunanufaika au la.
Takwimu sio za kuziamini sana muda wote. Kuna kipindi zinapikwa kisiasa.Steven Joel Ntamusano haya unayoandika yanajibu ni Kwa nini sisi tumeshuka kwa 30.16% na huku Kenya wameongeza upelekaji mizigo Rwanda kwa 361.43%
Huoni kama Kuna tatizo hapo?
Wakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.
Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.
Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.
Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya bahari. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.
Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.
Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.
Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.
Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.
Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .
Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.
Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.
Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.
Katika hizi takwimu, Kwa nini Rwanda ipike hizi takwimu na inafaidika vipi?Takwimu sio za kuziamini sana muda wote. Kuna kipindi zinapikwa kisiasa.
Umeongea mambo mengi sana ya maana. Hili la mwisho linafikirisha Sana.Tuendelee tu kutekana na kuuana wakati wengine wakipanga mipango imara ya kunusuru nchi zao kiuchumi.
Siasa chafu za chuki za chadema
Ndiyo zimesababisha Rwanda wahame?Siasa chafu za chuki za chadema
Kama kipindi cha Magufuli, data zilikuwa zinapikwa hadi inakuwa aibu.Takwimu sio za kuziamini sana muda wote. Kuna kipindi zinapikwa kisiasa.
Umemuweza!National institute of statistics of Rwanda. "Formal external trade on Goods" .
Chakarika.
Deal la nchi tatu za afrika mashariki na DPW ni kubwa na lilipangwa miaka kadhaa iliyopita.Katika hizi takwimu, Kwa nini Rwanda ipike hizi takwimu na inafaidika vipi?
Jee takwimu sahihi ni zipi tofauti na hizi?
Unajuaje kuwa hata hizi za Bongo hazijapikwa?Takwimu sio za kuziamini sana muda wote. Kuna kipindi zinapikwa kisiasa.
Tanzania hawafanyi utafiti shindani wa masoko, wao wanaamimini wateja watakuja tu, hata kama wana tozo za ajabu ama mapungufu, pia wanadhani wateja ni wajinga na wapumbavuWakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.
Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.
Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.
Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.
Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.
Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.
Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.
Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.
Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .
Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.
Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.
Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.
Yaani tuko bize kujadili uingizwaji wa goods ambazo hatujui zimetengenezwa wapi! BADALA ya kuhoji uhalali wa WanyaRwanda waliopenyezwa kwenye idara nyeti za nchi hii