Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Du hii noma nikadhani alivoambiwa na madaktari walikuwa wanamtania kumbe kweli hata humu napata jibu hilo hilo
 
Mwanamke 1 katika wanawake 3 hupatwa na tatizo la kuvuja damu nyingi wakati za siku zao. Hata hivyo, mara nyingi ni vigumu kujua kama mwanamke anatoka damu nyingi au kawaida

ikilinganishwa na wanawake wengine wakati wa hedhi. Baadhi ya wanawake ambao wanahisi kuwa huvuja damu nyingi wakati wa siku zao hakika wanapoteza damu kiasi cha wastani.Baadhi ya wanawake ambao wanaona kuwa wanapoteza kiasi cha kawaida huwa wanapoteza damu nyingi.

Ufafanuzi

mzunguko wa kawaida - upotevu wa damu hukadiriwa kuwa kati ya mls 20 na 60 (vijiko vya chai 4-12 ). Kutokwa na damu inaweza kudumu hadi siku nane, lakini wastani ni siku tano .

Kutoka damu nyingi - upotevu wa damu ni kati ya mls 60-80 au zaidi. Hii ni kama nusu kikombe au zaidi. Hata hivyo, ni vigumu kupima kiasi cha damu ambacho kinapotea wakati wa mzunguko. Lakini unaweza kutambua kama unavuja damu nyingi iwapo :

-Damu zinafurika na kulowanisha nguo au matandiko.
-Unahitaji kubadilisha mara kwa mara kitambaa au pedi.
-Unahitaji vitambaa au pedi mbili au zaidi.
-Unapata damu zenye mabonge .

Menorrhagia ni hali ya kuvuja damu nyingi kila mwezi mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Pia, damu inayovuja inaweza kuathiri ubora wa maisha . Kwa mfano,hufanya mwanamke kushindwa kufanya shughuli zake za kawaida kama vile kufanya kazi au kwenda shuleni.

Sababu.
Mara nyingi sababu haijulikani. Lakini magonjwa yafutayo yanaweza kusababisha mwanamke kuvuja damu nyingi
-Dysfunctional uterine bleeding-katika tatizo hili mwanamke huvuja damu bila kuwepo ugonjwa wowote katika mfuko wa mayai. Inadhaniwa kuwa chemikali iitwayo prostaglandin inaweza kuchangia tatizo hili. Linatokea katika miaka ya mwanzo baada ya kuvunja ungo.
-Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi
-maambukizi kwenye kizazi
-matatizo ya hormoni
-saratani ya kizazi hasa kwa wanawake wenye umri mkubwa.
-kitanzi(IUD)-hiki ni kifaa kinachowekwa kwa utaalamu kwenye mfuko wa kizazi.
-Dawa mfano dawa za kutogandisha damu,matibabu ya saratani nk

Uchunguzi
Vipimo mbalimbali vinaweza kuhitajika ili kujua sababu ya kuvuja damu nyingi wakati wa hedhi mfano ultrasound,kipimo cha hormoni na wakati mwingine uchunguzi hufanywa kuangalia kama kuna tatizo lolote wakati mwanamke amepewa dawa za usingizi.

Matibabu
Matibabu ya msingi hutegemea dalili na chanzo cha tatizo. Hata hivyo daktari anaweza kuanza kutibu dalili wakati akiendelea na uchunguzi.

Last edited by a moderator:
Pole sana dear wangu

  1. Ulikua katika dozi yoyote ya dawa?
  2. Umebadili mazingira?
  3. Kwa kawaida mzunguko wako ni wa siku ngapi? Au ni wa namna gani(regular or irregular)
 
My dia pole........ila umewahi kumwona dactari.....

Nimewahi kusikia pia vidonge vya uzazi wa mpango

huwa inasababisha pia khali hii,imekutokea mara nyingi !!!!!

Ni mara ya kwanza inatokea........
Sijawahi tumia hayo mavitu mamii tokea kujitambua kwangu.

Hayo mavitu nayaogopa ile mbaya
 
Pole sana dear wangu

  1. Ulikua katika dozi yoyote ya dawa?
  2. Umebadili mazingira?
  3. Kwa kawaida mzunguko wako ni wa siku ngapi? Au ni wa namna gani(regular or irregular)

Asante mamii.......

Huwa niki bleed km tarehe 5 mwez huu bas mwez ujao waweza kuwa tarehe hyo hyo au ikarud nyuma siku moja o 2.

