Nini kimewapelekea viongozi wa Simba kumsajili mshambuliaji Mcameroon Lionel toka USM Algiers?

Mkuu kuna namba 9 wangapi pale Simba ambao hawapewi nafasi na muda ? Na kama waliona ilo kwanini walimuacha Freddy na na kumbakisha goalkeeper Ayoub Lakred maana saivi ni useless tu na inawapa shida kuamua nani atoke
 
Kama Kibu Dennis hakushiriki preseason ya klabu lakini viongozi wamelazisha acheze tu
Hakika hao viongozi wa Simba wanayumba.
MUKWALA- ni bonge la striker, kwanini wamemkatia tamaa kabla hata hajacheza mechi ya league
 
Mukwala hajakatiwa tamaa, fredy ndo amekatiwa tamaa na kocha na hayupo kwenye mipango ya mwalimu analetwa mshambuliaji mwingine wa kusaidiana na Mukwala
Mukwala mchezaji mzuri anahitaji vitu vichache sana kumuongezea awake, ila kwa Freddy na uyo mpya Lionel ndio wasiwasi wangu upo .
 
Hii ni inaweza kuwa na sababu nyingi lakini kwangu naona 1-viongozi wanapuuzia maoni ya mashabiki
2-Maslahi binafsi ya viongozi kwa mchezaji
3-Kelele za wachambuzi mchele wa bongo
Nilisha sema humu na kupendekeza nini kifanyike 1 Tatizo la simba ni wanachama hawana uwezo wa kuwajibishana viongozi na muwekezaja. yaani timu ilishanunuliwa, pia wanachama walisha sahau kuichangia timu kama waliambiwa wasichangie ndiyo sababu ya wanachama kutokuwa na sauti
 
 

Mkuu ayo ni mapendekezo au umetoa sababu?? Nafikiri cha kufanyika ni ushirikiano tu na maoni ya mashabaki na wanachama yaheshimiwe na kufanyiwa kazi ipasavyo pia kuweka team sahihi ya scout na kuachana na wachezaji wa kuletewa toka kwa mawakala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…