Nini kimeikumba Airtel? Wameuza minara yake yote na kugeuka wapangaji!

Yaani unaunza nyumba halafu unaenda kupanga tena nyumba ulioiunza unapanga hiyohiyo .
Hapo kutakuwa na kitu kimejifiza nyuma ya panzia tu
 
Ngoja nifafanue kidogo,

Kwenye hii sekta ya Mawasiliano umiliki wa minara huenda sambamba na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutafuta location, kujenga minara, kuifanyia marekebisho Mara kwa Mara, kuhakikisha muda wote site iko hewani, kushughulikia umeme wa site na kuweka mafuta kwenye Standby Generator, Ulinzi n.k. Yote Haya yanagharimu pesa nyingi.

Sasa makampuni ya Mitandao (i.e Voda, Tigo na sasa Airtel) yalijikuta katika wakati mgumu kuingia gharama za kujenga minara na baada ya hapo kuihudumia kila siku. (Ni sawa na mtu ulazimike kujenga nyumba kubwa ambayo kiuhalisia unahitaji hapo chumba kimoja tu). Kwamba lazima ujenge mnara wa mita hamsini ilhali kiuhalisia unahitaji nafasi ya mita tatu tu kati ya hizo hamsini zote.

Sasa ili kuepuka huu usumbufu ndipo wakaamua kuuza minara ambayo tayari walikwisha ijenga na kisha kuwa wapangaji, na yule anayeinunua anakupangisha wewe na wenzako wengine kwenye mnara huo huo uliomuuzia i.e Tigo, Smile, TTCL, Halotel etc..

Tuchukulie mfano maintanace cost ilikuwa inakugharimu Tsh. 20 kwa mwezi ila mtu anakwambia umuuzie kisha akupangishie kwa Tsh. 10 kwa mwezi na hapo unaondokana na stress za site kuzima, kuibiwa vifaa na Mafuta n.k kwa makubaliano kuwa ikitokea usipokuwa hewani kwenye huo mnara yeye mpangishaji anakulipa fidia..

Kifupi hili walilofanya Airtel sasa, lilitarajiwa kufanyika nadhani miaka ya 2016/17, ila Serikali kaweka pingamizi baada ya kubaini kuwa Airtel alipora miundo mbinu mingi ya Serikali kipindi kile TTCL imekufa.. Ndiyo maana mpaka Leo Serikali ina fungu lake ndani ya Airtel.
 
Nimekuelewa..
 
Running cost ni kubwa, wamewauzia RAHA TOWER .

Pia wameuza ghorofa lao pale Morocco kwa dola milioni 172.

Ghorofa hilo siyo lao kama sikosei ghorofa ni la UWT
 
Hamjioni kuwa mnaonekana wajinga!
Sasa Lissu ameingiaje hapa?
Tatizo majadiliano ya kitaalamu mnaingiza u- kada wa chama.sio kila kitu lazima muingize mambo ya siasa,

Mkae kwa kutulia mjifunze kupitia michango ya wataalamu wa biashara.
 
Ni kitu Cha kawaida sana kwenye biashara maana ataachana na kufatilia mambo ya ujenzi wa minara, kuweka walinzi, majenereta, mafuta.

Voda na Tigo waliishauza yao kwa HTT tangu 2014
Wewe umetoa jibu zuri. Kuna wengine hata kufikiri mara mbili hawawezi. Unajua kampuni zinapiga mahesabu: gharama ya kusimamia minara vs kukodi. Bila shaka wameona kukodi inalipa zaidi. Ni kama unavyokuta kampuni kama Voda mambo ya customer care walivyo outsource. Au unakuta kampuni badala ya kaajiri vibarau eg wa kufanya usafi wanawapa tenda kampuni nyingine.
 
Yaani unaunza nyumba halafu unaenda kupanga tena nyumba ulioiunza unapanga hiyohiyo .
Hapo kutakuwa na kitu kimejifiza nyuma ya panzia tu
Mkampuni mengi duniani yanafanya hivyo. kuendesha ile minara siyo kitu rahisi kama unavyodhani. Kuna kampuni moja yenye mtandao wa maduka makubwa Europe juzi juzi wameuza moja ya majengo yake makubwa yalikuwa na maduka halafu wakaendelea kuwa wapangaji.
 
Hiyo deal ilikua iende kwa American Towers Ila walikumbana na vikwazo wakasepa lakini naona wamekuja Kwa mlango wa nyuma tena.(paradigm)
 
Running cost ni kubwa, wamewauzia RAHA TOWER .

Pia wameuza ghorofa lao pale Morocco kwa dola milioni 172.

You can't be serious..revisit your article comprehension skills. Kuna jengo Tz hii lina gharama ya dola milioni 172?
 
Ngoja nifafanue kidogo,

Kwenye hii sekta ya Mawasiliano umiliki wa minara huenda sambamba na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutafuta location, kujenga minara, kuifanyia marekebisho Mara kwa Mara, kuhakikisha muda wote site iko hewani, kushughulikia umeme wa site na kuweka mafuta kwenye Standby Generator, Ulinzi n.k. Yote Haya yanagharimu pesa nyingi.

Sasa makampuni ya Mitandao (i.e Voda, Tigo na sasa Airtel) yalijikuta katika wakati mgumu kuingia gharama za kujenga minara na baada ya hapo kuihudumia kila siku. (Ni sawa na mtu ulazimike kujenga nyumba kubwa ambayo kiuhalisia unahitaji hapo chumba kimoja tu). Kwamba lazima ujenge mnara wa mita hamsini ilhali kiuhalisia unahitaji nafasi ya mita tatu tu kati ya hizo hamsini zote.

Sasa ili kuepuka huu usumbufu ndipo wakaamua kuuza minara ambayo tayari walikwisha ijenga na kisha kuwa wapangaji, na yule anayeinunua anakupangisha wewe na wenzako wengine kwenye mnara huo huo uliomuuzia i.e Tigo, Smile, TTCL, Halotel etc..

Tuchukulie mfano maintanace cost ilikuwa inakugharimu Tsh. 20 kwa mwezi ila mtu anakwambia umuuzie kisha akupangishie kwa Tsh. 10 kwa mwezi na hapo unaondokana na stress za site kuzima, kuibiwa vifaa na Mafuta n.k kwa makubaliano kuwa ikitokea usipokuwa hewani kwenye huo mnara yeye mpangishaji anakulipa fidia..

Kifupi hili walilofanya Airtel sasa, lilitarajiwa kufanyika nadhani miaka ya 2016/17, ila Serikali kaweka pingamizi baada ya kubaini kuwa Airtel alipora miundo mbinu mingi ya Serikali kipindi kile TTCL imekufa.. Ndiyo maana mpaka Leo Serikali ina fungu lake ndani ya Airtel.
Hapa mi najiuliza. Kama kupaendesha patakugharimu tsh 20 na ukipanga unapalipia tsh10 wakati uliyemuuzia anapaendesha kwa gharama zilezile ambazo umezikwepa wewe. Je nikivipi atapata faida?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mnara mmoja anapangisha kampuni hata 4, hapo anakuwa kapata tsh 10. Faida tsh 30
 
Hii tofauti mkuu, Airtel mwanzo alikuwa mmiliki wa minara, ameamua kuiuza na kuwa mpangaji. Ni sawa na wewe ujenge nyumba, uamue kuiuza kisha umwambie uliyemuuzia akupangishe.

The same to voda na tigo walikua wanamiliki wakauza so walichofanya airtel sio kigeni….. wanapunguza management headache na kuongeza ufanisi zaidi
 
Running cost ni kubwa, wamewauzia RAHA TOWER .

Pia wameuza ghorofa lao pale Morocco kwa dola milioni 172.

Hukijui unachokiongea boss[emoji4] ghorofa dola million 172? Lile jengo kwanza sio lao wamepanga ni la manji
 
Hii tofauti mkuu, Airtel mwanzo alikuwa mmiliki wa minara, ameamua kuiuza na kuwa mpangaji. Ni sawa na wewe ujenge nyumba, uamue kuiuza kisha umwambie uliyemuuzia akupangishe.

Actually maintenance ya minara ni ghali zaidi. Bora kukodisha.
 
Back
Top Bottom