LGE2024 Nini kimetokea kiasi kwamba Wananchi hawataki kujiandikisha hadi wanafatwa majumbani na wanatoa majibu ya dharau kwa wahamasishaji?

LGE2024 Nini kimetokea kiasi kwamba Wananchi hawataki kujiandikisha hadi wanafatwa majumbani na wanatoa majibu ya dharau kwa wahamasishaji?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kabla ya mwaka 2015 kulikuwa na mwamko mkubwa sana kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutimiza adhima yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka.

Kuanzia 2010 hadi 2015 ulizuka msemo unaitwa Kichinjio. Yaani kadi ya mpiga kura ambapo mwenye nayo anaamua kumkatilia mbali Diwani, Mbunge au Rais anayeonekana hafai kwenye uongozi.

Wananchi walijivunia sana Viparata vyao is it" vichinjio" Ilikuwa hakuna kusukumana kwenda kujiandikisha.

Ghafla bini vuu wananchi wamesusa. Yaani imefika mahala hata ukiwapa rushwa hawaendi Ng'oo

Tutafakari kama taifa nini kimetokea? Je, uzalendo utatoka wapi ikiwa wananchi wanakwama kushiriki mambo ya kitaifa mepesi kama haya?

Je, tunaweza kufikia level ya uzalendo wa Wananchi wa Israel, Irani, Lebanoni au China?
Jana huko nyanda za juu Kusini, kuna kijiji fulani Afisa Mtendaji wa kijiji, karani na wakala wa chama tawala, walikuwa wanapita nyumba kwa nyumba hadi saa 2.30 usiku.

Karani mwanamke mwenye majukumu ya kifamilia, tangu aanze kazi saa 2 asubuhi kahenyeshwa hadi saa 2.30 usiku. No allowance.
 
No allowance kivipi ..karani analipwa 30,000/= Kwa siku ... Siku 10 ni 300,000/= ya bure kabisa. Na makarani wote ni watumishi ... Haujiulizi Kwa Nini Tamisema imetaka makarani wote wa daftari la Uchaguzi wa Serikali za mitaa wawe watumishi!??.....
 
Allowance hiyo ni ya saa za kazi zilizoainishwa na kwa kukaa kwenye kituo kilichopangwa, siyo kutembea ana wala muda wa ziada kuanzia saa 12 jioni hadi huo muda wa saa 2.30 usiku.
 
Allowance hiyo ni ya saa za kazi zilizoainishwa na kwa kukaa kwenye kituo kilichopangwa, siyo kutembea ana wala muda wa ziada kuanzia saa 12 jioni hadi huo muda wa saa 2.30 usiku.
Huo ni ubwege wake ..... Wewe umepewa kituo kaaa kituoni.... Tunaenda kutembeza fuvu Ili iweje....
 
No allowance kivipi ..karani analipwa 30,000/= Kwa siku ... Siku 10 ni 300,000/= ya bure kabisa. Na makarani wote ni watumishi ... Haujiulizi Kwa Nini Tamisema imetaka makarani wote wa daftari la Uchaguzi wa Serikali za mitaa wawe watumishi!??.....
Kwa mazingira kama haya ni dalili tosha kwamba hakutakuwa na uchaguzi huru kabisa.

Vyama vya upinzani huwa wananishangaza sana, wanakubali kushiriki uchaguzi ambao mazingira yanaonyesha wazi kwamba wameshashidwa kabla hata ya uchaguzi wenyewe.
 
Maisha ni ushindani, binadamu tumeumbwa na kaushindani fulani hivi ndo asili. Upinzani wakisusa, wananchi wakisusa, CVM watakosa radha, watapoa - huna mtu wa kumwamwia sera zako na uongo, yaan nobody cares- automatically nao wataanza kukata moto - nao wataona havina maana - watasusa bila kujitambua, haijalishi hata mtu akapata uongozi fake, akaiba, akajilimbikizia mali - maisha na raha ya siasa na ubinadamu ni hekaheka - Angalia US watu wanavyopashana - watu wanaongea - watu wanasemana - wanaongea sera zao - wanaenda kwenye midahalo - watu wanashindana - inaleta utamu fulani hivi na ukamikifu wa kibinadamu.
Angalia kwetu sasa - kwanza hakuna kinachofanyika cha maendeleo mtaani huku ( ni hili sio kosa lao) waani viongozi wa serikali ya mtaa hata barabara kidogo tu ikaharibiwa na mvua - hawana uwezo wa kurekebisha, usafi chali, yaani hawana influence ya moja kwa moja, mazingira mabovu, ujenzi holela - HAWA viongozi wa serikali za mitaa hawasaidii moja kwa moja wananchi kikubwa wanakuwa ni kama extension ya executive tu: Kuwa mashushu na wambea, kuandikisha zile barua za kwenda kufungua akaunti, kuchukua 10% za mauzo ya ardhi - kusainisha mikataba ambalo sio hata jukumu lao, kuwa madalali, kuwa mahakama ndogo - kusuruhisha ikishindikana wanapiga kimya, ofisi zao wenyewe zinatia huruma, unaenda ofisi ya serikali ya mtaa unakuta mara mibendera ya vyama vya siasa hasahasa CCM, viti na meza vilovyojichokea, watu waliochoka kuanzia taswira mpaka uhalisia wa maisha n.k.
Mtu anaweza maliza miaka 5 hajawahi kumuona na hamjui hata kiongozi wa serikali ya mtaa na hana.Hivi kwa mzingira hayo hawa vijana wa siku hizi wataheshimu kweli uchaguzi wa kuwaweka hao madarakani, na tunakoelekea na uchaguzi huu utaendelea kudharaulija mpaka ujifie kabisa.
Na ndo maana huwezi ona vijana wenye mawazo mapya wanapambana et awe mteule wa mtaa - watu wanapambana waingie bungeni - wapige perdiem, wanapambana waingie serikali kuu - wapate mav8 n.k.
Mpaka pale tutakapopata katiba itakayoempower watu wa chini ndo na hizi chaguzi zitakuwa na maana.
Nchi yetu inasikitisha sana - inauma sana - viongozi wetu hawajali na ni kama hawajui kusolve matatizo au sijui ni uelewa?? Ni kama wao wanaulimwengu wao na wananchi wanaulimwengu wao.
Pale ambapo tutawezs kuepower watu huku chini kabisa, watu wafanye na wawe na uwezo wa kujifanyia maendeleo yao madogo madogo ndo tutapata maendeleo kama taifa na uzalendo, otherwise kila mtu aendelee kugombania goli- ale alipo mpaka siku akili zitukae sawa.
 
Huwezi kua na akili timamu ukafanya kosa lile lile kila siku, Kujiandikisha na kupiga kura kwa katiba na tume ile ile ni Kosa la makusudi ambalo majuto yake ni Kilio cha mjinga mlevi aliechoka na mwendo.

Watu wanazunguka tu, ila huu ndo ukweli, walete katiba mpya, tume huru ya uchaguzi watu wataenda kupiga kura, na siyo kutuletea mazingaombwe hapa,
 
Wanaojiita wapinzani nao hatuwaoni kwenye zoezi hili....watakuja baadae sana kwenye kutangaza matokeo wanajifanya kura zao zimeibiwa!
 
Huku kwetu hata wakifuatwa wanataka walipew kwanza ndo wajiandikishe. Wachache wanaojitokeza wanahitaji kupata vitambulisho kwa ajili ya mambo Yao japo zoezi lenyewe sio la vitambulisho. Kazi ipo!
Tuendelee kuwaelimisha
 
Back
Top Bottom