Hapana mazingira sijabadilisha na pia hakuna doz natumia mamaa.
 
Bi dada japo huwa navaa suruali ila ujuzi hauna mipaka...kuna sababu anuai za hali hii kutokea! Yumkini umebadili mazingira uliyokuwa unaishi kigeografia ama kupata na msongo wa mawazo karibuni! Pia kuna matumizi ya madawa/kemikali ambazo hii inaweza kuwa mojawapo ya side effect! Muhimu ni kuwaona wataalamu wa kitabibu kabla hali haijawa ya kudumu!
 
ni hali ya kawaida tu hiyo wala sio tatizo linalo hitaji utabibu,
simply ni kwamba ulikuwa na multiple maturation ya ova na amabzo ziliforce endometrium thickening kwa haraka kabla mzunguko haujaisha.

uzuri uterus inajins ya kujilinda so ilipoona endometrium imekuwa thick ilibidi erosion ifanyike. sio kitu kipya labda kwakua ndio umeona kwa mara ya kwanza kwako.

linekuwa ni tatizo la kitabibu kama damu yake inakuja na maumivu makali halafu ni dysfunctional yaani inatoka tu bila sababu unajikuta mwezi mzima bado inatoka tu.

Hata hivyo nikupe hingera kwamba bado u-kigori
 
Thanks kwa ushaur wako.......kuhusu msongo wa mawazo hapana kwa sasa maana nipo kawaida tu.Ntacheck hali mpk kesho then fasta ntakwenda hospitali
 
Asante dada gfsonwin......
Ni kweli mara ya kwanza imenitokea,nashukuru kwa ushaur wako ingawa wakitaalamu sana.
 
Last edited by a moderator:
Asante dada gfsonwin......
Ni kweli mara ya kwanza imenitokea,nashukuru kwa ushaur wako ingawa wakitaalamu sana.

hapo bold sasa ulitaka uwe wa aina gani??
kumbuka afya haina njia nyingine lazima useme ukweli tu.
huwez ukaliita jicho pua.
huna tatizo mwaya relax na endelea na maisha yako ya kawaida mumie!!
 
Thanks kwa ushaur wako.......kuhusu msongo wa mawazo hapana kwa sasa maana nipo kawaida tu.Ntacheck hali mpk kesho then fasta ntakwenda hospitali

Pole lakini...kuwa mwanamke ni issue sana,mama yangu mwanamke najua...na namheshimu sana huyu bi dada wa zamani japo alinitwanga sana kwa makosa ambayo mengine aliover look! Nikiona mwanume anayempiga mwanamke huwa nafikiri alijizaa mwenyewe! Quote me!
 
hapo bold sasa ulitaka uwe wa aina gani??
kumbuka afya haina njia nyingine lazima useme ukweli tu.
huwez ukaliita jicho pua.
huna tatizo mwaya relax na endelea na maisha yako ya kawaida mumie!!

Nashukuru dada......Mungu akubariki sana!!!
 
Pole lakini...kuwa mwanamke ni issue sana,mama yangu mwanamke najua...na namheshimu sana huyu bi dada wa zamani japo alinitwanga sana kwa makosa ambayo mengine aliover look! Nikiona mwanume anayempiga mwanamke huwa nafikiri alijizaa mwenyewe! Quote me!

Asante sana.....Mungu na akubariki na uzid kuheshimu wanawake
 
pole my twin. mie sina utaalamu katika hilo. labda umsome Chocs hapo juu. kama hakuna katika hayo basi nikuitie MziziMkavu aje labda atatusaidia.

Asante sana pacha wangu.....Subir watakuja walioxperience hii kitu watazid kushaur na huenda ukajifunza kitu pia kwa faida ya baadae!!!!
 
Last edited by a moderator:
Habar wana Jf.........
Tarehe 21 ya mwez uliopita nilimaliza hedhi yangu lakin kinachonishangaza jana tarehe 6 nmeanza kupata siku zangu.
Naombeni ushaur wenu jaman maana haijawahi tokea hali hii!!!!!!

Je kufululiza kunywa ulabu inaweza ikawa sababu???
Naomben ushaur wenu
Heaven on Earth, DEMBA, Madame B, Chocs, Karucee, mimi49, Smile, atug, charminglady, ladydoctor, Kongosho, Mamndenyi na wana jf kwa ujumla!!!!

Pole sana mamie... Ngoja tuwaite MaDr waje....

Wapi Dr. Riwa, MziziMkavu, mimi49 na mummy measkron....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom