Nini kimelikumba Jeshi letu? Imekuwaje linatumika kwa ajili ya kampeni za CCM?

Hawawezi kukuelewa hawa wehu wanafikiri madaraka utapewa kwenye sahani
Kila mtu amepanga foleni uvcc awe mkuu wa wilaya, wao wanajiita wazalendo kumbe wajinga na wehu tu, watoto wa watawala wanapewa kila kitu wao kazi yao kuvishwa minguo ya kijani asubuhi hadi usiku.

Wakija humu wanalia lia mara sijui Abdul ana pesa, rizwani atakuwa rais.
Mtaamka!lini kuipigania nchi jama mnajipendekeza kutwa kucha.
 
JESHI NI CCM KINDAKI NDAKI TANGU UHURU NA HAIJAWAHI KUWA TOFAUTI.

TANU ILIFANYA MAJESHI YOTE NI CCM HAYO MENGINE NI YA MDOMONI TU.

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Hatunaga jeshi tuna mfano wa jeshi, ww ulionao wapi komando wa IDF anavunja mbao? Mtu anaingia jeshi mpaka anastaafu Tena cheo cha General hajawahi fanya operation yeyote ya kijeshi operation pekee kwao ni kugombania mademu Bar ndio maana ukiwaona Wana vitambi mpaka unajiuliza hawa watu wanalinda nchi kweli?
 
Uhuru wa Nchi hii uliletwa na TANU na Waislamu wa Kariakoo na Yanga. Baada ya maasibya Jeshi 1964 ndipo Nyerere akalusuka upya Jeshi let kwa kutumia Vijana wa TANU Youth League, kwa hiyo TPDF haiwezi kusagau lilikotoks
 
Kwani Haujui kwamba Samia Suluhu Hassan Bado ni Rais wa JMT na ndiye Amiri Jeshi Mkuu?

Jeshi lazima limpe Ulinzi Hasa nyakati hizi ambazo Mh Rais yupo katikati ya watu wengi(Mass)

Mnalaumu vitu hata havina kichwa hata mguu!
Mbona haijawahi kutokea kwa Maraisi wengine waliopita,wakati wanafanya kampeni?
Kwa Mwinyi? Kwa Mkapa,JK na JPM?
 
Jeshi ta Tanzania sasa limekuwa kama jeshi la Kongo, hamna lolote. Sikutegemea kama jeshi letu pamoja na kupata habari za uhakika dhidi ya uhujumu uchumi wa CCM wakafanya ujinga huu.
 
Level hii bado sana kuwapata wabongo,kama wanaogopq hata virungu na mabuti ya FFU ndio utawapeleka porini wapambane na silaha kali za kivita?
Usifanye masihara
 
Hii nchi shamba la bibi, ukitaka kuielewa lazima uchizi, mambo ya hovyo hovyo yanaendelea mengi tu: Kila mtu sasa hivi ni mpigaji na dalali wa 10% ...Imagine askari wanawekwa kwenye ma-bus kupelekwa kwenye kampeni za CCM
 
Jeshi ta Tanzania sasa limekuwa kama jeshi la Kongo, hamna lolote. Sikutegemea kama jeshi letu pamoja na kupata habari za uhakika dhidi ya uhujumu uchumi wa CCM wakafanya ujinga huu.
Inasikitisha sana, ila ukiangalia kwa jicho la kiroho (spiritual eye) unaweza ukawa ni mpango wa Mungu, yaani zile taasisi nyeti (Usalama, Jeshi la Polisi na Jeshi la wananchi) ambzo zingekuja kuzuia raia siku ambayo hasira zao zimeamka kuutoa utawala, ni kama zimeanza kuvuliwa nguo na kuchonganishwa na Raia, na pengine kugawanyika.

we fikiria aibu hii ya Jeshi la wananchi walio ipata, yaani uzalendo wao wote umewekwa mashakani na wao wanajua, na ndani uko lazima watanyoosheana vidole kuwa uongozi wao wajuu wajeshi umewapaka matope mbele ya wananchi, maana sifa ya kwanza ya Jeshi la nchi yoyote ni kupendwa na watu ili siku ikitokea majanga basi wananchi wanakuwa nanyi na hata wengne kujitolea kusaidia kupambana na adui au kutoa msaada mwengne, ila mkichafuliwa na mkachukiwa na watu ambao ndo kimbilio lenu la mwisho siku za maafa basi Jeshi linatakiwa kufumuliwa ili kuleta imani na wananchi.

We kwa aibu hii unafikiri maandamano yakitokea, jeshi linaweza tena kuingia ikiwa tayari ishajulikana kuwa inalinda CCM kwa njia haramu, hapa Mungu karuhusu hili litokee ili wakose ile nguvu ya kunyooshea vidole wananchi siku ikifika maana kwasasa watajitahidi kurekebisha hii taswira mbaya iliyochafuliwa. Mi naamini huu ni mpango wa Mungu.
 
Na nafikiri 29 Oct, Samia atakuwa zanzibar kizimkazi, akiangalia kwa mbali hali ya hewa ya bara, kimenuka au kipo shwari.
 
kwa mujibu wa polepole MKUU WA MAJESHI awezi kuteuliwa kama hana card ya ccm
 
Una hoja usikilizwe ili kuanzisha jeshi labla ndani ya jwtz watokee wakuasi ili ligawanyike. Ila kuanzia chini ngumu watakudaka na kukupoteza mazima
 
Nani kaipa kibali cha kuingia nchini? CCM wana uwezo wa kukodi helicopter kutoka jeshi la Czech?
 
Na kwa taarifa yako huu mfumo nduo u ao ifanya Tanzania iwe na amani hadi sasa
 
Nadhan mfumo wa vyama vingi Tanzania Umekosa Tija. Itafutwe njia mmbadala. Kwa nje ni kama tunamfumo wa vyama vingi lakini kwa ndani ,vyama vya upînzani havitakiw
Kabisa
 
Kwani Haujui kwamba Samia Suluhu Hassan Bado ni Rais wa JMT na ndiye Amiri Jeshi Mkuu?

Jeshi lazima limpe Ulinzi Hasa nyakati hizi ambazo Mh Rais yupo katikati ya watu wengi(Mass)

Mnalaumu vitu hata havina kichwa hata mguu!
Mkuu reforms ni muhimu, kutenganisha explicitly shughuli za chama kutoka shughuli za serikali.

Kwa mazingira ya siasa zetu Mkuu, ili tutoboe ni lazima tutenganishe serikali kutoka Dola.

Bila hivyo tutaendelea hivi kwa miaka mingine 60!!!
 
Na kwa taarifa yako huu mfumo nduo u ao ifanya Tanzania iwe na amani hadi sasa
kuna amani Tanzania?? au amani kwako ni "absence of war/anarchy"??kama ni hivyo, basi u must be an imbecilic disgusting animal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…