Nini kimeifanya Rwanda ipunguze kupitishia mizigo Tanzania na kugeukia Kenya?

Nini kimeifanya Rwanda ipunguze kupitishia mizigo Tanzania na kugeukia Kenya?

Lucas Mwashambwa hajapita hapa?
Wakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.

Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.

Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.

Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.

Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.

Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.

Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.

Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.

Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .

Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.

Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.

Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.

Wakipita huko Kenya wanajiumiza wenyewe maana unafuu ni bandari ya daslamu
Shauri yao bwana! Hiyo inaitwa hasira ya Mkizi!
 
Taja wawili tu kwa mfano ambao wapo serikalini na sio watz?

Mkuu wenu wa majeshi aliropoka hadi Leo hajataja hata mmoja ili achukuliwe hatua. Mnapenda sana story za vijiweni.
Hizo hatua unachukua wewe?
 
Wakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.

Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.

Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.

Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.

Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.

Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.

Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.

Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.

Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .

Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.

Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.

Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.
watanzania kila siku nasema, Rwanda ni kanchi ambako tunatakiwa kukaweka second choice after Burundi. hii ni kwa sababu wao ni landlocked lakini huwa wanapenda kutuendesha wapendavyo. kipindi cha kikwete walipogundua mizigo mingi inapita kwao kwenda congo, walipandisha ushuru wa kupitishia kwao hadi laki 5 kwa lori moja, na kipindi cha corona wakalazimisha magari yakifika boda madereva wao ndio wapokee. sasa, dawa yao ni moja tu, tuchepushe njia tuwe tunapiga Burundi ili wao watutafute wenyewe badala ya sisi, anajua sana udhaifu wa viongozi wetu na hutumia hiyo kama fimbo kuwachapa. reli ya SGR na barabara to congo pitishia both burundi na rwanda ili kama kagame (ambaye umri umeenda muda wowote anakata) wakileta kiburi still tutakuwa na option wateja wetu kupitia burundi kwa raha zao. rwanda kadanganya viongozi wetu waingie mkataba na DP WORLD kwa sababu yeye anajenga bandari kavu ya DP world pale rwanda ili mizigo ya congo itue pale kwake kwanza na apige ushuru. yaani hana bahari ila anatuzidi akili kwamba mizigo ipite hapa kwetu ikatue kwake yeye apige ushuru, na viongozi wetu wametoa mimacho tu. kama hiyo dp world yake atategemea mombasa peke yake, basi ngoja tuone.
 
Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini. Bandari za Rwanda ni zile zilizoko kwenye ziwa Viktoria.
Mkuu 'Allen', leo vipi. Mbona andiko lako limekaa isivyo kawaida yako?
Kwanza kabisa unachepukia kwa Mwigulu, bila ya muunganisho na mada unao eleweka. Sasa tena unazungumzia bandari zipi za Rwanda zilizopo ziwa Victoria?

Hata hivyo, nikichangia mada yako husika; Rwanda ni jirani asiye aminika kabisa. Kila mara anachokonoa chokonoa jirani zake katika maswala mbalimbali.
Kwa hali ya kawaida, Rwanda hana sababu hata moja ya kupitisha mizigo yake Mombasa; kwa sababu huko ni mbali, na zaidi inabidi avuke mipaka mingi.

Sasa, kutotumia bandari ya Dar es Salaam hata wakati inaonyesha ufanisi katika kuondosha mizigo, inawezekana pakawepo na sababu zingine; labda aina ya mizigo anayo ipitisha, kuwa hataki ionekane na ijulikane na hao wanao ipitisha. Kama si hivyo, ni kiburi na ujinga tu; kwa maana jiografia hana uwezo wa kuibadilisha.

Jambo ambalo haitafaa tumruhusu ni kupitisha mizigo Mombasa, halafu ailete kupitia Tanzania kwenye ile barabara toka Arusha hadi Singida. Kama akitaka hivyo, na tayari anasaidiwa na marafiki zake huko kulazimisha iwe hivyo; basi hana budi kulipia matumizi stahiki ya barabara hizo.

Rwanda chini ya Kagame, usitegemee kuwepo na mabadiliko katika misimamo isiyo ya kueleweka ya nchi hiyo.
 
Mbongo siku zote huona mabaya tu, hanaga matumaini kichwani mwake.
Na wewe usiye 'Mbongo', unaona mazuri tu, hata yasiyo kuwepo!
Hizo porojo. Rushwa iko TRA ndio maana wafanyabiashara wa Kariakoo hadi sasa wanalia. Ili mzigo utoke kazime uwe na TRA clearance. Sio DP WORLD

Pili Kabla ya kuja hao DP World kuna uwekezaji mkubwa ulifanyika kwa mkopo wa World Bank na kwa kawaida kabla ya investment huwa tunafanya economic analysis ya projected income kwa miaka kadhaa, sasa kabla hujawasifia tafuta data kwa ule mkopo tuliokopa mapato yangekuwa kiasi gani ( net income) ambayo yote yalikuwa yanaingia hazina kwa asilimia 100. Kisha chukua baada ya kuja DP World mapato ni kiasi gani then ondoa kile wanachochukua DP World na tazama kile kunachoingia Hazina baada ya kugawana na DO World kisha ltoa kile tunacholipa mkopo wa Workd bank then lnganisha kinachobaki na kile ambacho tungepata kutokana na ule mkopo wa Works bank kama tungebaki pwke yetu
Baada,ya hapo ndio useme kama tunanufaika au la.
Ni mara ngapi tumejibishana juu ya haya aliyo eleza hapa mkuu 'RMC'.
kama kawaida yako, maneno ni yale yale tangu DP World aingie ; na wewe ndio wakati ule ule ukaajiriwa kuingia JF kupambania mradi!
 
SGR ya Kenya itapita Uganda hadi Rwanda na kuunganisha Tanzania
Nashangaa hujasikia barabara inayo jengwa toka Malindi, kupitia Mombasa hadi Bagamoyo.
Kwa nini wasubiri SGR kukamilika miaka yote hiyo wakati tayari Mombasa inatumiwa na mikoa yote ya Kaskazini mwa Tanzania; na sasa barabara inayoingia Singida ipo tayari kupeleka mizigo toka Mombasa hadi Rwanda na Burundi; na hatimae mikoa yote ya Ziwa ya Tanzania!
Acha Dar ibaki kuhudumia Morogoro, na mikoa mingine ya Kusini na Nyanda za Juu!
Ujuha wa nchi hii unapatikana sehemu chache sana duniani.
 
Wamiliki wa DPW walianza kusaini mikataba na Raiis Tshisekedi kule DRC wakaja kwa Kagame kisha wakamaliza na Samia, ni biashara kubwa sana ya logistics inakwenda kufanyika baada ya SGR kuwa imekamilika kujengwa.
Kenya wanatumia SGR au nao ni barabara kama chichi
 
Hiyo reli ya SGR inakwenda kuchukua mzigo wa Rwanda kutoka kwenye yard ya pale Kigali kuuleta TPA, kuna neema kubwa na haina miaka mingi kuanzia leo,
Hivi haya maneno uli yakariri kwamba hata siku moja hayabadiliki?
Unajua leo Treni la abilia limezima Tena pwani ?

Abilia tu shida mizigo ndio mtaweza? Ninaashaka makubwa na utendaji mipango wabongo tunaongiza Ila utendaji sasa
Sita shangaa ukipata jibu toka kwa 'Steve' kuwa hiyo reli wapewe DP World; lakini ukimwambia tuwape serikali ya mama na mama mwenyewe akae pembeni; hapo hutapata jibu.
 
Back
Top Bottom