Nini kimempata Aslay, Nyimbo zake kwa sasa zina shida gani?

Nyimbo zake znafanana kuanzia beats had melody.....binafsi hata hiyo nyimbo mpya sitak kuiskia nahis beat na melody ni zile zile tu...

Sema Natamba ngoma kal sana.
wimbo mpya nao sijaona utofauti wake na zilizo pita
 
Tatizo jamaa alikuwa anatoa ngoma mfululizo sana, then ladha ni ile ile. Ikumbukwe kuwa mpaka ikasikika jamaa alikuwa na daftari lote la ngoma za Yamoto Band.

Kumbuka binadamu tumeumbwa kuchoka pia.
Ajipange upya aje na sound tofauti inaweza msaidia.
 
aslay ni msanii wa kawaida sana sema mleta mada inaonekana ulimpa hadhi kidogo ndomana unashangaa
 
Ukigombana na Fella,tegemea anguko la mapema sana
CC Juma Nature.
 
Acheni kumpangia..muziki unatokana na hisia za mwanamuziki na mazingira anayopitia kwa wakati huo.Dogo ameachwa au ameporwa mchumba wake na wazee wenye kisu kikali. Hivyo,maumivu ya mapenzi ndio yanamfanya kuimba au kutunga hizo nyimbo zake.Hebu fuatilieni nyimbo zake na maneno yake hawezi kupiga beat za kuchezeka wakati anaisikitika.Yote kwa yote anafanya vizuri.
 
Amtafute Mwinjuma Muumini ampe ushauri.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Kuna kitu kinaitwa kupokezana kijiti,hauwezi kuwa namba moja milele,his career is over like Mike any one Tyson,Jacskon,Jordan.
 
ni kawaida kwa wanamiziki kupanda na kushuka,haijaanzia kwa aslay tu
 
Hata Mimi nimejikuta Sina vibe nae tena kabisaa yanii...!! Sijui why now namkubali Mbosoo zaidi
 
Kupitia aslay na Darasa inabidi Diamond platnumz tumheshimu sana..

Haijawahi kutokea Tz kwa msanii wa Bongo fleva kuwa nambari 1 kwa miaka 10 mfululizo....

Wamekuja watu wamekaa mwaka mmoja kwenye climax wamepotea ila huyu mshenzi tokea 2009 anaachia mawe tuu...

kila siku tunaambiwa atafulia ila ndio kwanza anabarikiwa , ukitaja ngoma 5 zilizofanya vizuri mwaka huu hapa bongo unakuta kwenye 2 au 3 yupo na Bado hapo nyimbo zake hazipigwi radio kubwa za Tz.. Diamond ni noma sana na anastahili heshima msisubiri ashuke ndio mje mseme jamaa alikuwa noma
 
Uko sahihi sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…