LGE2024 Nini kimetokea kiasi kwamba Wananchi hawataki kujiandikisha hadi wanafatwa majumbani na wanatoa majibu ya dharau kwa wahamasishaji?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wapi huko,huku nilipo mimi mtaa mzima wenye sifa wameshajiandikisha
Wasijiandikishe tu, ikibidi wakaishi kabisa na familia zao kwenye hivyo vituo vya kura hadi siku ya uchaguzi ili wapige kura vizuri kwenye hizo chaguzi za kikhanithi.
 
Ule ushenzi aliofanya Magufuli 2019/2920 ndiyo umewavunja moyo watu wanaona kumbe sanduku la kura siyo linalotoa mshindi bali matakwa ya mtawala.
Kweli kabisa, tuliona wazi uchaguzi ukinajisiwa, eti wanasema Magufuli anakubalika. Hata wakati wa Magufuli kulikuwa na wapiga kura wachache sana. Na sababu hasa ni ccm kumuachia mtu asiyejua siasa, akalazimisha kuwapa ccm kura za kihuni ili ionekane ccm inakubalika, sijui ni imara chini yake.

Kama kujiandikisha watu ni wachache hivi, basi uchaaguzi ndio utakuwa na watu wachache mno. Na uchaguzi mkuu ujao ndio itakuwa aibu. Na hao watu wachache ndio huwa kura za ccm kisha wanapora.
 
Upige kura usipige kura lazma ashinde.

Kiongozi mmoja wa serikali alisikika akisema 🤔
 
Yaan Leo walikuja wakagonga geti tukachungulia dirishan tulipo ona ni wenyewe na mikaratasi kwakweli sikwenda kufungua.Drama nyingi so mtu unaona haya mambo ya kujiandisha ni kiini macho tu
 
Walishajinadi kuwa "form ni moja tu"
Sasa kama ishu ipo hivyo mshindi si ashajulikana kwanini tupeane heka heka kupitia hekaya za kujifanya kura ni haki😁?
 

Kama MaCCM ya aina chaguzi, kuna sababu gani Wananchi kupoteza muda wao.

Mwenye Kifua Kipana tayari keshajipanga kukwapua uchaguzi, Wananchi wameshasoma mchezo, wanafanya vitu vyao.
 
Kuna kila dalili kilichofanyika katika uchaguzi wa 2020 kitajirudia tena ya nini kujichosha na misururu ya foleni.
 
Yale maneno ya Nape kule Kagera yamewatia baridi Wananchi labda !
😳🙄 !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…